Kanisa la Ulaya linawaombea wahanga wa tetemeko la ardhi huko Uturuki na Siria
Na Angella Rwezaula; - Vatican.
Kutoka jiji la Praga ambako mkutano awamu ya Pili ya kibara kuhusu mchakato wa Sinodi uunaendelea ulioanza tarehe 5 Februari, Makanisa barani Ulaya kutoka na janga wameonesha ukaribu wao na wakazi wa maeneo ya kusini mwa Uturuki na kaskazini mwa Siria walioathiriwa sana na tetemeko la ardhi lilitokea usiku wa tarehe 6 Februari iliyopita. Hadi sasa idadi kubwa ya vifo inazidi kuongezeka pamoja na idadi inayokusudiwa kuongezeka zaidi na uharibifu, mateso ya watu wengi ambayo yameathiri sana na kugusa roho zao. Washiriki wa Mkutano huo wamebainisha kwamba “hili ni jeraha kubwa, ambalo nchini Siria linaongezwa na lile la vita vinavyoendelea katika eneo hilo kwa miaka 12 sasa”.
Katika taarifa yao, wamebainisha kwamba “Tuko karibu na jumuiya Vikarieti ya Iskenderun, ambapo iliona kanisa lake kuu likiharibiwa, lakini kwa bahati nzuri bila kulipa gharama katika maisha ya binadamu. Mawazo yetu yanaenda kwa Vicariati ya Anatolia, ambayo inakabiliwa na hali ngumu ya uharibifu. Kwa hiyo hebu tutazame Aleppo, mji ambao uliuawa kishahidi kwa vita huko Siria na ambao sasa unapitia mauaji haya zaidi ya kishahidi”.
Washiriki wa mkutano wa kibara huko Praga katika tamko lao aidha amebainisha kwamba “.Zaidi ya yote, mawazo na shukrani zetu zinakwenda kwa wale ambao kwa sasa wanaleta juhudi za usaidizi, katika hali ngumu sana, na joto la msimu wa baridi. Caritas yetu imejitolea kushughulikia dharura, kutibu majeruhi, kuwafariji waliopoteza wanafamilia, kutafuta paa kwa wale ambao hawana tena. Makanisa mahalia tayari yanatoa kila aina ya usaidizi na makaribisho, na ni mfano mzuri ambao tunautazama kwa kustaajabisha. Kwa hisia, Makanisa yaliyoko Ulaya hukusanyiji na ukaribu na watu waliokumbwa na tetemeko la ardhi, wakifanya kwa upya maomo yao na kutangaza kama sasa kila msaada unaowezekana kushughulikia dharura”.