Tafuta

2021.11.11 Kwa sababu ya ukame na njaa watu wa Angola kusini walikimbia kwenda Namibia na sasa wanaomba msaada baada ya kunyesha mvua na kukosa mahali pa kukaa. 2021.11.11 Kwa sababu ya ukame na njaa watu wa Angola kusini walikimbia kwenda Namibia na sasa wanaomba msaada baada ya kunyesha mvua na kukosa mahali pa kukaa. 

Namibia:wahamiaji kutoka Angola wanateseka na ukosefu wa makazi

Wahamiaji kutoka Angola waliofika kwenye kambi moja nchini Namibia kutokana na balaa la ukame na njaa sasa wanateseka sana baada ya kuanza kipindi cha mvua licha ya uwepo wa nge na nyoka wenye sumu.Wakimbizi wameandika barua kuomba msaada wa haraka wakishukuru serikali ya Namibia kwa msaada wanao utoa japokuwa hawawezi kumalisha shida hii bila msaada.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Kwa kufikia kipindi cha mvua, lakini inaongeza ugumu kwa wahamiaji wa Angola. Hali duni ya maisha ya wahamiaji hao sasa inazidishwa na hali mbaya ya hewa pamoja na uwepo wa nge na nyoka wenye sumu. Kwa mujibu wa barua iliyotumwa kwa kwa shirika la Habari za kimisionari Fides, tangu mvua zianze kunyesha mashamba wanayoishi watu hao yamefurika kabisa na familia za wahamiaji zimelazimika kwenda kulala kwenye baa za Buca, nyumba zisizo na leseni inayouza pombe, au kwenye familia katika eneo la Etunda. Watoto wako katika  hatari kubwa sana kwa mujibu wa barua hiyo na kwamba Wiki tatu, wakilala kwenye makambi chini ya blanketi zilizolowa. Kundi la kwanza liliwasili mapema mwezi Machi mwaka huu, ili kuepuka njaa na ukame kutoka katika makazi yao ya awali. Zaidi ya watoto 50 wamezaliwa tangu wakati huo. Hawa wanahitaji nguo na chakula, kwani kile wanachopokea kutoka kwa wafadhili kinaisha haraka, kutokana na ongezeko la wahamiaji.

wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada
wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada

Hata hivyo barua inabainisha kushukuru serikali ya Namibia kwa kuwatunza kila mara tangu twalipofika Namibia, kwa mujibu wa  baadhi ya wahamiaji ambao wanaendelea kuiomba serikali ya Namibia kuwasaidia ili kupata makazi wakati wa mvua hizo. Kwa upande wake gavana wa Omusati Erginus Endjala amesema kuwa ofisi yake haina vifaa na fedha za kutosha kujenga vibanda vya wakimbizi hivyo anatoa wito kwa taifa, wafanyabiashara na viongozi wa kisiasa kujumuika pamoja kusaidia watu hawa ili kujenga kambi za wakimbizi.na kuwawekea usafi wa mazingira wa kutosha.

wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada
wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada

Katika Nchi hiyo Kanisa Katoliki linasikika sana. Takriban asilimia 40-50% ya shule nchini Namibia zimejengwa na wamisionari wa Kikristo, pamoja na vituo vingi vya afya. Hospitali ya wamisionari ya Onandjokwe ni maarufu, katika eneo la kabila la Ondonga huko Ovamboland, iliyoanzishwa na Selma Raino, daktari mmoja wa kimisionari kutoka Finland. Tangu siku za vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoharibu  nchi ya Angola, wahamiaji wanaotafuta maisha bora walikwenda  Namibia zaidi ya yote kutoka nchi hiyo  inayoteswa sana. Walihama kutafuta kazi ya kuvuna na kupura mahangu ambayo ni aina ya ngano.

wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada
wakimbizi wa Angola waliopo Namibia wanaomba msaada
26 November 2021, 12:47