Maaskofu wa Marekani Maaskofu wa Marekani   (AFP or licensors)

Askofu Mkuu wa Baltimore atoa wito wa kupyaishwa sera za kisiasa za Marekani

Kabla ya maadhimisho ya miaka 250 ya Uhuru nchini Marekani, itakayoadhimishwa Julai 4,2026,Askofu Mkuu William Lori wa Baltimore aliandika barua ya kichungaji huku akiwaalika Wamarekani wote kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa taifa lao huku wakifanya upyaishwaji wa sera za kisiasa.

Na Jenny Kraska – Baltimore

Katika kuelekea maadhimisho ya  makubwa  ya kihistoria ya miaka 250 ya Azimi la Uhuru nchini Marekani, itakayoadhimishwa tarehe 4 Julai 2026, inahitaji mang’amuzi. Shukrani kwa baraka za taifa lazima zifanyike pamoja na utambuzi wa kweli wa migawanyiko inayounda maisha ya kiraia sio tu Amerika, bali katika demokrasia  ulimwenguni kote. Haya yanaonekana katika barua ya kichungaj yenye kichwa: Upendo na Ukweli: Kuelekea mfumo mpyaisho wa utamaduni wa sera za kisiasa, iliyoandikwa na Askofu Mkuu Williamo Lori, wa Jimbo Kuu la Baltimore nchini Marekani, akiandika  kwamba mgogoro wa kisiasa wa leo hii  si wa kitaasisi tu ni wa kimaadili na kiroho. Ingawa sheria na miundo ni muhimu, haviwezi kuchukua nafasi ya wema. Unaanza na kurudi kwa Yesu Kristo. Askofu Mkuu alisisitiza kwamba maisha halisi ya kisiasa yanategemea kurejesha maono wazi ya mwanadamu, aliyeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu, aliyepewa hadhi isiyoweza kuvunjika, na kuitwa kuwajibika kwa wengine.

Sinodi zaidi ya miundo ya Kanisa

Mada ya barua ya kichungaji ya Askofu Mkuu ni Sinodi. Kwa njia hiyo ingawa mara nyingi hujadiliwa kwa maneno ya kikanisa, Askofu Mkuu anapendekeza roho yake ina mafunzo kwa ajili ya  maisha ya umma pia. Kiini chake, Sinodi ni kuhusu kusikiliza kwa unyenyekevu, kuzungumza kwa uaminifu, kutambua kwa uvumilivu, na kutembea pamoja badala ya kujitenga katika vikundi, jambo amalo halikubaliki. Na kikinachokataliwa ni kugawanyika. Maisha ya ndani ya Kanisa hayawezi kuunganishwa tu na sera za kisiasa za kidunia. Hata hivyo tabia ambazo sinodi huendeleza ni usikivu, uvumilivu, uzito wa maadili, heshima kwa utu ni muhimu kwa jamii yoyote inayotarajia kuvumilia wingi bila kujitenga.

Kurejesha mawazo ya maadili

Katika Kiini cha barua hiyo kwa ajili ya wito wa kurejesha kile kinachoweza kuitwa mawazo ya maadili katika  maisha ya kisiasa, Askofu Mkuu anabainisha kuwa hii si ujinga. Wala si kujitenga na imani. Mawazo ya kimaadili ni uwezo unaoundwa na wema, wa kufikiria maisha ya umma ambapo ujasiri hauwi uchokozi, haki haihitaji udhalilishaji, na ukweli hautenganishwi na upendo.

Upyaishaji kutoka miongoni mwetu

Utamaduni wa kisiasa huundwa na tabia za maadili za watu wa kawaida. Taasisi ni muhimu, lakini haziwezi kufidia upungufu wa wema. Mabadiliko yanayohitajika hayawezi kulazimishwa; lazima yapandishwe kupitia dhamiri, mshikamano, na kujitolea upya kwa kutembea pamoja licha ya kutokubaliana. Katika enzi inayojaribiwa na kujiondoa upande mmoja na utawala upande mwingine, kwa Upendo na Ukweli: Kuelekea mfumo mpya isho wa utamaduni wa sera za kisiasa,inapendekeza njia nyingine: siasa inayoongozwa na wema, inayoendelezwa na mawazo ya kimaadili, na iliyojengwa katika imani kwamba upendo na ukweli ni pamoja. Katika  uwanja wa umma uliochoka, hilo linaweza kuwa pendekezo kubwa zaidi kuliko yote.

Kwa kifupi Azimio la Uhuru la Marekani ni hati ya kihistoria iliyoidhinishwa na Kongamano la pili la Bara la Amerika mnamo tarehe 4 Julai  1776, ambalo lilitangaza uamuzi wa makoloni kumi na tatu ya Marekani kujitenga na Uingereza. Ilikuwa ni hatua ya kutangaza rasmi kutengana kwa makoloni na utawala wa Uingereza na kuweka msingi wa kuanzishwa kwa Nchi za Umoja wa Marekani. Kwa nia hiyo tangazo hili linasherehekewa kama alama ya uhuru, demokrasia, na haki za binadamu, na misingi yake imeathiri harakati za uhuru na haki za raia Ulimwenguni kote.

Askifu Bartimore

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

17 Februari 2026, 13:42