Tafuta

2022.11.26 Papa amekutana na Washiriki wa Kumtano wa Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kiume(U.S.G.) 2022.11.26 Papa amekutana na Washiriki wa Kumtano wa Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya kiume(U.S.G.)  (Vatican Media)

Papa kwa watawa:kuwa na mamlaka yasipunguze usikivu kwa wengine

Katika hotuba iliyokabidhiwa kwa Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya Kitawa(USG),walioshiriki Mkutano 23- 25 Novemba,Papa anawashauri wawe mafundii wa amani na kutoa mfano kwa Kanisa umoja na kisinodi.Wawe makini dhidi ya hatari ya mitindo ya kimabavu katika madaraka ya jumuiya za kitawa,ili isiwe dhuluma.Watembea pamoja na kuthamini za karama za kila mmoja.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko amekutana  mjini Vatican  Jumamosi tarehe 26 Novemba 2022 na washiriki wa Mkutano wa Umoja wa Wakuu wa Mashirika ya watawa (U.S.G) uliofanyika kuanzia tarehe 23-25 Novemba Roma, ambao amewakaribisha wote wakiwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume na kumshukuru Padre Arturo Soza kwa hotuba yake. Katika hotuba yake aliyokuwa ameandika amewakabidhi wajisomee kwa  kupendelea kuzungumza bila kusoma. Kwa maana hiyo ifuatayo ni hotuba yaliyowakabidhi ambapo Baba Mtakatifu ameandika kwamba Mkutano wao umeongozwa na Kauli mbiu ya Waraka wa Fratelli Tutti yaani Wote ni Ndugu na kukabiliana na  suala la kualikwa kuwa mafundi wa amani. Huu ni wito wa dharura ambao unatutazama wote kwa namna ya pekee watawa, ya kuwa mafundi wa amani, wa ile amani ambayo Bwana alitupatia na anaendelea kufanya wahisi ndugu wote. “Yeye alisema “Ninawachia amani, ninawapa amani. Sio kama dunia inavyowapatia, mimi ninawapatia ninyi” (Yh 14,27).

Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G
Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G

Ni amani gani ambayo Yesu anatupatia, nayo inatofautianaje na ile ambayo ulimwengu hutoa? Katika nyakati hizi, kusikia neno “amani” tunafikiri juu ya yote yasiyo ya vita au hali ya mwisho wa vita, hali ya utulivu na ustawi. Hii  tunajua  hailingani kikamilifu na maana ya neno la Kiebrania shalom, ambalo, katika muktadha wa kibiblia, lina maana tajiri zaidi. Amani ya Yesu kwanza kabisa ni zawadi yake, tunda la upendo, kamwe si ushindi wa mwanadamu; na, kuanzia karama hiyo, ni uhusiano mzima wenye upatanisho na Mungu, mwenyewe, na wengine na kazi ya uumbaji. Amani pia ni uzoefu wa huruma, msamaha na ukarimu wa Mungu, ambao nao unatuwezesha kudhihirisha huruma, msamaha, kukataa aina zote za unyanyasaji na uonevu. Ndiyo maana amani ya Mungu kama zawadi haiwezi kutenganishwa na kuwa wajenzi na mashuhuda  wa amani; Kama Waraka wa Fratelli tutti usemavyo, “wasanii wa amani walio tayari kuanzisha mchakato wa uponyaji na kukutana upya kwa werevu na ujasiri” (n. 225). Kama Mtakatifu Paulo anavyotukumbusha, Yesu alibomoa ukuta wa uadui uliogawanyika kati ya wanadamu, akiwapatanisha na Mungu (rej. Efe 2:14-16). Upatanisho huu unafafanua njia za kuwa “wapatanishi” (Mt 5:9), kwa sababu hiyo  kama tulivyosema kwamba  sio tu kutokuwepo kwa vita au hata usawa kati ya vikosi vinavyopingana (taz. Gaudium et spes, 78). Badala yake, msingi wake ni utambuzi wa hadhi ya  mwanadamu na unahitaji utaratibu ambao haki, huruma na ukweli vinapatana bila kutenganishwa (taz. Fratelli tutti, 227).

Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G
Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G

Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu anaandika kwamba “kufanya amani” ni kazi ya ufundi, inayopaswa kufanywa kwa shauku, uvumilivu, uzoefu, ushupavu, kwa sababu ni mchakato unaoendelea kwa wakati (taz. Ft 226). Amani si bidhaa ya viwanda bali ni kazi inayotengenezwa kwa mikono. Haijaumbwa kikarakana, inahitaji uingiliaji wa busara wa mwanadamu. Haijajengwa kwa mfululizo, na maendeleo ya teknolojia tu, lakini inahitaji maendeleo ya binadamu. Kwa sababu hiyo michakato ya amani haiwezi kukabidhiwa kwa wanadiplomasia au wanajeshi: amani ni jukumu la mtu mmoja na wote. “Heri wapatanishi” (Mt 5:9). Heri sisi watu waliowekwa wakfu ikiwa tunajitolea kupanda amani kwa matendo yetu ya kila siku, kwa mitazamo na ishara za huduma, udugu, mazungumzo, huruma; na ikiwa katika sala tunaomba bila kukoma kutoka kwa Yesu Kristo “amani yetu” (Efe 2:14) zawadi ya amani. Hivyo maisha ya kitawa yanaweza kuwa unabii wa karama hiyo, ikiwa watu waliowekwa wakfu watajifunza kuwa mafundi wake, kuanzia na jumuiya zao wenyewe, wakijenga madaraja na si kuta ndani ya jumuiya na nje yake. Kila mtu anapochangia kwa kutekeleza wajibu wake kwa upendo, kunakuwa na amani katika jamii. Ulimwengu pia unatuhitaji tuwe watawa ambao ni  mafundi wa amani! Tafakari hiyo ya amani, Baba Mtakatifu ameandika kwamba imemwongoza , kutafakari kipengele kingine cha watawa kuhusu  Sinodi, mchakato huu ambao sisi sote tumeitwa kuingia kama washiriki wa watu watakatifu wa Mungu, njia ya kushiriki katika hilo, kwa kuwa maisha kitawa tayari  ni sinodi kwa asili yake. Pia ina miundo mingi inayoweza kupendelea sinodi. Katika hili amefikiria mikutano mikuu ya shirika, ya provinsi au kikanda na mahalia, ziara zao katika jumuiya mbali mbali za kitawa na nyuma za mapadre, mikutano na tume na hata  miundo mingine inayofaa kwa taasisi binafsi.

Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G
Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G

Papa anawashukuru wale waliojitolea na wanaotoa mchango wao katika safari hiyo, katika ngazi mbalimbali na katika nyanja mbalimbali za ushiriki. Asante kwa sababu wanafanya sauti yao isikike kama watu waliowekwa wakfu. Lakini, kama tunavyojua, haitoshi kuwa na miundo ya sinodi: ni muhimu "kutembelea, kujiuliza kwanza kabisa: ni jinsi gani miundo hiyo imeandaliwa na kutumika? Katika muktadha huo, njia ambayo huduma ya mamlaka inatekelezwa lazima ichunguzwe na labda pia irekebishwe. Kiukweli, ni muhimu kuwa makini dhidi ya hatari ambayo inaweza kuharibika na kuwa aina za kimabavu, wakati mwingine za udhalimu, na matumizi mabaya ya dhamiri au kiroho ambayo pia ni msingi wa unyanyasaji wa kijinsia, kwa sababu mtu na haki zake haziheshimiwi tena. Na zaidi ya hayo kuna hatari kwamba mamlaka inatumika kama upendeleo, kwa wale wanaoishikilia au kwa wale wanaoiunga mkono, kwa hiyo pia ni kama aina ya ushirikiano kati ya vyama, ili kila mtu afanye anachotaka, na hivyo kupendelea aina fulani ya machafuko, ambayo husababisha uharibifu mkubwa kwa jumuiya.  Ni matumaini ya Papa  kwamba huduma ya mamlaka itatekelezwa kila wakati kwa mtindo wa sinodi, kwa kuheshimu sheria ifaayo na upatanishi unaotolewa, ili kuepuka ubabe, upendeleo, na kuacha wafanye; kukuza mazingira ya kusikilizana, kuheshimiana, mazungumzo, kushiriki na kushirikishana. Watawa, pamoja na ushuhuda wao, wanaweza kuchangia sana katika Kanisa katika mchakato huu wa sinodi tunayopitia. Isipokuwa wao wawe wa kwanza kuuona, kutembea pamoja, kusikilizana, kuthamini zawadi mbalimbali, na kuwa jumuiya zinazokaribisha.

Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G
Mkutano wa papa Francisko na UMOJA WA WAKUU WA MASHIRIKA YA KITAWA U.S.G

Katika mtazamo huo, Baba Mtakatifu amewaleza hawa wakuu wa mashirika kwamba  njia za tathmini ya ufanisi ina uwezo lakini ni muhimu upyaishaji wa kizazi katika uongozi wa taasisi ili kuweza  kufanyika kwa njia bora zaidi. Bila uboreshaji kiukweli, kuelewa matatizo ya sasa, mara nyingi inakuwa ngumu, na inahitaji mafunzo ya kutosha, vinginevyo hujui ni wapi pa kulekea. Zaidi ya hayo, upangaji upya au urekebishaji upya wa taasisi lazima ufanyike kila wakati kwa nia ya kulinda ushirika, ili usipunguze kila kitu hadi kuunganisha mizunguko, ambayo inaweza kuthibitisha kutoweza kudhibitiwa kwa urahisi au kusababisha migogoro. Katika suala hilo ni muhimu wakuu wawe waangalifu ili kuepuka baadhi ya watu kutoshughulika vizuri, kwa sababu hiyo, pamoja na kuwadhuru, huzua mivutano katika jamii. Papa amehitimisha akiwashuru tena na kuwatakia waendelee na huduma yao kwa utulivu na yenye kuzaa matunda na kuwa mafundi wa amani.

Hotuba ya Papa kwa U.S.G
26 November 2022, 15:44