Tafuta

Papa amekutana na Kurugenzi Kuu ya Kupambana na uhalifu Italia.Amepongeza uwepo wa wanawake wengi wanaojishughulisha kusaidia. Papa amekutana na Kurugenzi Kuu ya Kupambana na uhalifu Italia.Amepongeza uwepo wa wanawake wengi wanaojishughulisha kusaidia.  (Vatican Media)

Papa:wanawake ni waathirika wa ukatili&serikali ihakikishe usalama

Papa Francisko amekutana na wajumbe wa Kurugenzi Kuu ya Kupambana na Uhalifu,siku moja baada ya Siku ya Kimataifa ya Kupambana na ukatili dhidi ya wanawake,iliyoanzishwa na Umoja wa Mataifa na toleo la 2022 kwa Kampeni ya Polisi,Nchi Italia: “ Huo sio Upendo”.Wito wa Papa ni ule wa kusaidia wanaweke kuhakikisha usalama kwa hatari zinaonekana na kuwasindikiza kwa kila hatua.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumamosi tarehe 26 Novemba 2022 amekutana na wajumbe wa Kurugenzi Kuu ya Kupambana na Uhalifu nchini Italia. Amemshukuru Mkuu wa Polisi kwa maneno ya utangulizi wake. Amekuwa na furaha ya kukutana nao hasa siku moja baada ya  Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wanawake inayaohamasisha na Umoja wa Mataifa kila mwaka ifikapo tarehe 25 Novemba. Kauli mbiu ya mwaka huu ilikuwa ni wito wa kuungana katika mapambano ya kuondosha wanawake na watoto katika mitindo mbali mbali ya vurugu na ukatili ambao kwa bahati mbaya Papa amesisitiza unabaki kuenea  na unavuka mipaka kwa kulinganisha na muhimili wa  kijamii. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu amependa kuwashukuru, iwe kwa kazi ambayo wanapeleke mbele kwa bidii ya kitaalumu na kibinadamu, na iwe kwa sababu kwa kuomba kukutana naye katika muktadha huo kuwa  ni kuvuta hisia za kila mtu kwa hitaji la kuunganisha nguvu kwa lengo hili la hadhi na ustaarabu.

Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi  kupambana na uhalifu
Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi kupambana na uhalifu

Baba Mtakatifu Frsncisko ameshukuru huduma wanayofanya kila siku katika jamii ya Italia. Kwa bahari mbaya, taarifa kila siku zinaonesha vurugu dhidi ya wanawake na watoto. Na wao ni kituo cha marejeo cha kitaasisi kukabiliana na ukweli huu mchungu. Kuna wanawake wengi kati yao, na hiyo Papa ameipongeza kuwa ni rasilimali kubwa kwani ni wanawake wanaosaidia wanawake wengine, ambao wanaweza kuwaelewa vyema, kuwasikiliza, kuwaunga mkono. Papa amefikiria jinsi wavyohitajiwa wao, kama wanawake, kubeba ndani yao uzito wa hali wanazokutana nazo, na ambazo zinawahusisha kwa kiwango cha kibinadamu. Anafikiri jinsi maandalizi ya kisaikolojia yaliyolengwa ni ya thamani kwa kazi hiyo. Kwa hilo ameongeza neno la kiroho, kwa sababu tu katika ngazi ya kina mtu anaweza kupata na kuhifadhi utulivu na utulivu ambayo unaruhusu ujasiri kuwasilishwa kwa wale ambao ni waathirika wa ukatili na vurugu.  Nguvu hiyo ya ndani ambayo Yesu Kristo anatuonesha katika Mateso yake, na ambayo aliwasiliana na wanawake wengi Wakristo, ambao baadhi yao tunawaheshimu kama wafia dini . Papa Francisko ametaja baadhi kama vile kuanzia kwa Agata na Lucia hadi kufikia  Maria Goretti Sr . Maria Laura Mainetti.

Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi  kupambana na uhalifu
Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi kupambana na uhalifu

Katika muktadha wa uwajibikaji wao kitaasisi Papa Francisko amependa kugusa mantiki nyingine muhimu. Kwa bahati mbaya, wanawake mara nyingi sio tu kwamba wanajikuta wakikabiliwa na hali fulani za unyanyasaji, lakini pia  kesi inaporipotiwa, hawapati haki, au nyakati za haki  zao ni ndefu sana, zisizoweza kukomeshwa. Kwa maana hiyo Baba Mtakatifu ameshaukur kwamba tunahitaji kuwa makini na kuboresha juu ya hili, bila kuangukia katika uadilifu, hapana. Serikali lazima ihakikishe kwamba kesi inasindikizwa katika kila hatua na kwamba mwathirika anaweza kupata haki haraka iwezekanavyo. Kama vile ni muhimu kwamba wanawake waokolewe yaani, ni muhimu kuhakikisha kuwa wako salama kutokana na vitisho vya sasa na pia kutoka katoka katika  ambayo kwa bahati mbaya ni mara kwa mara hata baada ya hukumu inayowezekana.

Papa Francisko akirudi tena  kutazama siku ya Kimataifa ya kupambana na ukatili dhidi ya wanawake, amesema, “kiukweli ili kushinda mapambano hayo haitoshi muhimu  maalumu, hata kama unaweza kuleta ufanisi,; utekelezaji wa sheria na hatua muhimu za ukandamizaji pia hazitoshi.  Tunahitaji kuungana, kushirikiana, kufanya mtandao: na si tu mtandao wa kujihami, lakini ni juu ya mtandao wote wa kuzuia! Hili ni jambo la kuamua kila wakati linapojaribu kuondoa janga la kijamii ambalo pia linahusishwa na mitazamo ya kiutamaduni, mawazo na chuki iliyokita mizizi. Kwa hivyo wao, pamoja na uwepo wao, ambao wakati mwingine unaweza kuwa ushuhuda, pia hunafanya kama kichocheo katika muhimili wa kijamii: kichocheo cha kuguswa, sio kukata tamaa, bali kutenda. Ni hatua hiyo  juu ya yote ya kuzuia.  Baba Mtakatifu ameomba kufikiria familia. Na zaidi kwamba imeonekana katika  janga la uviko,  kwa karantini ya  lazima, kwa bahati mbaya ambayo imezidisha mienendo fulani ndani ya nyumba za familia.

Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi  kupambana na uhalifu
Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi kupambana na uhalifu

Mahangaiko ambayo sio ya kuumba,  kiukweli mara nyingi yamekuwa  mvutano wa siri, ambao unaweza kutatuliwa mapema katika ngazi ya elimu. Kwa maana hiyo Papa amethibitisha kwamba hilo, ndilo neno kuu: elimu. Na hapo  familia haiwezi kuachwa peke yake. Ikiwa athari za mgogoro wa kiuchumi na kijamii zinaangukia familia kwa sehemu kubwa, na haziungwi mkono vya kutosha, hatuwezi kushangaa kwamba huko, katika mazingira ya ndani ya kufungwa, na matatizo mengi, mivutano fulani hulipuka. Na kurugeniz ya kuzuia inakwenda kwa hatua hiyo. Kipengele kingine cha kuamua ni kwamba  ikiwa vyombo vya habari vinapendekeza kila wakati ujumbe unaolisha utamaduni wa watu wengi na watumiaji, ambapo wanamitindo, wanaume na wanawake, wanatii vigezo vya mafanikio, kujidai, ushindani, uwezo wa kuvutia wengine na kuitawala, hata hapo  basi  hatuwezi, kwa njia ya unafiki, kurarua nguo zetu mbele ya historia fulani za habari.

Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi  kupambana na uhalifu
Papa amekutana na Kurugenzi kuu ya Polisi kupambana na uhalifu

Aina hii ya hali ya kiutamaduni inatofautiana na hatua ya elimu inayomweka mtu katikati, na hadhi yake. Mtakatifu wa nyakati zetu ambaye Papa Francisko amemkumbuka akilini mwake ni Mtakatifu Josephine Bakhita. Yeye amewekwa kama msimamizi wanawake katika  kazi za kikanisa zinazofanywa pamoja na waathiriwa wa biashara mbaya ya binadamu. Sr Giuseppina Bakhita alikumbana na ukatili mkubwa katika utoto na ujana wake; alijikomboa kikamilifu kwa kuikubali Injili ya upendo wa Mungu na akawa shuhuda wa uwezo wake wa ukombozi na uponyaji. Lakini si yeye peke yake kwani kuna wanawake wengi, wengine ni “watakatifu wa mlango wa  karibu”, ambao wameponywa kwa rehemu,  kwa huruma ya Kristo, na kwa maisha yao wanashuhudia kwamba hatupaswi kujiondoa wenyewe, upendo huo,  ukaribu, mshikamano wa akina dada na kaka unaweza kutuokoa kutoka katika utumwa. Ndiyo maana Papa amesema kwamba: kwa wasichana na wavulana wa leo huu, wanatoa shuhuda hizi. Katika shule, vikundi vya michezo, historia, vyama, tunawasilisha historia za kweli za ukombozi na uponyaji, historia za wanawake ambao wametoka kwenye handaki la vurugu na wanaweza kusaidia kufungua macho yao dhi ya mitego, hatari zilizofichwa nyuma ya mifano ya uwongo ya mafanikio.

Papa amekutana na Kurugenzi Kuu ya Polisi ya kupambana na uhalifu
26 November 2022, 15:31