Tafuta

2021.09.20 Chanjo kwa watoto katika Hospitali ya kipapa ya 'Bambino Gesù' 2021.09.20 Chanjo kwa watoto katika Hospitali ya kipapa ya 'Bambino Gesù'  

Chanjo ya UVIKO:Hospitali ya Bambino Gesù imeanza dozi ya tatu kwa wagonjwa

Jumatatu tarehe 20 Septemba 2021,katika Hospitali ya kipapa ya watoto 'Bambino Gesù' wameanza utoaji wa dozi ya chanjo ya tatu dhidi ya UVIKO -19,kwa wagonjwa walio katika mazingira magumu kiafya,kulingana na vigezo vilivyoamriwa katika kiwango cha kitaifa na kikanda.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumatatu tarehe 20 Septemba 2021, katika Hospitali ya kipapa ya watoto Bambino Gesù wameanza utoaji wa dozi ya chanjo ya tatu dhidi ya Sars-CoV-2 yaani ya   UVIKO -19 , kwa wagonjwa walio katika mazingira magumu kiafya, kulingana na vigezo vilivyoamriwa katika kiwango cha kitaifa na kikanda. Kiwango cha dozi ya nyongeza kimekusudiwa kwa watoto wapatao 400 na watu wazima walio wadhaifu sana (wenye umri wa miaka 12 na zaidi) wanaofuatiliwa moja kwa moja na Hospitali ya watoto ‘Bambino Gesù’ ya  chanjo hapo awali katika Hospitali ya watoto ya Kipapa. Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa wamebainisha kwamba wao wataitwa polepole na hospitali kwa ajili ya usimamizi wa kipimo cha tatu kwa njia ile ile kama ile ya awali.

Hawa ni watoto wa kike na kiume walio wasio na kinga za mwili zilizo za kutosha na mabo wana matatizo makubwa kama vile ya kupandikizwa viungo, ugonjwa wa figo sugu, na saratani ya damu, ambapo vikundi vyote vinaoneshwa kama kupewa kipaumbele na mzunguko mpya ya Wizara ya Afya nchini Italia. Watu dhaifu wana hatari zaidi ya kuambukizwa maambukizo yote na wana uwezekano mkubwa kuliko wengine kuwa ngumu  kwa mujibu wa Profesa Alberto Villani, Mkurugenzi wa Idara ya Dharura, mapokezo na  Mkuu wa Kitengo cha Watoto cha  hospitali ya Bambino Gesù. Kwa njia hiyo ni muhimu sana kuwalinda na dozi ya tatu inawakilisha ubora wa kulinda watu wadhaifu  wa aina hii

20 September 2021, 16:34