Tafuta

Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula Von der Leyen akihutumia Bunge 14 Septemba 2022. Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula Von der Leyen akihutumia Bunge 14 Septemba 2022.  (AFP or licensors)

Umoja wa Ulaya,Von der Leyen:kuunga mkono Ukraine na vikwazo vya

Katika hotuba yake kuhusu hali ya Umoja wa Ulaya,aliyoitoa tarehe 14 Septemba 2022 katika Bunge la Strasbourg,rais wa Tume,Bi Ursula Von del Leyen,alisisitiza uungaji mkono wake kwa Ukraine na mkakati wa vikwazo dhidi ya Urusi,kwa kutafuta njia za kushinda mgoro wa nishati uliosababishwa na vita kati ya Kiev na Moscow.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hotuba nyuzi 360 iliyotolewa  asubuhi tarehe 14 Septemba 2022  katika jengo la Bunge la Ulaya huko Strasbourg kuhusu Muungano wa nchi  27 wa Bara la Ulaya. Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula Von der Leyen, aliweza kutoa nuru ya  mzozo wa nchini Ukraine.Katika Mkutano huo alikuwapo   hata Olena Zelenski, mke wa rais wa Ukraine, Volodomyr Zelenski. Bila wasi wasi, Bi Ursula alisema kuwa hiyo sio vita tu ya  Urusi dhidi ya Ukraine, ni vita dhidi ya nishati yao,  uchumi wao, maadili yao na demokrasia. Kwa ujasiri na mshikamano alisisitiza kwamba Putin atashindwa, na kwa maana hiyo Ulaya na Ukraine zitashinda. Kwa mujibu wa Bi  Von der Leyen, sera ya vikwazo, inayokusudiwa inabaki kuwa  na nguvu kwa muda mrefu, na ndio mkakati wa  kuendelea kushinda  Moscow.

Rais wa Tume ya Ulaya akihutubia Bunge la Ulaya
Rais wa Tume ya Ulaya akihutubia Bunge la Ulaya

Lakini lengo kuu, alisisitiza rais wa Tume ya Ulaya, sio tu kusaidia Kiev ili kushinda vita hivi kwa kila njia, lakini pia ni mpango wa kuleta nchi ya Ukraine ili kuwa karibu na soko moja. Kuhusu hili na zaidi, alisema, atakavyoweza kuzungumza moja kwa moja na Rais Zelenski, ambaye angekutana naye huko Kiev siku hiyo.

Rais wa Tume ya Ulaya akihutubia Bunge la Ulaya
Rais wa Tume ya Ulaya akihutubia Bunge la Ulaya

Mada nyingine nzito iliyokabiliwa na Bi Ursula Von der Leyen ni ile ya uhuru wa nishati, ambayo Ulaya yote lazima ifuate ili kujikomboa kutoka mikononi mwa utegemezi wa hidrokaboni za Kirusi. Kwa kuwa na ufahamu kamili wa matatizo ambayo familia za Ulaya zinapitia kwa usahihi kwa sababu ya kuongezeka kwa bei ya mafuta, gesi na umeme alisema kwamba “Mamilioni ya Watu wa Ulaya wanahitaji msaada na Mataifa Wanachama tayari yamewekeza mabilioni ya euro kusaidia familia zilizo hatarini zaidi. Lakini tunajua haitatosha. Kwa sababu hii tunapendekeza kupunguzwa kwa mapato ya kampuni zinazozalisha umeme wa bei ya chini . Pendekezo hili, kwa nia ya Von der Leyen, litafanya uwezekano wa kuongeza zaidi ya euro bilioni 140 ambazo zitasaidia kukabiliana na tatizo  la nishati ya gharama kubwa.

Rais wa Bunge la Ulaya Bi Roberta Metsola,Olena Zelenska mke wa Rais na Rais wa Tume ya Ulaya Be von der Leyen
Rais wa Bunge la Ulaya Bi Roberta Metsola,Olena Zelenska mke wa Rais na Rais wa Tume ya Ulaya Be von der Leyen

Mabadiliko hayo, kwa mujibu wa Kiongozi huyo anasema, hata hivyo, lazima yafanyike katika ngazi zote. “Tunahitaji mpango wa kuokoa nishati kutekelezwa familia kwa familia, jiji kwa jiji, nchi kwa nchi. Kuhama kwa nishati mbadala basi ni muhimu na zaidi ya yote kufuata uhuru wa nishati kuhusiana na vyanzo vya jadi. Katika mazoezi, jiepushe na utegemezi wa gesi ya Kirusi kwa njia zote. Ni kwa njia hii tu, Bi Ursula Von der Leyen alihitimisha, itawezekana kuleta bei ya gesi chini ya euro 100 kwa saa ya megawati tayari mwanzoni mwa mwaka ujao.

Hatimaye, Bi Ursula Von del Leyen alihimiza  kama jukumu kubwa la nchi wanachama kuheshimu yale ambayo yamekubaliwa, pia shukrani kwa mageuzi ya Mkataba wa Utulivu, ambao unapaswa kuzingatia sheria rahisi ambazo kila mtu anaweza kufuata.

15 September 2022, 14:43