Tafuta

25.11.2021: Kukomesha ukatili wa kijinsia ni moja ya changamoto kubwa duniani kwani takribani mwanamke 1 kati ya 3 ulimwenguni amekumbwa na ukatili,huku majanga yakisababisha takwimu kuwa juu zaidi. 25.11.2021: Kukomesha ukatili wa kijinsia ni moja ya changamoto kubwa duniani kwani takribani mwanamke 1 kati ya 3 ulimwenguni amekumbwa na ukatili,huku majanga yakisababisha takwimu kuwa juu zaidi. 

Siku ya Kimataifa ya kukomesha ukatili wa kijinsia:Uviko-19 umezidisha sana

Takribani mwanamke 1 kati ya 3 ulimwenguni amekumbwa na ukatili,huku majanga yakisababisha takwimu kuwa juu zaidi. Ukatili wa kijinsia ni moja ya vitendo vya ukiukwaji mkubwa zaidi wa haki za binadamu si jambo ambalo ni la kiasili au halikwepeki na linapaswa kuzuiwa.Katika kuadhimisha siku XVI za harakati za kupinga ukatili dhidi ya wanawake shirika la UN la kushughulikia masuala ya wanawake,‘UN Women’ linabainisha takwimu mpya ni udharura wa juhudi za pamoja.

Ripoti mpya iliyotolewa na Shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa UN Women ambayo iliangazia athari za janga la COVID-19 kwa usalama wa wanawake nyumbani na katika maeneo ya umma imeonesha kuwa hisia za usalama za wanawake zimepotea, na kusababisha athari mbaya kwa hali yao ya kiakili na kimihemko. Ripoti hiyo iliyotolewa tarehe 24 Novemba ikiwa ni siku moja kabla ya siku ya Kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake ambayo ufanyika kila mwaka ifikapo tarehe 25 Novemba wakati ambapo ulimwengu unaanza siku  Siku 16 za kuhamasisha  kupinga Ukatili wa Kijinsia. Mkurugenzi Mtendaji wa UN WOMEN Bi Sima Bahous amesema unyanyasaji dhidi ya wanawake ni mgogoro uliopo wa kimataifa ambao unastawi kutokana na kuwepo kwa migogoro mingine duniani. Migogoro ya  majanga ya asili yanayohusiana na mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa uhakika wa chakula na ukiukaji wa haki za binadamu vyote huchangia wanawake na wasichana kuishi katika hali ya hatari, hata katika nyumba zao na jamii zao.

Kwa mujibu wa Bi amesema  Bahous: “Janga la COVID-19, ambalo lililazimu kukakaa karantini na kutengwa kwa jamii, liliwezesha kuzuka kwa  janga la pili la kivuli cha  ukatili dhidi ya wanawake na wasichana, ambapo mara nyingi walijikuta wamefungwa na wanyanyasaji wao. Takwimu zetu mpya zinasisitiza udharura wa juhudi za pamoja kukomesha hili,”. Maadhimisho ya siku XVI ya  kupinga ukatili wa kijinsia   mwaka huu ambayo kwa siku kumi na sita hadi tarehe 10 Desemba mwaka huu yanaongoza na  kaulimbiu ya kimataifa ya  Kampeni iliyowekwa na  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa isemayo:“Orange the World: Tokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake Sasa ”.

Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake
Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Ripoti hiyo imeonesha karibu mwanamke 1 kati ya 2 aliripoti kwamba yeye au mwanamke anayemjua alikumbwa na hali fulani ya ukatili tangu kuzuka kwa janga la COVID-19 lianze. Wanawake ambao waliripoti hali hii walikuwa na uwezekano mara 1.3 zaidi wa kuripoti kuongezeka kwa athari kiakili na mihemko kuliko wanawake ambao hawakuripoti. Matokeo hayo pia yamefichua kuwa takriban mwanamke 1 kati ya 4 anahisi kuwa salama nyumbani huku migogoro iliyopo imeongezeka ndani ya kaya tangu janga hili lianze. Wanawake walipoulizwa kwa nini walijihisi kutokuwa salama nyumbani, wametaja unyanyasaji wa kimwili kuwa mojawapo ya sababu (21%). Baadhi ya wanawake waliripoti hasa kwamba waliumizwa na wanafamilia wengine (21%) au kwamba wanawake wengine wanaowafahamu  katika kaya walikuwa wakiumizwa (19%). Kwa upande wa nje ya nyumba zao, wanawake pia wanahisi kuathiriwa zaidi na dhuluma, huku 40% ya waliohojiwa wakisema wanahisi salama kidogo kutembea peke yao usiku tangu kuanza kwa COVID-19.  Takriban wanawake 3 kati ya 5 pia wanafikiri kuwa unyanyasaji wa kijinsia katika maeneo ya umma umezidi kuwa mbaya wakati wa janga la COVID-19.

Kwa maelezo zaidi bonyeza hapa: https://data.unwomen.org/sites/default/files/documents/Publications/Measuring-shadow-pandemic.pdf

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres amesema unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana umeendelea kuwa suala linaloenea na linaloonesha ukiukwaji wa haki za binadamu duniani leo. Amesema suala hilo ni uhalifu wa kuchukiza na ni dharura ya afya ya umma, yenye madhara makubwa kwa mamilioni ya wanawake na wasichana katika kila kona ya dunia. Ameeleza takwimu zilizotolewa na UN Women zinathibitisha kwamba wakati wa janga la COVID-19, viwango vya ukatili dhidi ya wanawake na wasichana vimeongezeka. “Unyanyasaji dhidi ya wanawake hauepukiki. Sera na mipango sahihi huleta matokeo. Hiyo ina maana ya kuwa mikakati ya kina, ya muda mrefu ambayo inakabiliana na visababishi vikuu vya unyanyasaji, kulinda haki za wanawake na wasichana, na kukuza vuguvugu dhabiti na linalojitegemea la haki za wanawake. Mabadiliko yanawezekana, na sasa ni wakati wa kuongeza juhudi zetu ili kwa pamoja tuweze kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ifikapo mwaka 2030,” amesisitiza Katibu Mkuu Guterres.

Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake
Siku ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake

Na Wataalam wa Umoja wa Mataifa na wale wa kikanda wametoa wito kwa mataifa yote ulimwenguni kufanya bidii ipasavyo na kuondoa vipingamizi vinavyokwamisha usawa wa kijinsia. Taarifa ya wataalamu hao iliyotolewa katika fursa hiyo mjini Geneva, Uswisi imesema wanawake na wasichana kila mahali wanaendelea kukabiliwa na aina nyingi za ukatili wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na mauaji ya wanawake, ukatili mtandaoni na unkatili wa majumbani.

26 November 2021, 13:28