Tafuta

2023.02.08 Siku ya Kimataifa ya tafakari kuhusu biashara haramu ya binadamu. 2023.02.08 Siku ya Kimataifa ya tafakari kuhusu biashara haramu ya binadamu. 

Siku ya Kimataifa ya sala na tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu

Siku ya kamataifa ya sala na tafakari kuhusu biashara haramu.Kuna ukatili mkubwa na matokeo makubwa ya madhara ya kiafya kimwili na kisaikolojia kwa wale wanaoteseka na matokeo yanajitokeza kwa muda mfupi lakini pia yanaweza kujitokeza kwa muda mrefu,ikiwa hakuna hatua zinazochukuliwa.

Na Angella Rwezaula; - Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko mnamo mwaka 2015 alianzisha Siku ya Kimataifa ya sala na Tafakari kuhusu mapambano dhidi ya Biashara haramu ya binadamu ambayo huadhimisha kila mwaka ifikapo tarehe 8 Februari sambamba na Siku Kuu ya Mtakatifu Josephine Bakhita. Kwa mwaka huu 2023, siku hii unaongozwa na kauli mbiu: “Kutembea katika utu”. Baba Mtakatifu Francisko akiwa nchini Sudan Kusini kwenye Ziara yake ya Kitume aliyohitimisha tarehe 5 Februari 2023, kabla ya kuwaaga waamini na watu wenye mapenzi mema walioudhuria Misa Takatifu Dominika hiyo alisema: “Tumaini ni neno ambalo ningependa kuwaachia kila mmoja wenu, kama zawadi ya kushirikishwa, kama mbegu inayozaa matunda. Kama sura ya Mtakatifu Josephine Bakhita inavyotukumbusha matumaini, hasa hapa, iko katika ishara ya wanawake na ningependa kuwashukuru na kuwabariki wanawake wote wa nchi katika tukio hili  maalum".

Siku ya Tafakari kuhusu biashara haramu na utumwa mamboleo
Siku ya Tafakari kuhusu biashara haramu na utumwa mamboleo

Katika fursa ya siku hii, ndugu msomaji na msikilizaji wa Vatican News, tutafakari zaidi na kuelewa juu ya aina nyingi za utumwa ambazo zinaweza kujiwakilisha kila kona na mara nyingi zimesukana pamoja. Wale ambao wanauzwa wanakumbana na mateso makali mno ya vurugu katika maisha yao. Tunaweza pia kusema kwamba vurugu hizi na utumwa huo unajiwakilisha kwa kutumia mbinu nyingi ambazo awali ya yote ni woga, hofu ya matokeo kwa wale ambao wanateseka na ikiwa hawataweza kuthubutu kuasi na kujikomboa au hata bila kufanya jambo sahihi kwa mfano katika tabia ya kuzungumza au kukaa kimya. Wanaoteseka mara nyingi kama wasichana na wanawake wamekuwa wakifikiria kuwa ndio njia pekee ya kukubali kuacha bila kumsema anayesababisha mateso hayo kwa lengo la kumpatia fursa ya kubadilika.

Vurugu ya ndani ya mahusiano: Na kwa kuzungumzia aina hii ya vurugu za ndani ya mahusiano ya kihisia imeenea zaidi katika kila jamii na tamaduni, na ina mizizi yake katika usawa wa milenia wa haki na uwasilishaji wa wanawake katika jamii yenye mfumo dume. Kwa hiyo utakuta ukatili una matokeo makubwa ya madhara ya kiafya kimwili na kisaikolojia kwa wale wanaoteseka na matokeo ambayo yanajitokeza kwa muda mfupi, lakini pia yanaweza kujitokeza kwa  muda mrefu, ikiwa hakuna hatua zinazochukuliwa kwa yule anayeteseka. Na kwa upande wa wale wanaotumia jeuri, pamoja na kuwafanya wale walio karibu nao kuteseka na (kwa mfano katika visa vya jeuri ya familia, wafanyakazi kazini, wafanyakazi majumbani, hata katika mashirika, serikali na kidini) wanawapenda, na wanataka maisha ya kimahusiano yasiyoridhisha, kwa maana wanaopenda katika kesi ya (mke, watoto) na wanateseka kwa sababu ya tabia zao mbaya na kuziogopa, wakati huo huo hawataki kubadilika, kwa sababu ya jeuri walilo nalo.

Utumwa mambo leo
Utumwa mambo leo

Kwa anayetumia vurugu na jeuri, mara kadhaa anajionesha ndani ya nyumba au sehemu moja tu, lakini kwa nje au kwa jirani ni mkarimu kupindukia, akiuza sura na maneno matamu ambayo kamwe hayaweki katika matendo. Na ndiyo maana mara nyingi inapotokea jambo baya, (kwa mfano katika suala la mauaji dhidi ya wanawake) majirani hubaki kushangaa, imekuwaje mtu huyo, wakati kila wakati alionekana mwenye tabasamu, mpole, mcheshi na mkarimu? Kuna aina aina nyingi za ukatili wa kimwili au mali, ambazo zinajumuisha  matumizi ya hatua yoyote inayolenga kuumiza na/au kutisha. Hapo uchokozi unaweza kuwa dhahiri kwa mfano (kupiga teke, ngumi, kusukuma), maneno makali, lakini wakati mwingine kuna hila zaidi na ambazo zinaweza kulenga kitu ambacho mtu anajali (kwa mfano labda wanyama, vitu vyenye thamani au vitu ambavyo ni muhimu). Kwa hivyo ukatili huo hutofautiana kutokana na uchokozi katika familia).

Ukatili kimwili, unaohusisha majeraha unahitaji matibabu ya dharura, hadi kuwasiliana na kimwili ambapo ulenga kumtisha na kudhibiti mtu. Katika tafakari hii ya kuombea hasa waathrika wa  biashara ya Binadamu, inajikita kwa hakika katika sura nyingi sana kwa mfano unakutana na ukatili wa kisaikolojia ambao, nao una sura nyingi kama ile ukosefu wa heshima unaoudhi na kuharibu hadhi ya utu wa mwanadamu. Ni mara ngapi zinajidhihirisha katika familia, jamii na kazini?

Siku ya tafakari juu ya biashara haramu na utumwa mamboleo
Siku ya tafakari juu ya biashara haramu na utumwa mamboleo

Vurugu ya aina hii ya kisaikolojia inajidhihirisha sana, lakini daima iko katika aina nyingine zote za vurugu pia. Ndiyo ya kwanza kujidhihirisha yenyewe na ndiyo inayoruhusu maendeleo ya mitindo mingine ya ukatili. Ukatili wa kisaikolojia hauonekani sana kwa sababu, aina hiyo haiachi alama kwenye ngozi, sio tu kwa wageni, bali pia kwa wale wanaoteseka, kwa sababu mara nyingi huishia kuonekana kupitia macho ya wale wanaofanyiwa vurugu, na kama imekithiri inawezekana hata kuonekana nje. Unyanyasaji wa kisaikolojia inajionesha dhahiri kama vile vitisho, udhalilishaji hadharani au faraghani, kushushwa thamani mara kwa mara, ulaghai, udhibiti wa chaguzi za kibinafsi na mahusiano ya nje kijamii hadi kumshawishi mtu kuachana na marafiki na jamaa, na hatimaye kufikia  kutengwa kabisa na jamaa na marafiki.

Katika unyanyasaji wa kijinsia ninakumbuka wakati Baba Mtakatifu Francisko anakutana na wahanga huko Congo DRC ambao walitoa ushuhuda kama vile Bijoux, ambaye mnamo 2020 akiwa na umri wa miaka kumi na tano wakati anakwenda kuchota maji mtoni alitekwa nyara na kundi la waasi, na kubakwa kwa miezi 19 na kamanda wao. Alifanikiwa kutoroka akiwa mjamzito na sasa alikuwa pale mbele ya Mrithi wa Petro pamoja na watoto wake mapacha, lakini kila siku alikuwa ananyanyaswa kijinsia. Kama ile ya Emelda, ambaye aliishia kuwa mateka mikononi mwa waasi akiwa na umri wa miaka kumi na sita na kushikiliwa kama mtumwa wa ngono kwa miezi mitatu: wanaume watano hadi kumi walimnyanyasa kila siku. Kwa hiyo nyanyasaji wa kijinsia ni aina yoyote ya kushiriki katika shughuli za ngono bila idhini yoyote halisi, kitendo chochote cha ngono, au jaribio la tendo la ngono, maoni ya ngono yasiyotakika au ushawishi, au usafirishaji wa ngono, dhidi ya mtu kwa matumizi ya kulazimishwa.

Ni jinsi gani wahanga wanavyoteseka. Wakati vijana hao wanasimulia walifikia kusema kwamba hawakuwa na machozi kwa sababu hakuna yeyote ambaye angeweza kuleta msaada. Kwa hiyo kwa kulazimishwa tunamaanisha, pamoja na vitisho vya kimwili, au hali ambazo mtu huyo hawezi kutoa idhini kwa sababu chini ya ushawishi wa vitu, au kwa ulemavu wa kisaikolojia, au kwa sababu hawezi kuelewa hali hiyo, kama vile katika kesi ya unyanyasaji wa watoto wadogo. Ukatili huu unaweza kufanywa na mtu yeyote bila kujali uhusiano alionao na mwathirika, katika nyanja yoyote  ile ikiwemo ya familia na kazini.  Utambuzi wa unyanyasaji wa kijinsia ndani ya uhusiano wa wanandoa ni ngumu kwa sababu ya imani iliyokita mizizi juu ya majukumu ya ndoa na ikumbukwe kwamba, pamoja na maendeleo ya teknolojia, unyanyasaji wa kijinsia ndani ya uhusiano wa wanandoa unaweza kuchukua sura mpya (kwa mfano kueneza picha za kina za mwanamke na mpenzi wake katika mtandao).

Kuna aina nyingine za vurugu kijinsia na ambazo ni  utumwa mamboleo kama lile la ndoa ya kulazimishwa au kuishi pamoja, ikijumuisha ndoa za utotoni; kutumia vidhibiti mimba katika kujikinga na magonjwa ya zinaa, utoaji mimba wa kulazimishwa, ukeketaji au suala la kuthibitisha ubikira, ukahaba wa kulazimishwa au usafirishaji haramu wa binadamu. Kuna pia aina nyingine ya unyanyasaji ambao ni aina yoyote ya udhibiti wa uhuru wa kiuchumi. Hiyo ni vigumu kugundua na hata waathirika wenyewe hawajui.  Kwa sababu inajumuisha aina za udhibiti wa kiuchumi kama vile kuchukua au kuzuia upatikanaji wa pesa au rasilimali nyingine za kimsingi, kuhujumu kazi za wanawake, kuzuia fursa za elimu au makazi. Aina hiyo ya unyanyasaji inahusu kila kitu kinachochangia katika kuhakikisha kuwa mwanamke analazimishwa kuingia katika hali ya utegemezi na/au hana njia za kiuchumi za kukidhi mahitaji yake ya kujikimu na ya watoto wake. Mikakati hii inamnyima uwezekano wa kufanya maamuzi huru na kuwakilisha mojawapo ya vikwazo vikuu wakati mwanamke anahisi kuwa tayari kutoka katika hali ya unyanyasaji.

Siku ya Tafakari kuhusu biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo
Siku ya Tafakari kuhusu biashara haramu ya binadamu na utumwa mamboleo

Hii inatukumbusha tena wakati Papa akimshukuru Makamu mwakilishi maalum wa Umoja wa Mataifa, Bi Sara Beysolow Nyanti kwamba: “Wewe umesafiri nchi nzima, umewatazama akina mama machoni, ukishuhudia uchungu wanaoupata kwa hali ya watoto wao; Nilipigwa na butwaa uliposema kwamba, licha ya yote wanayoteseka, tabasamu na tumaini havijawahi kufifia kwenye nyuso zao. Na ninakubaliana na kile ulichosema kuwahusu: akina mama, wanawake ndio ufunguo wa kubadilisha nchi: ikiwa watapata fursa sahihi, kupitia bidii yao na uwezo wao wa kulinda maisha, watakuwa na uwezo wa kubadilisha sura ya Sudan Kusini, ili kuipa maendeleo tulivu na yenye mshikamano! Lakini, tafadhali, tafadhali wakazi wote wa nchi hizi: wanawake walindwe, waheshimiwe, na wanathaminiwe. Tafadhali walinde, heshimu, thamani na heshima kwa kila mwanamke, mtoto, kijana msichana, na mtu mzima, mama, bibi. Bila hiyo hakutakuwa na siku zijazo. (Hotuba ya Papa Francisko kwa wahamiaji wa ndani Sudan Kusini katika Ukumbu wa Uhuru, Juba 4 Februari 2023)

Ndugu msomaji kuna vurugu za kidini, ukosefu wa heshima kwa nyanja ya kidini au ya kiroho unatokea. Kama ilivyo kwa  wanandoa waliochanganyika na hutokea kila wakati katika nyanja ya kiroho kwa mtu anapodhurika kwa kutoruhusiwa kutekeleza mazoezi ya imani yake/zao za kidini au kwa kulazimisha yao wenyewe binafsi. Hatimaye kuna aina nyingine ya unyanyasaji wa kunyemelea ambapo ni aina ya kitendo chochote ambacho kinachodhuru uhuru na usalama wa mtu. Hii inaonesha aina za tabia za kudhibiti zinazotekelezwa na mtesaji kwa mwathirika. Ni aina ya vurugu ambayo imetambuliwa kwa miaka michache iliyopita hasa nchini Italia kwa ngazi ya udhibiti kisheria, lakini imekuwepo kwa siku nyingi katika mila na tamaduni nyingi. Inaweza kutokea wakati mwanamke anaamua kuvunja uhusiano na mwanamume au mme wake. Na mara nyingi hutangulia mauaji ya wanawake au majaribio ya wanawake. Inaweza kujidhihirisha kwa kutuma maua yasiyo na sababu na  kila siku zawadi, kuvizia nyumba akitembea nyuma kwa miguu au kwa vitisho vya simu au kupitia barua pepe, ujumbe mfupi wa maandishi uliotundikwa mbele ya nyumba za wanawake, mahali pa kazi au maeneo mengine ambayo kwa kawaida wanawake hao au wasichana hutembelea.

Siku ya kupinga biashara ya binadamu na madhara ya ukatili wa kila aina
08 February 2023, 15:47