Tafuta

Tarehe 9 Januari 2023 katika mapigano na wanajihadi jeshi la Mali linadai kuwa limepunguza magaidi 31. Tarehe 9 Januari 2023 katika mapigano na wanajihadi jeshi la Mali linadai kuwa limepunguza magaidi 31.  (AFP or licensors)

Mali:Bado ni janga katika kijiji cha Douna,kinachotishiwa na wanajihadi!

Ripoti ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,(UN) iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama mnamo tarehe 9 Januari 2023,inasema kuwa hali ya usalama iliendelea kuzorota kati ya mwezi Juni na Desemba 2022 katikati mwa Sahel,hasa katika nchi ya Burkina Faso na Mali.Mnamo tarehe 9 Januari 2023 katika mapigano na wanajihadi jeshi la Mali linadai kuwa limepunguza magaidi 31.

Na Angella Rwezaula; – Vatican.

Mali imekuwa ikiteseka tangu mwaka 2012 kutokana na ghasia zinazofanywa na makundi mbalimbali ya wanajihadi. Katikati ya nchi hiyo ni moja wapo ya maeneo yenye machafuko ambayo yameenea katika nchi jirani, kama vile Burkina Faso na Niger, na yanaenea kuelekea kusini. Askofu Jean Baptiste Tiama, wa Jimbo la  Mopti, nchini Mali akielezea kwa shirika la habari za kimisionari Fides kuhusu hali ya jumuiya ya Kikristo ya Douna (parokia ya Barapireli) inayotishiwa na wanajihadi. hivi karibuni alisema: “ Hali  halisi bado imezuiwa. Tunaendelea kuwaombea ndugu zetu huku tukitumaini kuwa juhudi za upatanishi zitafanikiwa ili kuruhusu waamini kuendelea kuishi kwa amani.”

Kwa muda kijiji cha Douna kimetishiwa na wanajihadi

Mnamo tarehe 4 Januari wanajihadi walirudi kijiji tena cha Douna na  kulazimisha jumuiya mbili za Kikristo kufunga makanisa kwa mujibu wa taarifa ya tarehe 5 Januari  2023, kutoka Jimbo la Mopti, iliyotumwa katika Shirika la Habari za Kimisionari Fides.  Kwa njia hiyo: “Sasa ni marufuku kupiga kengele, kupiga ala za muziki na kusali makanisani. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba wanajihadi wanaomba Wakristo kufuata dini ya Kiislamu” alisisitiza Askofu wa Jimbo la Mopti ambapo aliwaalika waamini kudumu katika maombi ili kushinda nguvu za uovu. Hasa katika eneo la Mopti, katikati mwa Mali, wanajeshi kumi na wanne wa Mali waliuawa na kumi na mmoja kujeruhiwa mnamo tarehe 9 Januari  2023 katika mapigano na wanajihadi. Kwa upande wake, jeshi la Mali linadai kuwa limepunguza magaidi 31.

Ghasia na makundi ya kijihadi

Mali imekuwa ikiteseka tangu mwaka 2012 kutokana na ghasia zinazofanywa na makundi mbalimbali ya wanajihadi. Katikati ya nchi hiyo ni moja wapo ya maeneo yenye machafuko ambayo yameenea katika nchi jirani, kama vile Burkina Faso na Niger, na yanaenea kuelekea kusini. Miaka 10 tu iliyopita mnamo tarehe 11 Januari 2013, Ufaransa ilianzisha Operesheni Serval ili kuzima hujuma ya jihadi ambayo ilitishia kuzidisha nchi. Sasa hali imebadilika. Wapangaji wa mapinduzi ya kijeshi ambao walichukua madaraka huko  putsch mnamo 2020, na kufuatiwa na mapinduzi ya pili mnamo 2021, wamejitenga na mshirika wa zamani wa Ufaransa na washirika wake, na wamegeukia kijeshi na kisiasa kwa Warussi.

Operesheni na mapigano  tarehe 9 Januari 2023

Ongezeko la kijeshi lilianzisha operesheni iliyolenga eneo la kati la Mali mwishoni mwa 2021, ikisema kuwa iliwalazimu wanajihadi kutoroka na kukimbia. Hata hivyo, ripoti ya Katibu Mkuu wake wa Umoja wa Mataifa,(UN) iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama mnamo tarehe 9 Januari 2023, inasema kuwa hali ya usalama iliendelea kuzorota kati ya mwezi Juni na Desemba 2022 katikati mwa Sahel, hasa ​​katika nchi ya Burkina Faso na Mali. Nchini Mali hata hivyo baada ya kuondoka kwa vikosi vya kimataifa, makundi yenye silaha yalisonga mbele mashariki mwa nchi, yakichukua udhibiti wa maeneo makubwa ya mpaka na Niger", kwa mujibu wa ripoti hiyo.

12 January 2023, 13:15