Tafuta

2021.09.20 Mkutano huko Warsaw na Padre Zollner. 2021.09.20 Mkutano huko Warsaw na Padre Zollner. 

Pd.Zollner:Kutoka Warsaw habari ni nzuri lakini yapo mengi ya kufanya

Katika mahojiano na Mjumbe wa Tume ya Kipapa kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na ambaye ameandaa mkutano wa kimataifa Poland,amesema katika mada hiyo kuna shauku ya kushirikishana na kuboresha ulinzi lakini baadhi ya makanisa katika mikoa hiyo bado na lazima wakabiliane na kashfa hizi.

Na Sr. Angela rwezaula - Vatican

Katika mkutano ulionza tarehe 19 Septemba huko Warsaw  Poland na ambao unafungwa tarehe 22 Septemba, Padre padre Hans Zollner, Mjesuit, Mkurugenzi wa Taasisi mpya ya Anthropolojia ya Chuo Kikuu  cha Kipapa Gregoriana na ambaye ni mmoja wa waandaaji wa Mkutano huo wa Kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto na watu wazima katika mazingira magumu kwa ajili ya Kanisa la Ulaya ya Kati ya Mashariki amehojiwa na Vatican News. Katika maelezo yake amesema kuhusu mkutano huo, wamefanya vizuri kwa mtazamo wa mada ambazo walitaka kuzionesha, kuunda hasa kuhusu mazingira ya kushirikiana na kujitoa kwa pamoja. Yeye amehisi shauku kubwa ya kushirikiana kati ya watu walioshiriki na anayo hamu kwamba wataendelee kuimarisha kazi ya kuzuia na kulinda.

Mwamko wa ulinzi umeanza taretibu katika makanisa ya Ulaya ya kati na mashariki

Mkuu wa kitengo hicho Padre Zollner amesema hadi miaka michache iliyopita katika Makanisa ya Ulaya ya Kati na Mashariki, maoni yalikuwa yaliyokuwa yameenea kuwa unyanyasaji wa kijinsia uliofanywa na wahusika wa dini ni jambo la Magharibi, kwa mfano katika jamii za watu wasio na dini, wakati huko Ulaya ya Kati hakukuwa na kesi kwa sababu serikali za Kikomunisti zisingewza kuvumilia katu hali hiyo. Badala yake, katika miaka ya hivi karibuni upepo pia umebadilika katika makanisa ya eneo hilo la bara la kizamani na sasa kuna unyeti zaidi juu ya masuala kama haya. Amebainisha Padre Zollner kuwa huko Poland, shukrani kwa filamu na vyombo vingine vya habari  mwamko umekua na kwamba visa vya unyanyasaji pia vilitokea wakati wa ukomunisti na hiyo hiyo ilitokea katika nchi nyingine za mkoa huo. Na sasa kuna harakati zilizoundwa na watu walionyanyaswa ambao husaidia kuchangia kuleta mabaya haya na uhalifu wa zamani

Tusiwaache peke yao wanaopambana na nyanyaso

Malengo mengine ya mkutano wa Warsaw nchini Poland kwa mujibu wa kiongozi huyo na mtaalamu, likuwa kuunda majukwaa ya ushirikiano na kubadilishana. Kiukweli, katika nchi nyingi, kazi ya kuzuia na kuwasikiliza waathiriwa imekabidhiwa tu kwa watu wenye utaalam ambao mara nyingi huhisi kutengwa, kutelekezwa kutoka katika majimbo na kutoka katika mashirika ya kitawa. Kwa hiyo ni muhimu kuwasaidia kuwasiliana na kila mmoja, ili waweze kutiana moyo na waweze kubadilishana mazoea mazuri ya kuboresha huduma na kupata nguvu mpya, ili wasijisikie wameachwa. Matumaini ya Padre ni kwamba hali inaweza kuboreka zaidi katika ukanda huu pia. 

Wapo wanaofikiria mgogoro huo  wameushinda

Walakini, Padre Zollner amesema inabaki kuboresha maarifa ya kile ambacho Vatican imefanya katika miaka ya hivi karibuni hasa katika sekta ya mapambano dhidi ya dhuluma hii ya unyanyasaji. Kama karibu kila mahali, upokeaji wa kanuni mpya ambazo Kanisa limezindua katika miaka ya hivi karibuni ni tofauti sana na sio Makanisa yote ya hapa yamefikia kiwango sawa cha utekelezaji. “Hii ilikuwa moja ya malengo tuliyokuwa nayo akilini wakati tulileta mkutano huu Ulaya ya Kati, ambapo - kama inavyotokea katika mikoa mingine kuna Mabaraza ya Maaskofu, maaskofu na mashirika ya kitawa ambayo yanasonga mbele, wanatambua uzito wa hali hiyo na wamejitolea kwa kiasi kikubwa kuibadilisha na wengine ambao wanasubiri mgogoro huu upite au wanaamini kuwa tayari wameushinda”.

Ulazima wa kuendelea na ulinzi kwani bado kuna mengi ya kufanya

Katika kipindi cha miaka kumi au kumi na mbili iliyopita, viongozi wa Vatican wameelewa kuwa ilikuwa ni lazima kuendelea mbele kwa lengo zaidi zaidi ili Kanisa liweze kuelezea unyanyasaji wa watoto uliofanywa na wahusika wa dini, mbele ya waamini, Serikali na vyombo vya habari. Kanisa limejitoa kulaani wale waliohusika na maaskofu ambao hawakushirikiana, wakikiuka sheria za kanoni na za kiraia. Hata nchini Poland, katika miaka ya hivi karibuni, maaskofu wengine ambao wamejiuzulu, hata kama sababu hiyo haikutangazwa kwa umma, walikuwa wazembe kwa wahanga wa unyanyasaji na michakato waliyopaswa kuanzisha. Hakika motu proprio 'Vos Estis lux mundi' imesaidia kubadilisha fikira na kuunda uwajibikaji mkubwa, lakini bado kuna mengi ya kufanya,  amekumbusha Padre Zollner.

22 September 2021, 17:22