Caritas Yerusalemu kutoa msaada kwa wakina mama na watoto. Caritas Yerusalemu kutoa msaada kwa wakina mama na watoto. 

Caritas Yerusalemu yatoa msaada kwa akina mama na watoto wachanga huko Gaza

Caritas Yerusalemu imetoa msaada wa mikebe 10,000 ya maziwa kwa watoto walio katika mazingira magumu kama kitengo cha Caritas huku wakiwasaidia wote kufuatiwa kuweka sahihi kwa usitishaji wa vita na kwa kujali masilahi ya kibinadamu.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Caritas Yerusalem imetoa zaidi ya mikebe 10,000 ya maziwa ya watoto wachanga huko Gaza siku chache baada ya kuweka sahihi kwa usitishaji wa vita katika Ukanda wa Gaza. Mpango huo unaashiria moja ya hatua kubwa za kwanza za kibinadamu tangu kusitishwa kwa mapigano kutangazwa, na kuwapa nafuu familia zilizokuwa hatarini na zilizoharibiwa kwa miezi kadhaa ya migogoro,kwa mujubu wa taarifa iliyochapishwa tarehe 14 Oktoba 2025 na Caritas Yerusalemu.

Utoaji wa misaada

Utoaji huo wa misaada uliofanywa kupitia vituo vya matibabu vya Caritas katika Ukanda wa Gaza, uliwapa nafasi ya kwanza watoto wachanga na watoto wadogo ambao walikosa lishe wakati wa vita. Kitengo cha matibabu ya Caritas kinachotoa huduma katika maeneo tofauti, kilisambaza maziwa kwa lengo la kuwafikia watoto na mama wanaopata matatizo ya kulisha watoto wao. Katibu Mkuu wa Caritas Yerusalem, Anton Asfar, alisisitiza dhamira ya shirika la kudumisha utu wa kibinadamu na kulinda walio hatarini zaidi, akisema kuwa "tangu siku ya kwanza baada ya vita, tumekuwa tukifanya kazi bila kuchoka kusaidia watu wa Gaza, hasa wale walio dhaifu zaidi, watoto, akina mama na wazee. Na sio tu kuwapa watoto maziwa, bali pia kuwapa tumaini katika maisha.

Nuru ya matumaini

Kutokana na vita hivyo vilivyodumu kwa miaka miwili, familia nyingi zilikuwa zimeachwa kwa miezi kadhaa bila kupata maji safi, matibabu, au lishe bora kwa watoto wao. Katikati ya changamoto hizi kubwa, Caritas Yerusalem imejitolea kuwa karibu na watu, sio tu kuwapa riziki katika maisha bali pia kuwapa tumaini kwenye jumuiya wanapoanza safari kurejea hali ya kawaida. Katika Kusini mwa Gaza, Caritas Yerusalem inatoa huduma ya Afya Msingi, kama vile: msaada wa kisaikolojia na misaada ya dharura kwa familia zilizohamishwa na zilizoathirika. Inafanya kazi kwa utaratibu wa karibu na idara ya afya mahalia na Mashirika ya Kanisa ili kuhakikisha misaada ya kibinadamu inatolewa kwa usalama.

15 Oktoba 2025, 14:40