Tafuta

Mambomu ya Urussi yanaendelea kuharibu miji ya Ukraine Mambomu ya Urussi yanaendelea kuharibu miji ya Ukraine  (ANSA)

Ujasiri wa kumaliza vita na hatari kubwa ya kwenda mbali zaidi

Vita nchini Ukraine viko katika hatua ya kugeuka:Kremlin(ngome ndani ya mji wa Urussi)inazidi kuwa kona na vitisho vya nyuklia vinazidi kuwa halisi.Chaguzi zinazidi kuwa ndogo zaidi:Inawezekana kuthubutu kufanya amani au kuzidisha mzozo na matokeo yasiyoweza kufikirika.

Sergio Centofanti

Uvamizi wa Urussi kwa nchi ya Ukraine ulipaswa kuwa wa kijuu juu. Ni muda wa miezi saba sasa  vikisababsha vifo, maombolezo na uharibifu. Ilikuwa imechochewa kama vita vya ukombozi wa watu na Wanazi wachache. Badala yake, ngome ndani ya mji wa Urussi (Kremlin) imekutana na watu walioungana ambao wanataka kubaki huru na uhuru huku raia wa Urussi hawataki kwenda kufa katika ardhi ambayo sio yao na hawataki kutekwa.

Raia wengi wa Urussi hawataki kuwa lishe ya mzozo usio na maana na wakati wakubwa na watoto wa wakubwa wakijiweka mbali na kuwa mstari wa mbele. Motisha pekee uliyobaki ni kujiokoa na kutoroka kutoka katika kulazimishwa  uliotangazwa na  Putin. Moscow haikufanya mahesabu vizuri: ilikutana na watu wenye ujasiri ambao wanapinga na ambao wanapokea mshikamano wa kimataifa. Hata zile nchi rafiki ambazo aliziona kuwa karibu  zimanza kwenda mbali. Sasa inajikuta iko peke yake zaidi na zaidi kwa sababu ya vita ya kipuuzi ambayo alianza kufikiria kushinda kwa muda mfupi. Sasa anapaswa kuwa na ujasiri wa kumaliza haraka vita hivi bila kushinda.

Ni wazi kwamba aliyeanzisha mzozo, ikiwa haleti ushindi nyumbani, yuko hatarini. Ndio maana hali ya leo  hii ni hatari sana. Wale ambao wamekata tamaa wanaweza kufanya ishara za kukata tamaa. Vitisho vya kutumia silaha za nyuklia sasa viko wazi. Umbali kati ya ujasiri na kukata tamaa ni mkubwa, lakini ikiwa wajasiri wataongezeka kwa idadi na kuungana basi historia inaweza kubadilika. Historia inafundisha kwamba watu huasi wakati ukosefu wa haki unazidi kiwango cha ulinzi. Tuko kwenye hatua ya kugeuka. Tatizo gumu zaidi ni kwamba Kremlin inaishiwa na chaguzi zake. Ni hatua za hatari sana kwa sababu chaguzi zimepunguzwa hadi mbili: kuwa na ujasiri wa kumaliza vita au kuhatarisha yote kwa kwenda mbele zaidi, ambapo vitisho vinakuwa ukweli. Na hivyo janga linaweza kuwa kubwa. Mungu atulinde.

Vita nchini Ukraine
26 September 2022, 14:53