Tafuta

Rushwa ni adui wa haki, utu na heshima ya binadamu. Wafanyakazi watekeleze wajibu wao kwa weledi, uaminifu na uadilifu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. Rushwa ni adui wa haki, utu na heshima ya binadamu. Wafanyakazi watekeleze wajibu wao kwa weledi, uaminifu na uadilifu kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya wengi. 

Rushwa ni Adui wa Haki, Utu, Heshima na Haki Msingi za Binadamu

Waziri mkuu amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uadilifu ili waweze kuleta matokeo chanya katika sekta mbalimbali za kimaendeleo na hawapaswi kuwa wala rushwa. Pia amewataka wafanyakazi kutoa huduma kwa wananchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, - Kigoma, Tanzania.

Rushwa ni adui wa haki, utu na heshima ya binadamu. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa weledi, uaminifu na uadilifu ili waweze kuleta matokeo chanya katika sekta mbalimbali za kimaendeleo na hawapaswi kuwa wala rushwa. Pia amewataka watumishi hao wahakikishe wanafanya kazi ya kutoa huduma kwa wananchi kwa kufuata taratibu zilizowekwa pamoja na kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao. Ameyasema hayo Jumamosi, Septemba 18, 2021 wakati akizungumza na watumishi wa umma wilayani Kibondo wakati akiwa katika ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo na shughuli za kijamii mkoani Kigoma. Amesema kuwa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajia kuona mipango yote ya Serikali inatekelezwa katika jamii kwani kufanya kazi kwa bidii kutasaidia wananchi kujishughulisha na mambo mengine ya maendeleo.

“Wito wa Rais Mheshimiwa Samia ni kuona uchumi unaenda kwa kasi kuanzia mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla, tulianza na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ili kuwawezesha watanzania kufanya shughuli zao za kiuchumi“Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kuwahamasisha na kuwawezesha Watanzania kujishughulisha shughuli za kiuchumi. “Kama ni mkulima alime sana, kwenye migodi wafanye kazi sana, wanafanyabiashara wafanye sana biashara hata wanaosoma wasome sana” Amesema watumishi washiriki kikamilfu katika kusimamia makusanyo ili kuwawezesha kutekeleza miradi wanayoiona italeta tija kwa wananchi. “Kigezo cha ukusanyaji wa mapato kipimwe kutokana na ujenzi wa miradi ambayo inawahudumia wananchi.” Waziri Mkuu pia amewaagiza Wakuu wa Wilaya wahakikishe kuwa miradi yote inayotekelezwa inakuwa na thamani ya fedha iliyotolewa “Wakurugenzi simamieni utekelezaji wa miradi katika maeneo yenu ili Wakuu wa Wilaya wakija kuizindua ionekane thamani ya mradi huo”.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa fedha nyingi kwa ajili ya uendelezaji na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya maji, elimu na barabara. Amesema lengo la utekelezaji wa miradi hiyo ni kuboresha maisha ya Watanzania, hivyo amewasihi wananchi wafanye kazi kwa bidii kila mmoja kwenye eneo lake na waendelee kuwa na imani na Serikali yao. Ameyasema hayo Ijumaa, Septemba 17, 2021 wakati akiongea na wananchi wa wilaya za Kasulu na Kibondo mkoani Kigoma baada ya kuzindua ghala la kuhifadhia mazao katika kijiji cha Mvugwe na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji Kifura. “Rais wetu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amedhamiria kupeleka huduma mbalimbali za jamii kwa wananchi wote nchini Tanzania. Huduma hizo ni pamoja na upatikanaji wa maji safi na salama kwa sababu anajua namna akinamama na vijana wanavyohangaika kutafuta maji.”

Naye, Meneja wa RUWASA mkoa wa Kigoma Mathius Mwenda alisema mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.4 mkataba wake ulisainiwa Agosti mwaka 2021 na unatarajiwa kukamilika Februari mwakani. Mradi huo utakapokamilika utakuwa na vituo 50 vya kuchotea maji.  Meneja huyo alisema kuwa kukamilika kwa mradi huo kunakwenda kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa kijiji cha Kifura, hivyo watahakikisha unakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyostahiki. Akizungumza kuhusu ujenzi wa mradi wa ghala la kuhifadhia mazao, Mheshimiwa Majaliwa aliwapongeza kwa kubuni mradi huo na alisisitiza kuwa wananchi hao waendeleze ushirika wao na watumie ghala hilo kwa ajili ya kuuza mazao yao. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Joseph Rwiza alisema mradi huo uliogharimu shilingi milioni 464 unalenga kupunguza upotevu wa mazao, kutunza na kuongeza ubora wa mazao pamoja na kuwepo kwa soko la uhakika na bei yenye tija kwa wakulima.

22 September 2021, 08:59