Tafuta

ILO:Wengine wanaweza kusema kwamba ajira ya Watoto ni athari ya umaskini ambayo haiepukiki na kwamba ni lazima tuikubali.Lakini hilo si sahihi,kamwe hatuwezi kukumbatia ajira ya watoto. ILO:Wengine wanaweza kusema kwamba ajira ya Watoto ni athari ya umaskini ambayo haiepukiki na kwamba ni lazima tuikubali.Lakini hilo si sahihi,kamwe hatuwezi kukumbatia ajira ya watoto. 

ILO:Bara la Afrika linaongoza kwa ajira za watoto&ni ukiukwaji wa haki msingi

Rais wa Afrika Kusini katika hotuba ya ufunguzi wa Kongamano la V la Kimataifa kuhusu kutokomeza ajaira za utotoni:“Hakuna ustaarabu,hakuna nchi na hakuna uchumi unaoweza kujiona kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ikiwa mafanikio na utajiri wake umejengwa juu ya migongo ya watoto”. Wito huo umeungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa ILO Bwana Guy:“Ajira ya Watoto ni ukiukwaji wa haki msingi na malengo ya SDGs.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Kongamano la V la kimataifa kuhusu kutokomeza ajira ya watoto duniani lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kazi duniani ILO, limefunguliwa mnamo tarehe 16 Mei 2022 huko mjini Durban nchini Afrika Kusini kwa kutoa  wito wa kutaka kuchukuliwa hatua za haraka ili kukabiliana na ongezeko la idadi ya watoto wanaotumbukia katika ajira za utotoni. Akizungumza katika ufunguzi wa wiki ya majadiliano ya mkutano huo unaofanyika ana kwa ana na kwa njia ya mtandaoni, Rais wa Afrika Kusini, Bwana Cyril Ramaphosa amewataka wajumbe kujitolea kuchukua hatua mbali mbali kuleta mabadiliko katika maisha ya watoto, akielezea utumikishwaji wa watoto kama ajira ya watoto na ni adui wa makuzi ya watoto wote na adui wa maendeleo yak ila taifa, na hasa kwa upande wa Afrika.

Hakuna ustaarabu, hakuna nchi na hakina uchumi wa maendelo juu ya migongo ya watoto

Rais wa Afrika Kusini katika hotuba hiyo alisema kwamba “Hakuna ustaarabu, hakuna nchi na hakuna uchumi unaoweza kujiona kuwa mstari wa mbele katika maendeleo ikiwa mafanikio na utajiri wake umejengwa juu ya migongo ya watoto”.  Wito wake umeungwa mkono na mkurugenzi mkuu wa ILO Bwana Guy Ryder ambaye amesisitiza kwamba “Ajira ya Watoto ni ukiukwaji wa haki za msingi na malengo yote na hivyo lazima liwe kwamba kila mtoto kila mahali anakuwa huru dhidi ya ukiukwaji huo. “Hatuwezi kupumzika hadi pale lengo hilo litakapotimia. Wengine wanaweza kusema kwamba ajira ya Watoto ni athari ya umaskini ambayo haiepukiki na kwamba ni lazima tuikubali. Lakini hilo si sahihi, kamwe hatuwezi kukumbatia ajira ya watoto”, Bwana Ryder alisisitiza.

Mwisho wa lengo la (SDGs) la kutokomeza ajira ya watoto kukaribia 2025

Huku kikomo cha  lengo la maendeleo endelevu la kutokomeza ajira ya watoto ifikapo mwaka 2025 ukikaribia, wazungumzaji wengi kwenye mkutano huo wameeleza haja ya haraka ya kurejesha maendeleo ambayo yalikuwa yamefanywa katika kanda nyingi kabla ya janga la UVIKO-19.  Takwimu za hivi karibuni za ILO zinaonesha kuwa watoto milioni 160 karibu mtoto 1 kati ya 10 ya watoto wote ulimwenguni bado wako katika ajira ya watoto.  Na idadi inaongezeka, na janga hilo linatishia kurudisha nyuma miaka ya maendeleo yaliyopigwa.  ILO inasema ajira ya watoto imeongezeka hasa katika kundi la umri wa miaka 5 hadi 11.

Bara la Afrika linaongoza kwa ajira za utoto hasa katika kilimo

Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano wa kimataifa wa kutokomeza ajira ya watoto kufanyika barani Afrika katika  eneo ambalo kwa kuzingatia takwimu idadi ya watoto wanaotumikishwa iko juu zaidi na hatua za kuitokomeza yamekuwa ya polepole zaidi.  Shirika la Kazi  duniani linasema ajira nyingi za watoto katika bara la Afrika kwa asilimia 70 ni katika kilimo, mara nyingi katika mazingira ambayo watoto wanafanya kazi pamoja na familia zao.  Katika Mkutano huo utaendeleza yaliyojiri katika mikutano minne ya awali ya kimataifa, iliyofanyika huko: Buenos Aires (2017), Brasilia (2013), The Hague (2010), na Oslo (1997), ambayo iliibua ufahamu wa suala hilo, kutathmini maendeleo, kuhamasisha rasilimali na kuanzisha mwelekeo wa kimkakati wa harakati za kimataifa dhidi ya ajira ya watoto.  Mkutano huo unatarajiwa kuhitimisha kwa “wito wa Durban wa kuchukua hatua” ambao utaelezea ahadi madhubuti za kuongeza hatua za kukomesha ajira ya watoto.

KONGAMANO LA V KIMATAIFA LA ILO AFRIKA KUSINI
17 May 2022, 09:18