Tafuta

2021.09.20: Padre Adam Zak katika  Mkutano huko Warsaw Poland 2021.09.20: Padre Adam Zak katika Mkutano huko Warsaw Poland  

Tujifunze kutokana na makosa ya wengine ili tukue

Mkutano unaendelea huko Warsaw nchini Poland katika jitihada za Kanisa dhidi ya nyanyaso ambazo zinagusa kwa uchungu majareha.Jumanne Septemba 21 Padre Zak ameeleza nini maana ya tukio hilo katika mji wa Warsaw akihojiana na Vatican News.Jumatatu 20 Septemba Profesa Halik alifungua kikao.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Jumanne tarehe 21 Septemba kati ya watoa mada katika Mkutano wa Warsaw  nchini Poland Kuhusu Ulinzi wa Watoto, alikuwapo hata mjesuit Adam, Padre  Żak SJ, ambaye ni mratibu wa Baraza la Maaskofu Poland kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto. Akizungumza na Vatican News, ameonesha matokeo yaliyojiri kwa miaka ya mwisho, shukrani na mipango mingine tofauti iliyotekelezwa, lakini pia ameelezea kuwa bado kuna hatua ndefu ya kutumiza katika kupinga uhalifu huu. Kwa hakika muktadha kama huu katika hisia za watu wapoland zimesimanisha mapambano ya nyanyaso. Padre Adam Żak SJ, ameelezea juu ya muktadha wa kufanyika aina ya mkutano huu jijini Warsa kwamba “kwa hakika kufanyika mutano huo ni kichocheo kwa Kanisa letu kuendelea katika njia iliyofanywa kwa miaka kadhaa ya kupambana na aina zote za unyanyasaji. Tnaweza kuseme kwamba kuna ufahamu mkubwa kwa maaskofu na wakuu wa ya kitawa lakini ufahamu huu bado haujatokana na elimu, ambayo ni, juu ya mafunzo ya kitaalam ambayo badala yake ni muhimu kukabiliana na hali kama huu ngumu, mbaya kama ya unyanyasaji wa kijinsi kwa watoto na watu walio katika mazingira magumu. Nadhani uteuzi wa Warsaw utakuwa nyongeza zaidi, kati ya mengi ya kutosha ambayo tumepokea katika miaka mitatu iliyopita kutoka katika asasi za kiraia na vyombo vya habari”

Vile vile Padre Zak akielezea juu ya muunod wa ushiriki wa mkutano huo amesema  “Muundo wa washiriki sio sawa kwa mabaraza yote ya maaskofu, mashirika ya kitawa  na kadhalika. Makanisa mengine yana ujumbe mkubwa, kama vile Hungaria ambayo imetuma wawakilishi kutoka sehemu zote ambazo hatua huchukuliwa katika mwelekeo wa kuimarisha na kuhamasisha ulinzi wa watoto. Makanisa mengine, kwa upande mwingine, yana shida, kama vile Belarusi au Urusi ambayo imetuma mwakilishi aliyeteuliwa na Baraza la  Maaskofu kushughulikia suala hilo. Tayari kutokana na muundo huu tunaweza kuona ni Makanisa mangapi yanafanya kazi sana kwenye mada hii, lakini kwa sehemu tofauti zikiwa katika safari. Kwa maana hiyo ni lazima kujifunze kutokana na makosa ya wengine na ili tupate kukua”  hasa kwa kuwa na utambuzi wa nguvu ya ukweli.

Kazi iliendelea hata hivyo asubuhi Jumatatu tarehe 20 Septemba  2021 na kufunguliwa kwa hotuba ndefu ya Monsinyo Tomáš Halík, profesa wa Chuo Kikuu cha Charles huko Prague, pia rais wa Chuo cha Kikristo cha Czech, ambaye ni kati ya makuhani waliowekwa wekwa wakfu kwa siri wakati wa utawala wa kikomunisti, na kwa muda mrefu amekuwa katibu mkuu Baraza la Maaskofu  wa Kicheki Cecoslvakia. Kwa roho ya unyenyekevu na kwa moyo wenye uchungu alisema kuwa wanagusa jeraha moja lenye maumivu zaidi ya Kanisa.

Mkutano unaendelea huko Warsaw Poland kuhusu ulinzi wa watoto
Mkutano unaendelea huko Warsaw Poland kuhusu ulinzi wa watoto

Mwili wa fumbo wa Kristo aliyefufuka pia hubeba vidonda, na ikiwa watapuuza majeraha haya, au hawataki kuwagusa, wasingekuwa na haki ya kusema kama mtume Thomas:” Bwana wangu na Mungu wangu! “Kristo asiye na majeraha, Kanisa lisilo na majeraha, imani isiyo na majeraha, ni udanganyifu tu wa kishetani”, alisisitiza Monsinyo  Halík.  Kwa kujiamini katika nguvu ya uponyaji na ukombozi wa ukweli  kusema kuwa wao wanataka kugusa vidonda ambavyo kiongozi  huyo mwakilishi wa Kanisa ambaye amewakuwa bege kwa bega katika ulinzi wa wasio na ulinzi, hasa watoto na vijana; kwa sababu amesema tendo la kufanya hivyo limeweza kusababisha majeraha polepole na magumu kutibu uponyaji wa Kanisa katika ulimwengu wa leo. Kulingana na profesa, kesi za unyanyasaji pia zinaonesha kuwa mgogoro wa makuhani kwa ujumla ambapo inaweza kushinda tu kwa uelewa mpya wa jukumu la Kanisa katika jamii ya kisasa kama shule ya hekima ya Kikristo, hospitali kambini na mahali pa kukutana, kushiriki na upatanisho.

21 September 2021, 16:48