Tafuta

Baba Mtakatifu Francisko, kwa muda sasa, anatia saini nyaraka zake zote akiwa Laterano ili kuangazia kiungo na mahali panaposhikilia kiti cha askofu wa Roma. Baba Mtakatifu Francisko, kwa muda sasa, anatia saini nyaraka zake zote akiwa Laterano ili kuangazia kiungo na mahali panaposhikilia kiti cha askofu wa Roma. 

Tangu Desemba 13 Jumba la Kipapa la Laterano liko wazi kwa mahujaji

Kuanzia tarehe 13 Desemba 2021 nyumba ya Askofu wa Roma itafunguliwa milango yake wazi kutazamwa na watalii na mahujaji.Alikuwa ni Baba Mtakatifu mwenyewe aliyeshauri kuhamasisha utazamaji wa jumba hili ambalo kwa karne zilizopita lilikuwa ni makao ya Mapapa.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Ni takriban mita za mraba elfu tatu, vyumba kumi, ghorofa ya Papa, Kikanisa kidogo binafsi, ngazi kubwa inayoongoza moja kwa moja kwenye Kanisa Kuu la Mtakatifu Yohane huko Laterano na meza ambayo ilitiwa saini ya Mkataba wa Laterano. Kwa karne nyingi makao ya Papa au Ikulu ya Papa huko Laterano kabla ya kuhamishiwa Vatican, inafunguliwa kwa milango yake kwa wageni.

Kati ya sanaa na imani

Ikiwa imekarabatiwa kikamilifu katika mpangilio wake, kuanzia tarehe 13 Desemba 2021 itafurahiwa kwa usalama na vikundi vidogo vidogo vya wageni  hadi watu 30, wakisindikizwa na Masista Wamisionari wa Ufunuo wa Mungu, ambao wamekuwa wakitoa huduma ya mchakato wa safari za sanaa na imani huko Roma kwa miaka mingi.

Matakwa ya Papa

Ilikuwa ni Papa mwenyewe mnamo tarehe 20 Februari iliyopita, katika barua iliyotumwa kwa Kadinali Angelo De Donatis, makamu wa Jimbo la Roma ambaye alipendekeza kufufua mahali muhimu kama hapo akithibitisha tena kwa Kanisa kujitoa kwa karne nyingi kushuhudia imani kwa njia ya sanaa. Kardinali De Donatis kutokana na hilo amesisitiza kwamba: “Tunafahamu vyema maana ya kina ya mahali hapa na ingekuwa si vizuri sana kutoifungua kwa umma, kwa sababu wema mkubwa kama huu lazima ushirikishwe, lazima utolewe kwa wengine. Aidha ameongeza kusema kuwamba "Ambaye alikuwa ameshikamana sana na mahali hapa na alitaka hata kuja na kuishi, alikuwa Yohane XXIII. Baba Mtakatifu Francisko, kwa muda sasa, anatia saini nyaraka zake zote akiwa Laterano ili kuangazia kiungo na mahali panaposhikilia kiti cha Askofu wa Roma!

Safari katika historia ya Kanisa

Kwa upande wao, Masista Wamisonari wa Ufunuo ambao wanaishi tusema kwa bahati nzuri na heshima kubwa ya hudumia  shemu hii ya uinjilishaji kwa njia ya sanaa wamebainisha kuwa:“Yule atakaye inngia ndani ya Jumba la Laterano, itakuwa ni safari ya kusisimua katika kurasa za historia ya Kanisa, ambapo sanaa na imani vimefungamanishwa na kuzaa matunda ambayo yanaweza kusambaza maajabu, hekima na uzuri kwa vizazi mbalimbali".

04 December 2021, 16:40