Tafuta

Papa Francisko:Wahusika wawe mstari wa mbele kwa ajili ya amani

Baba Mtakatifu mara baada ya Misa Takatifu,Dominika tarehe 15 Mei ambapo amewatangaza watakatifu 10 ametoa wito kwa mara nyingine kufuata njia ya mazungumzo hasa katika mioyo na akili ya walio na majukumu makubwa na kwamba"wanaalikwa kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya amani na sio vita".

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Misa Takatifu, Dominika tarehe 15 Mei 2022 ambapo Baba Mtakatifu Francisko amewatangaza watakatifu kumi ametoa wito kwa mara nyingine “kufuata njia ya mazungumzo hasa katika mioyo na akili ya walio na majukumu makubwa kwahiyo wanaalikwa kuwa mstari wa mbele kwa ajili ya amani na sio vita”.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15

Baba Mtakatifu Francisko amesema kuwa kabla ya kumalizia maadhimisho ya Ekaristi amependa kuwasalimia na kuwashukuru wote kuanzia na ndugu Makardinali, Maaskofu, mapadre, watawa wa kike na kiume hasa wale ambao wanashiriki familia za kiroho za Watakatifu Wapya na waamini wote, Watu wa Mungu waliofika kwa wingi kutoka pande za ulimwengu.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15

Baba Mtakatifu aidha amewashukuru Wawakilishi maalum kutoka Nchi mbali mbali na kwa namna ya Pekee , Rais wa Jamhuri ya Italia Bwana Sergio Mattarella.  "Ni Vizuri kutambua kuwa kwa ushuhuda wao wa kiinjili, watakatifu hao walisaidia kukuza kiroho na kijamii, kwa mataifa mbali mbali hata katika familia nzima ya kibinadamu".

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15

Papa Francisko amebanisha: "Wakati huzuni mkubwa katika ulimwengu unazidi kuongezeka mivutano na vita, kwa umbali, Watakatifu wapya walihamasisha ufumbuzi wa kwa ujumla, njia za mazungumzo, hasa katika mioyo na akili za wale wanaoshikilia nyadhifa za uwajibikaji mkubwa na wanaoitwa kuwa wahusika wakuu wa amani na sio ya vita”.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15

Kwa kuhitimisha amewasalimia wote, mahujaji na wale wote waliofuatilia misa kipitia vymbo vyote vya mawasiliano. Na baadaye wakasali pamoja salamu Malkia ili Mama Maria atusaidie kuiga kwa furaha mdano wa Watakatidu wapya.

Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
Kutangazwa watakatifu kumi Mei 15
WITO WA PAPA KWA AJILI YA AMANI
15 May 2022, 11:52