Tafuta

Askofu Mkuu Fisichella:Malengo na bajeti ya utume yanavyofanya kazi

Baraza la Kipapa la kuhamasisha Unjilishaji mpya linasimulia kutoka ndani.Malengo na bajeti ya utume inavyofanya kazi katika muundo ambao unasaidia Huduma ya Kipapa ulimenguni.Mahojiano na Askofu Mkuu Rino Fisichella,Rais wa Baraz ala Kipapa la Uinjilishaji Mpya.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Muundo uliowekwa kwa tangazo na umisionari katika mwendelezo wa  mapenzi ya Mapapa. Ulizaliwa na Papa Mstaafu Benedikto XVI na kupanuliwa katika majukumu yake na Papa Fransisko. Baraza la Kipapa la Uhamasishaji wa Uinjilishaji Mpya katika miaka kumi ya maisha limetembea njia tofauti ili kuleta Injili kwa njia mpya katika vituo na pembezoni mwa ubinadamu. Hii ni pamoja na:  Jumapili ya Neno la Mungu, katika Jubilei ya Huruma, Siku ya Maskini Duniani kama sehemu ndogo tu inayomegeka kutoka katika barafu la utume ambao hutumia kitendea kazi cha kufanya shughuli zake za  bajeti ya utume  ambao, katika data rasmi ya 2021 ya Vatican, ni sehemu ya bajeti milioni 21 iliyotengwa kwa ujumla na makao makuu na taasisi tatu za Vatican. Rais wa Baraza la Kipapa la Uinjilishaji mpya, Askofu Rino Fisichella, ambaye ameiongoza tangu kuanzishwa kwake, anaelezea utendaji wake na mafanikio yake.

21 September 2021, 17:15