Tafuta

2022.05.17 Kardinali Parolin katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano 2022.05.17 Kardinali Parolin katika Chuo Kikuu cha Kipapa Laterano 

Kard.Parolin:Praedicate Evangelium ni chombo kwa manufaa ya Kanisa&huduma ya Maaskofu

Katibu wa Vatican,Kardinali Parolin ametoa hotuba katika Siku ya Mafunzo huko Laterano kuhusu Katiba ya Kitume 'Predicate Evangelium' iliyochapishwa mnamo 19 Machi."Sekretarieti ya Vatican haijapoteza hadhi yakekazi zake ni sawa lakini kwa njia tofauti.Katiba mpya inajaribu kujumlisha uzoefu na marekebisho ya miaka iliyopita,kufanya hatua mpya,ili kukamilisha picha yake kwa jumla".

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mabadiliko ya kimuundo, mambo mapya yanayoagizwa na dharura za sasa, michakato iliyofanywa kwa muda wa miaka na hatimaye kukamilika ndiyo maelezo ya Kardinali Pietro Parolin, alivyodadavua ndani ya kitovu cha Praedicate Evangelium, ambayo ni katiba mpya  ya kitume ambayo inarekebisha Curia Romana iliyochapishwa mnamo tarehe 19 Machi 2022 na ambayo itaanza kutumika rasmi mnamo tarehe 5 Juni 2022 ambapo, amesema ni moja ya malengo makuu ambayo tangu mwanzo, Papa wa sasa alikuwa amejiwekea. Kardinali Parolin amesema hayo Jumanne tarehe 17 Mei 2022 wakati wa Ufunguzi wa siku ya Mafunzo yaliyoongozwa na mada: “Praedicate Evangelium. Muundo, yaliyomo na habari mpya", iliyoandaliwa na Taasisi ya Utriusque Iuris ya Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano Roma. Ni siku muhimu, ya kwanza tangu kuchapishwa kwa Katiba ya ulinganisho mpana katika kiwango cha juu ili kuelewa muhtasari na vigezo vya hati ambayo Papa Fransisko alioanisha katika mabadiliko ya Curia Romana na  ambayo tayari yametekelezwa na ambayo yalianza kufanya kazi katika mchakato wa upapa wake hadi leo hii. 

Katiba Mpya ya Kitume ni jibu kwa maombi ya makardinali kabla ya mkutano wa uchaguzi 2013

Mbali na Kardinali Parolin,pia  Kardinali Marcello Semeraro, ambaye kwa miaka amekuwa katibu wa Baraza la Makardinali, na kwa sasa ni Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la kuwatangaza watakatifu, Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Uchumi, Padre Juan Antonio Guerrero Alves, Mwenyekiti wa  Baraza la Kipapa la Mawasiliano, Paolo Ruffini, mkaguzi mkuu wa hesabu, Alessandro Cassinis Righini walikuwapo bali alikosekana  Monsinyo Marco Mellino, katibu wa Baraza la Makardinali, kwa sababu za kiafya. Kwa hiyo katika Ukumbi mkuu, mbele ya walimu na wanafunzi wa 'Chuo Kikuu cha Kipapa cha Laterano, Kardinali Parolin amekumbuka hatua ambazo, katika miaka hii tisa, zimesababisha kuandikwa kwa Katiba iliyorekebishwa ya Curia Romana ambayo ni chombo katika mikono ya Papa kwa manufaa ya Kanisa na huduma ya maaskofu. Praedicate Evangelium, ni jibu moja  kuhusu maombi yaliyotolewa na makardinali wakati wa mkutano Mkuu, kabla ya uchaguzi 2013, amethibitisha Kardinali Parolin. Miongoni mwa matendo ya kwanza ya upapa,alianzisha Baraza la Makardinali na kazi ya kusoma mpango wa marekebisho ya Katiba ya Kitume ‘Pastor Bonus ‘Mchungaji Mwema’.

Katiba mpya inajaribu kujumlisha uzoefu wa marekebisho ya miaka iliyopita

Na mageuzi yaliyopendekezwa yametekelezwa hatua kwa hatua kwa miaka kadhaa, kwa kuundwa vyombo vipya na kwa marekebisho yasiyoepukika yanayofuata, katika taasisi mpya kabisa ambazo zinaingia na kutakiwa kufanya kazi pamoja, ameelezea  Kardinali Parolin. Sasa, katiba ya kitume  Praedicate Evangelium, inajaribu kujumlisha uzoefu na marekebisho ya miaka iliyopita, kufanya hatua mpya, ili kukamilisha picha ya jumla. Na kwa kufanya hivyo ni kulingana na vigezo vitatu: “Muungano wa taasisi za kikanisa, ushirikiano katika mahusiano ya kimihimili na kukabiliana na mitazamo inayofaa  ya kibinafsi". Sehemu kubwa ya hotuba ya Kardinali Parolin ililenga juu ya jukumu la Sekretarieti ya Vatican ambayo inabaki na hadhi fulani katika sheria kwa sababu ya kazi yake maalum ya kumsaidia kwa karibu Papa,  katika utekelezaji wa utume wake mkuu. Kazi kimsingi ni zile zilizofanywa hapo awali, pamoja na tofauti. Awali ya yote, mabadiliko yanayohusiana na nyanja ya kiuchumi. Kuhusiana na hili, Kardinali alikumbuka Motu Proprio ya 2020 ambayo ilithibitisha kwamba Sekretarieti ya Uchumi ilifanya kazi ya Sekretarieti ya Papa ya masuala ya uchumi na fedha na kwamba uwekezaji na fedha zilizokabidhiwa hapo awali  katika Ofisi  Tawala ya Sekretarieti ya Vatican.

Katiba Mpya inaimarisha mabadiliko ya kiofisi 

Katiba mpya inaimarisha mabadiliko haya. Hadhi ya Sekretarieti ya Papa, kama ofisi inayosaidia kwa karibu serikali ya kichungaji ya Baba Mtakatifu, kwa sasa inashirikishwa na taasisi mbili tofauti za Curia Romana. Katika masuala ya kiuchumi na kifedha, hali hii ni ya Sekretarieti ya Uchumi, na katika nyanja nyingine zote za Sekretarieti ya Nchi, amefafanua Kardinali Parolin. Kutajwa pia kwa mada ya mawasiliano rasmi ya Vatican, pamoja na kuundwa upya kwa Baraza la Kipapa la  Mawasiliano ambalo, pamoja na taasisi mbali mbali zilizounganishwa na Sekretarieti ya Vatican (Osservatore Romano, Radio Vatican), pia imejumuisha Ofisi ya vyombo vya habari. Nidhamu mpya, ameeleza Kardinali Parolin inabaki imehifadhiwa katika kitengo cha masuala makuu ya Jumla ya uchapishaji rasimi wa hati za Vatican kupitia Bulletin Acta Apostolicae Sedis;  kwa upande mwingine, kitengo hiki ni sawa na Baraza la Kipapa la Mawasiliano kwa ajili ya mawasiliano rasmi kuhusu matendo ya Papa na shughuli za Makao Makuu ya Vatican, kutoa muktadha huo na maelekezo sahihi ambayo Baraza hilo litalazimika kutekeleza" .

17 May 2022, 15:45