Tafuta

Papa Francisko:Kitu msingi ni kuwakaribisha maskini&wasioweza kurudisha

Kwa mtazamo wa Mungu,thamani ya mtu haipimwi na jukumu analojikita nalo, wala mafanikio,fedha katika benki,ni katika huduma.Papa Fransisko katika Tafakari kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana amesisitizia umuhimu wa ubora wa kuwa mtumishi unaogharimu na mara nyingi unahitaji juhudi inayotambua msalaba na ukaribu na Mungu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Katika Dominika ya Tatu ya Mwezi,  tarehe 19 Septemba 2021, Papa Francisko ametoa tafakari yake kwa waamini na mahujaji waliofika katika uwanja wa Mtakatifu Petro kusali naye sala ya Malaika wa Bwana. Kabla ya sala hiyo Papa Francisko amesema: “Injili ya siku kutoka Marko 9,30-37 inasimulia kuwa katika safari ndefu kuelekea Yerusalemu, mitume wa Yesu walikuwa wanajadiliana ni nani kati yao angekuwa mkubwa (Mk 9,34). Yesu akawageuki wao kwa sentensi  kali, ambayo inastahili hata kwetu sisi leo hii. “Mtu atakayetaka kuwa wa kwanza atakuwa wa mwisho kuliko wote na mtumishi wa wote. (Mk 9, 35). Ikiwa unataka kuwa wa kwanza lazima uende mwisho na uwe wa mwisho ili kuhudumia wote. Wakati wa kutamka sentensi hii kwa haraka, Bwana anazindua mabadiliko, kwani anapenda mantiki ambayo inaonesha ni kitu gani kilicho muhimu na kinacho hesabika kweli. "Thamani ya mtu haitegemei zaidi na nafasi anayofunika, ya mafanikio aliyo nayo, ya kazi anayoifanya, ya fedha alizo nazo kwenye Banki; Hapana! haitegemei hilo. Ukuu wake na uwezekano mbele ya macho ya Mungu vina kipimo tofauti; ambavyo hupimwa kutokana na huduma. Si katika mambo aliyo nayo lakini ni katika yale ambayo anatoa. Ninyi mnataka sifa? Muwe watumishi". Hii ndiyo njia! Papa amesisitiza.

Katika  tafakari hiyo, Baba Mtakatifu Francisko amebainisha kuwa, leo hii, neno huduma, linaonekana kidogo kuisha wakati, kuzeeka katika matumizi yake. Lakini katika Injili, lina maana kubwa na ya dhati. Kuhusu huduma  si  kielelezo cha utafadhali; ni kufanya kama Yesu ambaye kwa ufupi wa maneno ya  maisha yake alisema kwamba amekuja si kwa ajili ya kuhudumiwa bali kuhudumia (Mk 10,45). Hivyo ndivyo alisema Bwana, Papa amesisitiza. Kwa njia hiyo ikiwa tunataka kumfuata Yesu, lazima kupitia katika njia ambayo Yeye mwenyewe alionesha,  ni  njia ya huduma. Uaminifu wetu kwa Bwana unategemea na uwezekano wetu wa kuhudumia.  Na hiyo tunatua ni kwa jinsi gani mara nyini inagharimu kwa sababu inatambua  Msalaba. Lakini wakati  huduma inaongezeka ya matendo ya utunzaji na uwezekano kwa ajili ya wengine, ndipo  inageuka kuwa rahisi na  uhuru wa ndani na kufanana na Yesu. Kadiri tunavyohudumia zaidi ndivyo tunatimiza uwepo wa Mungu. Hasa ikiwa tunahudumia ambaye hawezi kuturudishia, kama vile maskini, kwa kukumbatia matatizo yao na mahitaji yao kwa upole na huruma; hapo tunagundua uwepo wake.

Yesu mwenyewe kwa kuonesha hili, baada ya kuzungumzia juu ya ukuu wa huduma, alitimiza ishara Papa amebainisha.  "Tuliona kuwa ishara za Yesu ni zenye nguvu zaidi ya maneno anayotumia. Je ni ishara ipi? Akatwaa kitoto, akamweka katikati, akamkumbatia akawambia: Mtu akimpokea mtoto mmoja wa namna hii kwa jina langu anipokea mimi na mtu akinipokea mimi, humpokea si mimi bali yeye aliyenituma ( MK 9, 37)". Papa ameongeza kusema: “tazama awali ya yote ni yule anaye hudumia., kwani je ni wangapi wanahitaji kupokea na hawana cha kurudisha?. Kuhudumia wale wenye kuhitaji kupokea lakini hawana cha kurudisha. Anayempokea aliye pembezoni, anayebaguliwa, anampokea Yesu mwenyewe, kwa sababu Yeye yuko hapo. Yupo katika aliye mdogo, yupo kwa maskini ambao tunawahudumia, tunapokea hata sisi mkumbatio wa upole wa Mungu.

Papa Francisko  akiendela na tafakari amebainisha kwamba kwa kualikwa na Injili hii tujiulize maswali: Mimi, ninayemfuata Yesu, ninajihusiha  na nani anayepuuzwa zaidi? Au, kama wanafunzi wa siku hiyo, je! Ninatafuta raha ya kibinafsi? Je! Ninaelewa maisha kama mashindano ya kujipatia nafasi kwa hasara ya wengine au nadhani kuwa ubora kunamaanisha kutumikia? Na, kwa dhati: je! Mimi ninajitolea wakati wangu mdogo kwa ajili ya mtu ambaye hana njia ya kurudisha? Je! Mimi niangalia mtu ambaye hawezi kunirudisha au tu jamaa na marafiki zangu? Haya ni maswasli ambayo tunaweza kujiuliza, Papa ameshauri. Kwa kuhitimisha amesema, "Bikira Maria, mnyenyekevu na mtumishi wa Bwana, atusaidie kutambua kuwa kuhudumia hakutupunguzi, badala yake ni kunatufanya tukue. Na kwamba kuna furaha zaidi ya kutoa kuliko kupokea (Mdo 20, 35)".

TAFAKARI YA PAPA DOMINIKA 19 SEPTEMBA
19 September 2021, 13:28