Colombia,Barrio San Bernardo:Kazi ya Kanisa ni kuleta matumaini kwa wakazi
Na Christine Masivo CPS, - Vatican.
Padre Juan Felipe Quevedo miezi michache iliyopita aliungana na Padre Carlos Olivero, anayejulikana kama Padre Charly katika Parokia ya "Nuestra Señora de los Dolores," yaani Mama Yetu wa Uchungu, aliyetumwa kutumikia sehemu ya Bogotá katika makao makuu ya Baraza la Maaskofu wa Amerika Kusini (CELAM) na kuendeleza mipango ya kusaidia watu waliotelekezwa wa Amerika kusini yote. Kwa mujibu wa Shirika la Kipapa la Habari za Kimisionari(Fides), limebainisha kuwa Padre Charly anatumia njia ya kujikita katika mbinu ya jamii ya mtandao wa Familia kubwa ya Kristo(Familia Grande hogar de Cristo), ambayo ilianzia Nchini Argentina kupitia kazi ya Mapadre ambao waliishi na kutumikia katika vitongoji duni vya Buenos Aires waliojulikana kama(Curas Villeros). Kwa miaka mingi, ‘San Bernardo’ imekuwa mojawapo ya kitovu cha madawa ya kulevya, mitaa imejaa watu wanaopambana na kuvuta bangi, wasio na makazi, na waliosahaulika, wale wasio na huduma za afya, hati, na bila tumaini.
Mwanzo wa uharibifu
Mabadiliko hayo yaliongezeka wakati wakazi wa kitongoji kingine maskini walipofukuzwa kwa nguvu ili kufanya maendeleo ya mahali hapo. Familia nyingi zilizohamishwa ziliishia San Bernardo, na hivyo kukawa na uhitaji mkubwa. "Katika nusu ya pili ya karne ya 20, Bogotá ilipitia mabadiliko makubwa ya idadi ya watu ambayo ilibadilisha muundo wa jiji," aliekezea Padre Juan felipe. "Matokeo yalikuwa vitongoji kama ‘San Bernardo,’ vilivyojaa matatizo magumu ya kijamii."Katika uwanja wa Parokia, kelele zinasikika zikitangaza kuwasili kwa dawa mpya za kulevya kwa ajili ya kuuza au kuonya kuhusu doria za polisi, kila kona utawaona wanaume na wanawake wasio na makazi, miili yao iliyowekwa alama na maisha ya barabarani na ulevi.”
Hatari kwa Usalama
Padre felipe alielezea: "Idadi ya watu wasio na makazi inaongezaka kwa haraka katika eneo letu, mizozo ya kijamii imezidi na kubadilisha maisha ya kila siku katika hiki kitongoji, ikiongeza idadi kubwa ya walioacha shule, wizi, na ujumuishaji wa vikundi vya wahalifu.” Padre anaeleza kuongezeka kwa migogoro, "wakazi wa kiutamaduni hawaoni tena wasio na makazi kama sehemu ya jamii lakini kama tishio. Takataka hulimbikiza, uhalifu kuongezeka na watu hupoteza tumaini. Jina Lenyewe 'Sanber' limekuwa sawa na kutengwa na vurugu.” Padre Charly, ambaye alitumia miaka mingi akihudumu katika Vijiji vya umasikini "Villas Miseria" vya Argentina, alisema kuwa yale aliyoona hapo yanazidi hata mambo aliyojionea hapo awali: "uchunguzi mmoja unazungumzia watu 5,000 wasio na makao mahali hapa, kiwango hicho ni kikubwa sana. Unahisi kutokuwa na msaada, kana kwamba hakuna mtu anayeamini suluhisho linawezekana.”
Matumaini katika kukata tamaa, hatua ya awali
Walakini, katikati ya kukata tamaa, mapadre na waamini hutenda kwa udogo wao kwa ishara zenye nguvu. Wanapogawa chakula, watu hukimbilia kwao, wakitamani kula. "Inavunja moyo, lakini hapa ndipo tunapaswa tuanzie kwa kuwapa chakula. Wakati huo huo, lazima tusaidie jamii kuona kwamba wale wanaoishi mitaani ni kaka na dada zetu. Inaweza kutokea kwa yeyote kati yetu. Kazi yetu sio kuchukua nafasi ya serikali, lakini ni kujenga madaraja.” Kwa Padre Felipe anasisitiza kuwa msingi wa utume huu ni tumaini la Kikristo. "Matumaini sio kutoroka kutoka katika ukweli lakini ni nguvu ya mabadiliko. Tunakutana na uso wa Kristo katika hiki kitongoji chetu, na hawaoni aibu kutukaribia. Parokia yetu lazima iwe mahali panapokaribisha, ambapo uvumilivu na upendo huambatana na safari ya kila mtu. Hakuna shimo lililo ndani zaidi ya rehema.”
Matumaini ya siku zijazo
Maono haya yanachukua sura katika nafasi mpya ya jamii: sio tu makazi au huduma, lakini mahali pa kukutana. Walio wanyonge zaidi wanaweza kukoga, kupokea huduma ya matibabu, kula, na, ikiwa watachagua, na wakipenda kuanza kufikiria maisha zaidi ya kutumia madawa ya kulevya. Wakaazi kukutana kama majirani na si wageni. Jamii inapofungua milango yake kwa wale wanaoteseka zaidi," Asema Baba Charly. Inamgundua Yesu kwa njia mpya na kupokea baraka zake.” Huko San Bernardo, kati ya watu waliovunjika moyo, mambo mapya yanaanza kuleta matumaini.”
Asante kwa kusoma makala hii. Ikiwa unataka kusasishwa,jiandikishe ili kupata habari za kila siku hapa: Just click here