Tanzania,Pad.Kitima:vifo vingi katika maandamano.Jitihada ya Kanisa katika mazungumzo
Na Federico Piana - Vatican.
"Ndiyo, kuna mamia ya vifo. Ni unyama kweli." Kile ambacho hakuna mtu aliyewahi kutaka kusikia sasa kimethibitishwa: Katika maandamano ya barabarani ambayo yameitikisa Tanzania katika siku za hivi karibuni na mapigano kati ya polisi na waandamanaji wanaopinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa hivi karibuni, waathiriwa hawakuwa wachache tu, kama baadhi ya waangalizi wa kimataifa walivyokadiria kwamba ni watu wengi. Kulikuwa na mengine mengi. Mauaji ya halaiki.
Mawasiliano ya Sehemu
Padre Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), alifanikiwa kuwasiliana na vyombo vya habari vya Vatican kama vile, asubuhi ya tarehe 4 Novemba, wakati mamlaka ilivyorejesha kwa kiasi fulani miunganisho ya simu na kuanzisha tena mtandao wa mara kwa mara, kwa pendekezo la kushtua, na la kutisha, kwa idadi ya watu wote ikisema kuwa: “epuka kushiriki na kusambaza, hasa kwenye mitandao ya kijamii, picha ambazo zinaweza kusababisha wasiwasi na "kukera maisha ya binadamu."
Upinzani Walaani
Baadhi waliona onyo hili kama jaribio la kuzuia kashfa ya upinzani, ambapo wanashutumu vikosi vya usalama kwa kutupa kwa siri miili ya mamia ya watu waliouawa wakati wa maandamano katika maeneo yasiyotajwa. Mirundiko ya miili ambayo mtu anaweza kuwa ameipiga picha na huenda, mapema au baadaye, itasambasambazwa au kwa kiasi fulani imekwisha sambazwa.
Makosa na Utekaji nyara
"Maandamano ya barabarani ambayo yameikumba nchi nzima yalianza kwa sababu ya makosa kadhaa yaliyogunduliwa wakati wa uchaguzi. Lakini pia kuongeza uelewa wa ukiukwaji wa kimfumo wa haki za msingi za binadamu kupitia utekaji nyara na mauaji ya wanasiasa na wale waliopinga serikali," alisema Padre Kitima. Hakanushi kwamba waandamanaji, katika baadhi ya matukio, wamejihusisha na unyanyasaji, uharibifu, na uporaji: "Lakini polisi walijibu kwa kuwafyatulia risasi watu kwa risasi za moto, kuwajeruhi na kuwaua.”
Kanisa lililohamasisha
Kwa hakika Kanisa mahalia hapo awali halikuketi tu. Tangu mwanzo kabisa, lilipogundua kuhusu makosa ya uchaguzi, liliandaa mikutano na maafisa wa serikali ili kudai kura ya haki, huru, na ya kuaminika. "Maaskofu pia waliitisha maombi ya kitaifa na kulaani kutoweka, utekaji nyara, na kukamatwa kwa wanasiasa na wawakilishi wengine wa vyama vya upinzani. Baraza la Maaskofu hata waliandika barua za wazi kulaani matukio haya na kuiambia serikali kwamba lazima ikae kwenye meza ya mazungumzo na kushiriki katika mazungumzo na vyama vya siasa vya upinzani."
Wito wa kuwa na Mazungumzo
Sasa kwa kuwa matukio yameongezeka, Maaskofu wameitisha mkutano wa haraka wa Kanisa kwa Juma lijalo ili kuunda mkakati wa kuchukua hatua madhubuti na za kuleta amani. Rais Samia Suluhu Hassan pia alizungumzia mazungumzo Novemba 3 wakati wa sherehe ya kuapishwa kwa muhula wake wa pili, ambayo ilifanyika licha ya mvutano katika mji mkuu uliofungwa. Padre Kitima bado ana shaka: "Bado tunasubiri mazungumzo. Tunaomba serikali iwasikilize watu kwa dhati, huku tukiwaambia watu wetu kwamba haki inahitaji kujadili ukweli: Kuna matatizo ambayo yanahitaji kutatuliwa, na wale walioyasababisha lazima wawajibike. Kanisa linatafuta njia ya kupona."
Vijana wako Mstari wa Mbele
Kama ilivyotokea katika mataifa mengine ya Afrika, kuna baadhi ya walio mstari wa mbele na muhimu nyuma ya maandamano yote nchini Tanzania hasa: vijana. Ni wao, alihakikishia Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu, wanaotaka mabadiliko, wanaodai ushiriki mkubwa na thabiti zaidi kutoka katika siasa, ambao wangependa kura yao ihesabiwe kweli, kama Katiba inavyotaka: "Hata hivyo, tatizo ni kwamba uchaguzi huru, wa haki, na unaoaminika ni tatizo kubwa hapa. Wako sahihi. Na Kanisa letu linajaribu kuwasaidia kwa kuwapa programu maalum ya elimu ya uraia na elimu ya haki za binadamu kwa ajili ya uelewa wa kisiasa, inayoweza kutoa maarifa na ujuzi unaohitajika kutekeleza haki zao za kisiasa." Hii ndiyo sababu vijana hawana shida wakibishana kwa sauti kwamba "taasisi pekee inayoweza kuwatetea ni Kanisa Katoliki."
Asante kwa kusoma makala haya. Ikiwa unataka kuendelea kupata taarifa mpya, tunakualika ujiandikishe kwa jarida letu:cliccando qui.