Mkutano kuhusu Tabia Nchi COP30 huko Belem nchini Brazil Mkutano kuhusu Tabia Nchi COP30 huko Belem nchini Brazil  (AFP or licensors)

USCCB na CRS Waomba Viongozi wa Dunia Kushughulikia Mabadiliko ya Tabianchi katika COP30

"Kama sisi sote tunavyoathiriwa,vivyo hivyo sote tunapaswa kuwajibika kushughulikia changamoto hii ya kimataifa."Hayo yamesema na wenyeviti wa maaskofu wanaoongoza kamati za Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani (USCCB) kwa sera ya tabianchi,wakiungana na rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Usaidizi wa Kikatoliki(CRS)kutoa wito wa hatua za haraka na za ujasiri ili kulinda kazi ya uumbaji wa Mungu na watu wake,katika kuelekea COP30.

Na Christine Masivo, CPS. - Vatican.

Viongozi wa Ulimwengu wakiwa wanakaribia kufanya mkutano wao wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabianchi (COP30), Novemba 2025 huko Belem nchini Brazil,  Wenyeviti wa Kamati  za  Mabaraza ya Maaskofu Katoliki nchini Marekani (USCCB) zinazoshughulikia sera ya tabianchi, waliungana na rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Usaidizi wa Kikatoliki (CRS), kutoa wito wa hatua za haraka na za ujasiri ili kulinda kazi ya uumbaji  wa Mungu na watu wake.

Kwa njia hiyo, Mkutano wa 30 kuhusu Mazingira (COP30) mwaka huu unafanyika huku Kanisa Katoliki likisherehekea Mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya  Matumaini 2025. Papa Leo XIV aliwataka washiriki wa Mkutano huo wa COP30 ‘kusikiliza kilio cha ulimwengu, maskini, familia, watu wa kiasili, wahamiaji wasio na mahali ulimwenguni kote. Katika Mwaka huu wa Jubilei ni fursa takatifu ya kurejesha uhusiano na kufufua kazi ya uumbaji wakati ambapo zawadi ya uhai iko chini ya tishio kubwa. Mabadiliko ya tabianchi upotevu wa Bayoanuawai na uharibifu wa mazingira,  ni jumuiya  zenye uharibifu ambazo tayari zimelemewa na umaskini na kutengwa. Familia za kilimo na uvuvi zinakabiliwa na vitisho kwa riziki zao, wenyeji wanakabiliwa na uharibifu wa ardhi za mababu zao; afya ya watoto, usalama, na mustakabali wao uko hatarini. Kushindwa kusimamia uumbaji wa Mungu, kunapuuza jukumu letu kama familia moja ya kibinadamu.

Laudato si'

“Muongo mmoja uliopita, katika Waraka wa Laudato si’, Papa Francisko  alitukumbusha kwamba hali ta Tabianchi  ni faida ya pamoja, ni ya wote na imekusudiwa kwa wote, na kwamba mshikamano wa vizazi mbalimbali si wa hiari. Tunawaomba viongozi wa dunia kuchukua hatua za haraka na kwa ujasiri kwa ajili ya utekelezaji wa Mkataba wa Paris wenye malengo makubwa unaolinda uumbaji na watu wa Mungu. Kama vile sisi sote tunavyoathiriwa, vivyo hivyo sote tunapaswa kuwajibika kushughulikia changamoto hii ya kimataifa.

“Katika Mkutano huo wa 30 kuhusu utunzaji wa Mazingira au COP30, nchi, pamoja na mashirika ya kiraia, zinapaswa kujitolea tena kutekeleza kuwekeza katika juhudi za kukabiliana na hali ili kuwezesha ustahimilivu na kukuza fursa za kiuchumi, kujitolea kwa juhudi za kupunguza uzalishaji wa joto la hali ya hewa, kusitisha hasara na ufadhili wa uharibifu unaohakikisha kipaumbele na ufikiaji wa moja kwa moja kwa jamii zilizoathiriwa na mazingira magumu, kuhakikisha mpito wa haki hadi uchumi endelevu unaozingatia wafanyakazi, jamii na uumbaji, na kutoa ufadhili kwa ajili ya suluhisho za hali ya hewa, ikiwa ni pamoja na unafuu wa madeni, kwa wakati unaofaa na kwa uwazi huku wakati huo huo tukidumisha utu wa binadamu. Kwa pamoja, vitendo hivi vinaweza kufanya kazi kuelekea ekolojia jumuishi na ‘kuwapa kipaumbele maskini na waliotengwa katika mchakato huo.’ “Tunaomba usaidizi na mshikamano na kuahidi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kulinda mustakabali wa nyumba yetu ya pamoja,”

"Kama sisi sote tunavyoathiriwa,vivyo hivyo sote tunapaswa kuwajibika kushughulikia changamoto hii ya kimataifa."Hayo yamesema na wenyeviti wa maaskofu wanaoongoza kamati za Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Marekani (USCCB) kwa sera ya tabianchi,wakiungana na rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Usaidizi wa Kikatoliki(CRS) kutoa wito wa hatua za haraka na za ujasiri ili kulinda kazi ya uumbaji wa Mungu na watu wake,katika kuelekea Mkutano wa COP30.

COP30 Brazil

 

06 Novemba 2025, 17:35