Tafuta

2019.11.28 Askofu Mathew Kukah wa  Sokoto nchini  Nigeria na mapadre wengine. 2019.11.28 Askofu Mathew Kukah wa Sokoto nchini Nigeria na mapadre wengine. 

Nigeria:Mwanafunzi apigwa mawe na kuuawa.Viongozi wa dini wadai ukweli

Ni sauti moja, Waislamu na Wakristo kwa pamoja, wanalaani kitendo hicho cha kikatili na wanatoa wito kwa mamlaka ya Serikali ya Sokoto kubaini sababu na kujaribu kuweka utulivu nchini.Sultan Saad Abubakar na Askofu wa Jimbo la Sokoto,eneo la tukio kuhusu mwanafunzi huyo aliyepigwa mawe hadi kuuwa hawaachi kuomba utulivu.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo Nchini Nigeria wamelaani vurugu zisizo na sababu na uhalifu ikiwa ni pamoja na mamlaka ya juu zaidi,  kwa Sultan Saad Abubakar, wakati Askofu wa Jimbo la Sokoto, eneo la tukio kuhusu mwanafunzi aliyepigwa mawe hadi kuuwa haachi kuomba utulivu. Kwa mujibu wa Askofu  Mathew Hassan Kukah akishangazwa na tukio hilo, ameomba haki itendeke kwa kitendo cha kihalifu, kisicho cha kibinadamu na kisichohusiana na dini. Kwa maana hiyo Wakristo na Waislamu katika ujumbe uliochapishwa kwenye tovuti ya Jimbo unabainisha kuwa daima wameishi pamoja kwa amani kwa miaka mingi.

Shuhuda zilizochapishwa na vyombo vya habari

Kulingana na shuhuda, zilizochapishwa na vyombo vya habari vya ndani, mwanafunzi anadaiwa kumshutumu kijana Deborah Samuel, aliyejiandikisha katika Uchumi, kwa kuchapisha matusi kwa Mtume Muhammad kwenye gumzo la kikundi cha wanafunzi. Kwa maana hivyo kuibuliwa kwa wazimu wa pamoja ambao ulikuwa kama ukumbi wake wa maonesho katika Chuo cha Elimu cha ShehuShagari cha Serikali ya  Sokoto kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Wanafunzi wenzake wa Kiislamu dhidi ya kijana huyo kijana Mkristo walimtoa nje ya shule ambako alikuwa ametafuta hifadhi na ulinzi bila mafanikio, na wakaanza kumpiga mawe na kumchoma moto mwili wake.Tayari wahusika wametambuliwa kutokana na video inayothibitisha kifo hicho kibaya, kilichothibitishwa na polisi wa Sokoto, huku Taasisi hiyo ikifungwa kwa amri ya serikali kwa muda usiojulikana.

Mauaji hayo ni ya kutisha

Shirika la Kipapa la Kanisa Hitaji katika Nchi ya Afrika linasema, limeshtushwa sana na mauaji haya ya kutisha. Hali ya itikadi kali na ghasia nchini katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ya kutisha. Karibu kila wiki kuna utekaji nyara na makumi ya vifo, lakini kitendo hiki cha kinyama kimewaacha hoi, kwa mujibu wa wa Thomas Heine-Geldern, rais mtendaji wa Wa Mfuko huo wa Kipapa. Kwa maana hiyo mawazo yake yamewaendea familia na jumuiya ya Kikristo na pia ombi la kulaani kwa kauli moja aina zote za itikadi kali.

Utekelezaji wa sheria ya sharia

Katika taarifa hiyo, Mfuko wa Kipapa wa Shrika Hitaji limekumbusha pia kwamba tangu  1999, majimbo kumi na mbili ya kaskazini mwa Nigeria yamepitisha kanuni za uhalifu za Sharia, sambamba na mahakama za kiutamaduni na kimila. Sheria nyingi za Sharia kaskazini mwa Nigeria hutoa sheria kali sana kwa adhabu kwa kukufuru, hadi hukumu ya kifo. Hata hivyo, Sharia inahakikisha angalau kesi ya haki, bila ya kutumia dhuluma na utekelezaji wa muhtasari, kama katika kesi mbaya ya Sokoto, ambaye sio wa kwanza nchini humo. Kwa mujibu wa ripoti ya mwisho kuhusu uhuru wa kidini, wa Mfuko wa Acs, d baada ya miaka 20 ya sharia, hali ya kaskazini mwa Nigeria imezidi kuwa mbaya. Ukabila na udini umekuwa njia mwafaka ya kupata mamlaka, rasilimali na mapendeleo. Kwa mujibu wa  ripoti ya ACS, sheria ya sharia imegawanya zaidi nchi.

14 May 2022, 14:51