Tafuta

2021.09.22 Papa Francisko na kundi la familia wa Afghanistani waliokimbia Kabul. 2021.09.22 Papa Francisko na kundi la familia wa Afghanistani waliokimbia Kabul. 

Papa Francisko akutana na kundi la familia waliokimbia kutoka Kabul

Kabla ya katekesi yake Papa Francisko amekutana na kundi la watu kama kumi na tano wakristo miongoni mwake watoto saba ambao wamemsimulia uchungu na ukosefu wa usalama mara baada ya kurudi Wataleban nchini Afghanistan na kabla ya kusafiri kuja Italia.“Tulijificha ndani ya andaki kwa siku nne usiku na mchana tukihofia kukamatwa."

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Pete na nguo. Ndivyo mwanamke kutoka Afghanistan asubuhi amejiwakilisha mbele ya Papa Francisko na kumpatia pete na nguo ya kumbu kumbu ya mme wake aliyekamatwa wakati wa ghasia za watalebani huko Kabul nchini Afghanstani na ambaye hawajuhi ameishia wapi, akisimulia maisha ya mateso. Papa Francisko Jumatano tarehe 22 Septemba 2021 kabla ya Katekesi yake katika ukumbi wa Paulo VI, amepokea zawadi ya pete, lakini akaiwekea hali  kwamba mama hiyo  Pary Gul awe ndiye mtunzaji kama ahadi ya urafiki na ishara ya matumaini. Na matumaini ya mwanamke ameyaonesha katika macho ya watoto wake wasichana  watatu na na mtoto wa kiume Nasim.  Hawa wana umri kati ya 25 na 14.  Hawa ni wasichana ambao kwa msaada wa SOS uliozinduliwa kwa njia ya simu mahiri iliwawezesha  watoroke kutoka Kabul.  Na hatimaye kufikia nyumba zao mpya katika eneo la Bergamo nchini Italia, ambapo wanaweza sasa kuzindua maisha yao kwa upya. Shukrani kwa njia ya mtandao wa mshikamano ulioratibiwa na mwandishi mmoja kutoka nchini huko, ambaye alikimbia Kabul miaka iliyopita kwa kujificha chini ya lori na pia kumuona kaka yake akifariki safarini na sasa yupo katika   Kituo cha Kukutana kibinadamu.

Wengine walioweza kutoroka ni familia tatu za Kikristo: watu 14, wanawake 8 na wanaume 6. Watoto saba(wote walikuwa na mchoro kwa ajili ya Papa). Aliyekuwa mdogo , ambaye ametimiza hivi karibuni mwaka mmoja na alilazwa hospitalini kwa dharura mara baada ya kufika Italia kwa sababu ya tatizo alilokuwa nalo na sasa hajambo. Historia ambayo familia tatu ziliwasilisha kwa Papa zinashangaza  kwa ukatili walioupata. Na ina maana ya maumivu. Na kuhusu ukweli kwamba wao walikuwa Wakristo uliibua malalamiko dhidi yao mara tu Wataliban walipoingia Kabul. “Mume wangu alifutwa kazi kwanza na kisha kukamatwa, na hatuna habari zozote kuhusu yeye,” anasema mwanamke huyo, mwenye umri wa miaka 57. “Tulibaki tumefungwa ndani ya andaki kwa siku nne,  usiku na mchana kwa kuogopa kila mtu kukamatwa, labda mtu kutusemea kuwa sisi ni Wakristo”.

Hata Familianyingine wote wawili wenye umri wa miaka  32 waliweza kuacha Kabul na watoto wao miaka 9 na miaka 4. Pamoja nao hata Familia nyingine mwanaume mwenye umri wa miaka 35 na mke miaka 34 na watoto wao wenye umri miaka 11, 8 na mdogo wa mwaka mmoja. 'Ndugu za Afghanistan' ni kauli mbiu ya kampeni ya chama cha kibinadamu ambacho ni Kituo cha Kutana na Binadamu kimejikita kufuatilia nchini Afghanistan na ushirikiano wa taasisi za kiraia na jeshi la Italia. Udugu ambao mara moja unachukua sura katika msaada halisi kwa familia tatu ili kujenga uhusiano, kupata kazi, na kupata elimu. Kwa kifupi, kurudia kuishi. Kwa kulinda “pete ya Papa”.

22 September 2021, 17:33