Tafuta

Bi Jill Biden, Mke wa Rais wa Marekani akitembelea kituo cha familia cha Mtakatifu Diego huko Califonia,katika siku ya Saratani duniani 4 Februari 2023. Bi Jill Biden, Mke wa Rais wa Marekani akitembelea kituo cha familia cha Mtakatifu Diego huko Califonia,katika siku ya Saratani duniani 4 Februari 2023. 

Kuongeza kwa kasi ya maarifa huzidisha matumaini ya kuponya saratani

Katika toleo la XXIII la Siku ya Saratani Duniani iliyonzishwa na Umoja wa Mataifa wa Kudhibiti Saratani (UICC) na kuungwa mkono na Shirika la Afya Duniani(WHO), inawakilisha wito muhimu wa kutafakari juu ya nini taasisi na watu binafsi kwa pamoja wanaweza kufanya katika kupambana na saratani kuanzia kinga na elimu.

Na Angella Rwezaula: - Vatican.

Katika kauli mbiu iliyoongoza Siku ya XXIII ya Kimataifa na kupambana  na Saratani Ulimwenguni kwa mwaka 2023 inasema “Kesi huongezeka kidogo lakini muhimu zaidi kuishi na kurefushwa.  Kattika taarifa  kuhusu siku hii wanabainisha kwamba kuna ongezeko kidogo la kesi ambalo bado katika miaka 15 iliyopita, kutokana na matibabu mapya, kuna sababu nzuri ya kuishi  watu 2.5 hadi milioni 3.6 na saratani miaka mitano baada ya kugunduliwa.

Ufikiaji sawa wa utunzaji kwa wote

Mada ya kampeni ya 2022-2024  ambayo ni “Funga Pengo la Utunzaji: Kila mtu anastahili kupata huduma ya saratani. Kauli mbiu inayotaka kumulika jinsi ilivyo muhimu kuelewa na kutambua ukosefu wa usawa katika utunzaji wa saratani ulimwenguni kote. Ukosefu wa usawa ambao unasisitiza tofauti katika upatikanaji wa matibabu ya ugonjwa ambao kiukweli unazidi kutibika, hasa ikiwa utatambuliwa kwa wakati. Na katika hilo, kinga na elimu ni mambo msingi.

Kuna utofauti wa miaka ya nyuma na sasa

Kwa kisikiliza maoni  kutoka katika mahojiano na Profesa Paolo Tortora ambaye ni  mkurugenzi wa Kitengo cha (Oncology) Matibabu  ya Saratani cha Hospitali ya Gemelli Jijini Roma, alielezea hali ya sasa kwamba kwa Italia inahusika, katika mwaka  2022 kulikuwa  na ongezeko la matukio ya saratani karibu 4% kwa wanaume na 0.7 kwa wanawake wenye wastani wa 1%. Inawezekana kwamba hiyo pia ni kwa sababu ya ukweli kwamba utambuzi haujafanywa mapema kwa sababu ya janga la uviko. Kwa hivyo, ongezeko kidogo lilirekodiwa kwa aina zote za saratani. Walakini, ikiwa tutazingatia kunusurika, ambayo ni dhahiri inahusishwa na maendeleo katika matibabu na uchunguzi, inaweza kuonekana kuwa kumekuwa na kiwango kikubwa katika miaka 15 ambayo labda hatungetarajia,” alisema daktari huyo.

Ujumbe wa matumaini

Kugunduliwa na saratani mapema kungeshtua mtu yeyote, lakini kuna matumaini. Daktari Tortorella alisema kwamba katika miaka ya hivi karibuni amekuwa akiona mambo ambayo hakuwahi kuyaona katika miongo iliyopita. Kwa kufanya utafiti, hata wa kwanza, kuna matumaini ya kuweza kuponya ugonjwa. Kwa wale wanaougua, uwezekano wa kupona ni wa juu sana kuliko hapo awali. Kuongeza kasi hii ya maarifa kunaongoza utafiti katika mwelekeo unaotakiwa. Huu ni ujumbe ambao ninahisi kuutoa, kwa uaminifu na utulivu uliokithiri”, alihitimisha Tortorella.

Kila tarehe 4 Februari ni siku ya Saratani duniani
06 February 2023, 16:05