Tafuta

kiongozi wa Suda Kusini KIIR kiongozi wa Suda Kusini KIIR 

Sudan Kusini:Maaskofu wanaomba mamlaka kuwaajibisha wahalifu

Ni mwezi umepita tangu watawa wawili sudan Kusini wauawe lakini bila wahusika.Tunakataa maneno ya watu wasiojulikana wenye silaha yaliyoelezwa na mamlaka.Ni wito wa maaskofu kuhusiana na tukio la mauaji nchini humo baada ya mwezi hakuna uchunguzi wowote uliofanywa.Jumuiya mahalia inawajua wahalifu hao ni nani,ambao wanaruhusiwa kukimbia bila adhabu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Sudan Kusini tarehe 16 Agosti 2021, katika barabara ndefu kati ya mji mkuu wa Juba na ule wa Nimule mpakani mwa Uganda kuiliibuka kwenye kichaka kikundi cha watu wenye silaha ambao walivamia Bus na ndani kulikuwa  na watawa na waamini katoliki. Katika mapambano hayo watu watano walikufa katika uvamizi huo, wakiwemo watawa wawili, Sr. Maria Abud na Sr. Regina Roba, wote wakiwa wa Shirika la Moyo Mtakatifu. Mwezi mmoja baada ya vifo vyao hadi sasa wahalifu hao bado hawajatambuliwa na wala hawajaweza kufikishwa mahakamani. Kwa maana hiyo, maaskofu wa eneo hilo wanalalamikia kutokana na ukosefu wa maendeleo katika uchunguzi, huku wakizindua wito wa kutafuta haki itendeke haraka iwezekanavyo.

Maaskofu wanaalani tendo la kutojali kile kilichokea katika barua yao ya tarehe 15 Septemba, wakiomba kwamba wahalifu hao watambuliwe na wawajibishwe kwa matendo ya uharifu wao. “Tunakataa maneno ya watu wasiojulikana wenye silaha yaliyoelezwa na mamlaka”, maaskofu wamesititiza. Jumuiya mahalia inawajua wahalifu hao ni nani, ambao wanaruhusiwa kukimbia bila adhabu. Maaskofu pia wana wasiwasi kuwa msiba huu unaweza kuficha jaribio la kuzuia mchakato wa amani nchini humo. Taifa hili la Kiafrika, kwa hakika limepondwa na mivutano ya kudumu ambayo ilizidi kuwa mbaya mnamo 2013, wakati wafuasi wa Rais Salva Kiir, wa kabila la Dinka, na wale wa Mkuu wa zamani wa Jimbo Riek Machar, wa kabila la Nuer, walipoanza mgongano. Mzozo mkubwa uliacha vifo na uharibifu nchini humo na waathrika 400,000 na wakimbizi milioni 4 na watu waliokimbia makazi yao.

Miaka mitano baadaye, mnamo 2018, makubaliano yalifikiwa ya kumalizika kwa vita, Mkataba uliofufuliwa juu ya Utatuzi wa Migogoro huko Sudan Kusini (R-ARCSS), wakati mnamo Februari 2020 vikundi vya kisiasa vilifikia makubaliano ya uundwaji wa serikali mpya ya mpito ya umoja wa kitaifa, inayoongozwa na Kiir na upinzani Machar. Lakini matokeo halisi hayafiki na vurugu zinaendelea, pia zikiathiri viongozi wa dini. Mwezi Aprili uliopita, kiukweli, askofu wa RumbekPadre Mkomboni Christian Carlassare, alipigwa risasi miguu na wanaume wasiojulikana.

Kwa mujibu wa Sr Alice Jurugo Drajea, mkuu wa Shirika wa Masista wa Moyo Mtakatifu wa Yesu, alionesha maskitiko yake kuhusiana na suala hili la ukosefu wa majibu kutoka kwa serikali ya kitaifa: “Hadi sasa hatujapata sasisho ​​dada zetu wamekufa kama watu wengine wowote wale. Katika nchi hii, kuuawa ni kama jambo la kuzaliwa: ni kawaida. Kwa hivyo, kumbukumbu inayogusa ya watawa wawili na ushuhuda wao,  Mary na Regina walifariki wakati wa hija kuelezea imani yao. Hao ndio mashuhuda wapya wa Sudan Kusini. Tunahisi kuimarika katika kujitolea kwetu kuendelea na kazi ya Mungu kwa watu”.

Hata Baba Mtakatifu Francisko, katika telegramu iliyosainiwa na Katibu wa Vatican Kardinali, Pietro Parolin, aliyetuma mnamo Agosti 17 kwa Askofu Mark ubalozi wa Kitume huko Sudan Kusini, alelezea kusitikita sana kujua juu ya shambulio la kinyama lililosababisha kifo cha watawa wawili. Baba Mtakatifu alielezea salamu zake za rambirambi kwa familia na jumuiya nzima ya kidini kwa kitendo hiki cha vurugu kisicho na maana. Na alisema alikuwa na imani kwamba sadaka yao itaendeleza sababu ya amani, upatanisho na usalama katika kanda hiyo. Kwa upande mwingine, Papa amekuwa akijitolea sana kwa ajili ya Sudani Kusini: ahadi ambayo ilitekelezwa tarehe 11Aprili 2019, na wito wa mafungo ya kiroho katika nyumba ya Mtakatifu Marta na ambayo Salva Kiir na makamu wa rais waliochaguliwa walishiriki. Tukio hilo kutoka mbali, na ambalo kwa hakika liliweka alama na ishara muhimu sana. Itakumbukwa siku hiiyo Papa Francisko alipiga magoti na kubusu miguu ya wanasiasa, akiomba amani kwa nchi hiyo changa ya Afrika.

18 September 2021, 16:55