Seminari Kuu ya Mashahidi wa Uganda yafanya warsha ya malezi kuhusu Sinodi
Na Caroline Kavita – Gulu, Uganda.
Warsha ya Sinodi iliwaleta pamoja walimu wa seminari-mapadre, watawa wa kike na kiume, wafanyakazi wa kawaida, wanaume na wanawake ili kuongeza uelewa wao wa Sinodi kama njia ya maisha katika Kanisa lenye mizizi katika ushirika, ushiriki, na utume, ni kwa mjibu wa taarifa zilizochapishwa katika Shirika la habari Za Kanisa la CISA -Afrika.
Kanisa la Afrika linalotekeleza Sinodi
Warsha hii ni sehemu ya mpango unaoendelea wa ASI wa bara unaolenga kuimarisha malezi ya kichungaji katika seminari kuu za kitaifa. Tangu 2023, warsha kama hizo zimefanyika Rwanda, Ivory Coast, Afrika Kusini, Nigeria, na Namibia, zikiwashirikisha Maaskofu, mapadre, watawa, na mamia ya waseminari. Mpango huu unalenga kusaidia Makanisa ya Kiafrika katika kutekeleza matokeo ya Sinodi kuhusu Sinodi (2021–2024) huku Kanisa likielekea kwenye Mkutano Mkuu wa Kanisa wa 2028.
Warsha hiyo iliendeshwa na timu kutoka Mpango wa Sinodi za Kiafrika (ASI), kila moja ikileta uzoefu wa kina katika malezi ya Kitaalimunguuongozi wa kichungaji, na hali ya kiroho na utendaji wa sinodi. Padre Agbonkhianmeghe E. Orobator, SJ, Mkuu Chuo cha Kijesuiti cha Taalimungu, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Clara na mjumbe katika Sinodi kuhusu Sinodi, alitoa ufahamu kuhusu maana na mchakato wa sinodi katika Kanisa leo hii.
Kusikiliza ishara za nyakati
Padre Marcel Uwineza, SJ, Rais wa Chuo Kikuu cha Hekima (HUC) na Mkurugenzi Mshirika wa ASI, aliwaongoza washiriki kuhusu kuunganisha maadili ya sinodi katika malezi na uongozi wa kikuhani. Sr. Anne Arabome, SSS, mtaalimungu, mkurugenzi wa kiroho, na mwanzilishi wa Taasisi ya Sophia ya Masomo ya Taalimungu na Uundaji wa Kiroho, aliongoza kikao hicho kuhusu misingi ya kiroho ya sinodi na jukumu muhimu la wanawake katika maisha ya kikanisa.
Bi. Ndanu Mung’ala, mtaalamu wa usindikizaji wa kichungaji, ushiriki wa vijana na mwenye uzoefu mkubwa katika ujenzi wa amani, jinsia, na mshikamano wa kijamii, aliongoza tafakari kuhusu kusikiliza ishara za nyakati na kukuza ushiriki jumuishi huku Bi. Caroline Kavita, Mratibu wa Programu wa ASI na mtaalamu stadi katika uwezeshaji wa kikundi, akihuisha vipindi kuhusu Mazungumzo katika Roho, na kuwawezesha washiriki kupata uzoefu wa sinodi kama uzoefu wa kijamii.
Kuelekea Mkutano wa Kikanisa wa 2028
Warsha hiyo ilitumia mbinu shirikishi na ya uzoefu iliyojikita katika Mazungumzo katika Roho kama ilivyowezeshwa na Padre Orobator. Vipindi vilijumuisha mawasilisho, sala ya faragha, mazungumzo katika vikundi vidogo, kushiriki kwa pamoja, kutafakari kwa mwongozo, na ukimya wa kutafakari ili kukuza usikilizaji wa kina na utambuzi wa kijamii. Matukio ya kesi na mazoezi ya vikundi yaliyopangwa yaliwaruhusu washiriki kufanya mazoezi ya ujuzi wa uongozi wa sinodi katika miktadha halisi ya kichungaji, kuhakikisha sio tu uelewa wa kinadharia bali pia uzoefu wa kuishi wa kusafiri, kupambanua, na kuamua pamoja kama jumuiya. Kanisa barani Afrika linapojiandaa kwa Mkutano wa Kanisa wa 2028, mbegu zilizopandwa kupitia programu hizi za malezi zitaendelea kuwaunda viongozi wanaohudumu kwa unyenyekevu na kukuza ushirikiano katika utume wa pamoja wa Kanisa.