2022.09.13 Ziara ya Papa nchini Kazakhstan 2022.09.13 Ziara ya Papa nchini Kazakhstan 

Khazakhstan,Askofu wa Almaty:ziara ya Papa ni kipindi muafaka kuimarisha wito wao

Askofu José Luis Mumbiela Sierra,wa Utatu Mtakatifu huko Almaty,mji wa Kazakhstan na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki,Asia ya Kati katika mkesha wa kufika Papa Francisko aliyeondoka Septemba 13 hadi 15 Septemba nchini Kazakhstan,amesema ziara yake ni kipindi cha kuzaa matunda ya kutafakari kwa kina wito wa kumfuasa Kristo.

Na Angella Rwezaula -Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko ameanza safari kuelekea nchini Kazakhstan kuanzia tarehe 13 -15 Septemba 2022, ikiwa ni ziara yake ya kitume ya XXXVIII ambapo kwa siku tatu huko Nur-Sultani katika moyo wa Asia atashiriki Kongamano la Wakuu wa kidini ulimwenguni na Dini za Jadi. Papa Francisko Dominika tarehe 11 Septemba wakati wa sala ya Malaika wa Bwana alikuwa amesema anakwenda kwa ajili ya kuzungumza katika ndugu wanaouhishwa na shauku moja ya amani. Katika mkesha wa kufika huko, Papa Francisko katika ziara ya kitume, naye  Askofu José Luis Mumbiela Sierra, wa Utatu Mtakatifu huko Almaty, mji wa Kazakhstan na Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki, Asia ya Kati amesema kuwa  Ziara ya Papa nchini Kazakhstan kwao wote ni habari kubwa, na ukweli wa Habari njema ambayo inawasidia kuelewa vizuri maana na utume wa uwepo wao nchini Kazakhstan  na thamani ya imani yao ulimwenguni. Askofu amesema wanamwomba Bwana ambaye kwa siku hizi maalum ziweze kuwa kwao kipindi cha kuzaa matunda  na ili waweze kutafakari kwa kina wito wao wa kumfuasa Yesu Kristo, Mfalme wa amani.

Papa Kazakhistan
Papa Kazakhistan

Askofu José Luis Mumbiela Sierra, ambaye ni mhispania alibainisha kuwa kauli mbiu ya ziara yake: “Mjumbe wa amani ya Umoja, sio kuelekeza wito wa wakristo nchini Kazakhstan, tu bali  inaleza hata maana ya uwepo wa Papa, ambaye anafika kushiriki Kongaano la viongozi wa kidini katika mji huo wa Astana ambao hufanyika kila baada ya miaka miwili. Ziara ya Kitume ya Papa Francisko ina maana ya ulimwengu. Muktadha ambao ulimwengu wa sasa unajikutana nao, kati ya janga la Uviko-19, vita na wasi wasi mkubwa kutokana na mwendelezo wa migogoro ya kidunia. Mambo hayo kiukweli yanafanya kutambua kuwa ziara hiyo sio tu ya kichungaji kwa ajili ya jumuiya ndogo ya waamini, badala yake uwepo wa Papa katika Kongamano  pia si kueneza thamani ya juu ya mkutano huo, bali inatoa fursa kubwa na mkondo wa kuweza kuzungumza kwa ulimwengu mzima.

Papa Kazakhistan
Papa Kazakhistan

Askofu ameendelea kueleza kuwa ikiwa kwa upande mmoja ziara ithamanisha matendo, serikali ya Kazakhistan ya kujenga vifungo na maelewano kati ya makabila na dini tofauti, kwa upande mwingine inaonesha ubinadamu ambao kila dini ambayo inagusa uhusiano wa mtu na Mungu ni wa kina kama sababu ya kuweza kuunda amani na umoja kwa ubinadamu wote. Dini hazijawahi kamwe kuwa sababu za migogoro, bali kila dini inaalikwa kuhamasisha udugu ambao Papa mara nyingi anausisitiza na kutegemea mabadiliko ya mfuundo wa kiakili wa migogoro iliyoko katika ulimwengu wa leo hii. Kwa upande wa Askofu Mumbiela Sierra amesema kufika kwa Baba Mtakatifu nchini Kazakhstan ni kipindi muafaka si tu kwa nchi ya Kazakhstan, bali hata kuzindua kwa kupitia Kazakhstan, ujumbe kwa ulimwengu mzima na ubinadamu wote.

Papa Kazakhistan
Papa Kazakhistan

Kwa kutazama mantiki mahalia, Askofu amesema wao ni jumuiya ndogo ambayo inaishi imani kila siku kwa neema ya Mungu. Ikiwa kuwa wajumbe wa amani na umoja ni wito wa kila mkatoliki na kila mkristo, ina maana kutoka Kazakhstan leo hii unaamshwa juu  ujumbe kwa ubinadamu wote, kwamba wote wameitwa na ni wachukuzi wa amani, ili kuuishi na kuiunda kati ya watu na katika jamii. Kuwa na Papa kati yao amesema anawakilisha pongezi kubwa katika kugundua furaha ya wito wao, lakini pia hata msukumo wa dunia nzima ambayo inaanzia hapo katika jumuiya yao ndogo. Kwa kuhitimisha Askofu alisema kwa kuwa kinjili inawezekana kukumbusha picha au mfano wa chumvi ambayo licha ya kuweka chembe kidogo, kwenye vyakula vinakuwa na ladha.

Chumvi ni ishara ya kihifadhi vyakula visiharibishwa, kwa maana hiyo wakristo wote wanaalikwa kuwa kama chumvi ambayo inatoa ladha na hata kwa sababu jamii isiweze kuharibika. Kuwa chumvi maana yake ni kuunda amani na udugu  hata kama wao ni wachache au wasioonekana katika macho ya ulimwengu; ina maana ya kuishi wito wake katika kushuhudia na kutoa amani ambayo inakuja kutoka kwa Yesu Kristo, Mfalme wa Amani, kwa watu wote, hata kama ni tofauti kwa ajili ya dini, mawazo, utamaduni na makabila. Kanisa Katoliki nchini Kazakhstan hadi leo hii wanahesabu majimbi 4 na maparokia 70 na waamini 120,000 tu ambao wanapeleka mbele utume hata kwa kufanya kazi katika nyanja ya kijamii, kiutamaduni na kielimu.

Papa kazakhistan
13 Septemba 2022, 11:49