Tafuta

Vita nchini Ukraine vinaendelea kuharibu miundo mbinu Vita nchini Ukraine vinaendelea kuharibu miundo mbinu  

Bi Von der Leyen atembelea kwa upya mji wa Kiev na kukutana na rais Zelenski

Hofu katika mji wa Kryvyi Rih nchini Ukraine kuhusu shambulio la kombora la Urusi kwenye bwawa.Rais Zelenski ametembelea maeneo yaliyotekwa kwa upya na kuahidi kuendelea hadi ushindi.Moscow inaionya Marekani kutosambaza makombora ya masafa marefu kwa Kiev ili kuepuka kueneza mzozo huo.

Na Angella Rwezaula - Vatican

Mvutano wa kimataifa kuhusiana na mzozo wa Ukraine bado haujapungua na wakati huo huo Moscow ikionya  kwamba ikiwa Kiev itapata makombora ya masafa marefu kutoka Marekani, hii itamaanisha kuhusika moja kwa moja kwa Marekani katika makabiliano ya kijeshi na Urusi. Tarehe 15 Septemba 2022 Rais wa Tume ya  Umoja wa Ulaya, Bi Ursula Von der Leyen, aliwasili katika mji mkuu wa Ukraine. Katika ujumbe wake mfupi wa tweet aliandika kuwa ziata take ya tatu huko tangu mwanzo wa vita vya Urusi. Mengi yamebadilika na  Ukraine sasa ni nchi Mgombea wa Umoja wa Ulaya. Bi Ursula alisema atajadiliana na Rais Zelensky jinsi ya kuendelea kuleta uchumi wao na watu wao karibu zaidi wakati Ukraine inapoelekea kwenye uanachama wa Umoja wa Ulaya.   

Mkutano wa Samarkanda

Rais wa Urusi, Vladimir Putin, badala yake amewasili Samarkand, nchini Uzbekistan, kwa ajili ya mkutano wa viongozi wa nchi za Jumuiya ya Ushirikiano wa Shanghai (SCO), kulingana na ripoti kutoka  Interfax. Hata hivyo kuna subira ya mkutano ambao mkuu wa Kremlin atakuwa na Rais wa China Xi Jinping, ambaye alifika kwenye mkutano huo tarehe 14 Septemba usiku. Mkutano huo ni wa kwanza kati ya viongozi hao wawili tangu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ulipoanza mnamo Februari 24.

Hali juu ya ardhi

Tarehe 14 Septemba Rais wa Ukraine Zelenski alitembelea eneo la Kharkiv ambalo ni karibu sana  kukombolewa lililoachiliwa na  uvamizi wa Urusi na kulitaka jeshi kusonga mbele na kushinda. Mkuu huyo wa nchi ambaye pia alipata hata  ajali ya barabarani, aliingia katika jiji la Izyum na kusema kuwa bendera ya Ukraine itapepea katika kila kijiji nchini humo. Ardhini bado kuna milipuko ya mabomu. Makombora manane ya kivita ya Urusi yaligonga bwawa la Kryvyi Rih tarehe 14 Septemba alasiri na baadhi ya wakazi walihamishwa baada ya Mto Inhulets kufurika mitaani. Kiwango cha maji katika Mto Ingulets huko Kryvyi Rih, mkoa wa Dnipropetrovsk kilipungua kwa sentimita 40 alhamisi 15 Septemba  na kinaendelea kushuka.

Makombora yanazidi kuharibu Zaporizhzhia

Haya yalitangazwa na mkuu wa kijeshi wa mkoa wa Dnipropetrovsk, Valentin Reznichenko: "Shukrani kwa washiriki wa kwanza, kwa huduma za dharura na kwa wale wote waliofanya kazi mara moja na kuendelea kufanya kazi sasa. Kila mmoja wao aliongeza amefanya kazi ya ajabu sana. Mashambulizi mapya pia huko Zaporizhzhia, mji ulio kusini mwa Ukraine karibu na kinu kikubwa cha nyuklia kinachodhibitiwa na Moscow. Meya huyo alisema shambulio la kombora lililofanywa na wanajeshi wa Urusi katika mji huo lilisababisha uharibifu kadhaa, na kuvunja madirisha ya kiwanda na kusababisha kukatika kwa umeme kwa muda. Hakuna majeruhi walioripotiwa.

15 September 2022, 15:28