Tafuta

2022.09.21 Sanamu ya "Be Welcoming" dya mchongaji Tim Schmalz ikibarikiwa na Kardinali Czerny huko Chicago Marekani. 2022.09.21 Sanamu ya "Be Welcoming" dya mchongaji Tim Schmalz ikibarikiwa na Kardinali Czerny huko Chicago Marekani. 

Marekani:Kard.Czerny amebariki sanamu kuhusu ukaribu wa wahamiaji&wakimbizi

Afla fupi iliyoongowa na Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Maendeleo Fungamani ya Binadamu ndiyo ilifanyika katika uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Maria wa Ziwa,huko Chicago,Marekani kwa kubariki sanamu yenye mfano wa malaika kuonesha ukaribu wa wahamiaji na wakimbizi.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Sanamu ya shaba, iliyopewa jina la Be Welcoming yaani Kuwa mkarimu ni kazi ya Timothy Schmalz, mtengenezaji wa Kumbusho sanamu nyingine kubwa ya  wahamiaji  katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ,mjini Vatican. Mwaliko wa wema kwa wale ambao mara nyingi hulipa ghrama ya  kutojali kwa wengine, yalikumbushwa na  sanamu ya Mkanada Timothy Schmalz, mchongaji pamoja na mambo mengine ya sanamu kubwa ya "Malaika usiowjua",  ya wahamiaji na wakimbizi, iliyobarikiwa miaka mitatu iliyopita na Papa katika uwanja wa Mtakatifu Petro, ambapo iko karibu na nguzo katika uwanja. Mtindo ule ule wa kweli na nyenzo sawa, shaba vinarudi kuwa  kazi iliyobarikiwa na Kadinali Michael Czerny, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Maendeleo Fungamani ya Binadamukatika nafasi mbele ya Kanisa la Mtakatifu Maria wa Ziwa huko ChicagoMarekani

Malaika aliyejifichwa

"Kuwa Mkarimu", ndilo jina la sanamu, au kuwa wakarimu, kwa mtazamo wa kwanza inaonesha mgeni ameketi kwenye benchi na kifungu kwenye mabega yake. Lakini ukigeukia sanamu, hapa kuna mshangao: mgeni anageuka kuwa kweli malaika aliyejificha na kwa kufungua mabawa yake.  Ni matumaini ya  mchongo huo unaweza kuwafanya waendelee kuwa makini kila wakati  kwa kujua malaika ni nani, kuwatahadharisha  kuwa malaika kwa wengine katika kugundua kuwa Mungu "anatutumia malaika kupitia masikini, waliopotea na waliosahaulika",  alisema Kardinali Czerny, huku msanii huyo alisema kwamba kazi hiyo imeongozwa na kifungu cha Biblia kinachokumbusha hitaji la kuonesha fadhili na ukarimu kwa wale wanaokutana.

Sanamu ya Kuwa Mkarimu ya Mchongaji Tim Schmalz
Sanamu ya Kuwa Mkarimu ya Mchongaji Tim Schmalz

Timothy Schmalz ametumia miaka 25 kuchonga kazi kubwa za shaba ambazo zimewekwa  ulimwenguni kote. Mada ya wengi wao inahusu masuala ya sasa ya haki ya kijamii, kama vile ukosefu wa makazi, wahamiaji, biashara ya binadamu. Nguvu ya sanaa, Schmalz alisema katika mahojiano na Vatican News mapema mwaka huu, ni "kujenga ufahamu kwa njia ya hila na nzuri kwa jamii nzima".

Sanamu ya Kuwa Mkarimu ya Mchongaji Tim Schmalz
Sanamu ya Kuwa Mkarimu ya Mchongaji Tim Schmalz
23 September 2022, 16:04