Maaskofu wa Kenya. Maaskofu wa Kenya. 

Kenya:Wasiwasi wa Maaskofu kuhusu kuongezeka kwa vurugu ambazo hazikubaliki!

"Kwaresima ni kipindi kitakatifu ambapo tunatafakari,kuomba,kufunga,kutubu na kutoa sadaka kwa ajili ya kuwasaidia maskini na walio katika mazingira magumu katika jamii yetu.Ni fursa ya kuwaalika Wakenya kuchunguza wajibu wao binafsi na pamoja katika kujenga jamii yenye haki;kukataa ufisadi,vurugu na kutojali.Matumizi ya nguvu dhidi ya raia wasio na silaha,wakiwemo wanawake,watoto na wazee,hayakubaliki na tunalaani bila vitendo hivyo vya kikatili."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Maaskofu Katoliki nchini Kenya katika ujumbe wao wa Kichungaji wa Kwaresima 2026 kati ya mambo mengi waliyosema, walirejea juu ya  tukio lililotokea Dominika ya tarehe 25 Januari 22026, katika Kanisa la Kianglikan (ACK) huko Othaya, Kaunti ya Nyeri, Kenya. Maafisa wa polisi waliokuwa wamevaa nguo za kiraia walifyatua gesi ya kutoa machozi wakati wa waamini wamekaa kwenye ibada. Kuhusiana na tukio hilo Baraza la Maaskofu nchini Kenya wanaonesha wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa vurugu ambapo walitoa wito wa kufanya "uchunguzi kuhusu shambulio dhidi ya Kanisa hilo la  Kianglikani." Kwa mujibu  barua hiyo ya kichungaji,  Maaskofu wanabainisha kwamba: “Makanisa ni mahali patakatifu na lazima yaheshimiwe kila wakati. Kuwafyatulia waamini gesi ya machozi ndani ya makanisa ni ukiukwaji mkubwa wa haki ya kikatiba ya kuabudu, iliyoainishwa katika Kifungu cha 32 cha Katiba ya Kenya."

Waamini na watoto walipata madhara ya kuwashwa macho na njia za upuaji

Waamini mia kadhaa, wakiwemo watoto na wachanga, walipata dalili za kukosa hewa na kuwashwa macho na njia zao za upumuaji. Shambulio hilo lilimlenga Makamu wa Rais wa zamani Rigathi Gachagua, ambaye alikuwa akihudhuria ibada hiyo pamoja na baadhi ya wasaidizi wake na wafuasi wake. Wakati wa shambulio hilo, magari kadhaa ya Gachagua na wafuasi wake yalichomwa moto na kuharibiwa. Kulingana na mashahidi, washambuliaji hao pia walifyatua risasi za bunduki aina ya AK-47 hewani, na kuongeza hofu na mkanganyiko zaidi kwa waamini. Maaskofu Katoliki wanatoa wito wa "uchunguzi wa kina na mashtaka dhidi ya wale wote wanaohusika katika vitendo vya vurugu za kisiasa, wakiwemo wachochezi wao. Matumizi ya nguvu dhidi ya raia wasio na silaha, wakiwemo wanawake, watoto, na wazee, hayakubaliki, na tunalaani bila shaka vitendo hivyo vya kikatili."

'Tunahimiza heshima kamili ya Katiba, na kufuata utawala wa sheria'

Katika ujumbe huo Maaskofu wa Kenya wanabainisha kuwa: "Tunahimiza heshima kamili kwa Katiba, kufuata utawala wa sheria, na uhuru wa taasisi zinazohusika na kulinda haki za binadamu." Maaskofu wanasema "wana wasiwasi mkubwa kuhusu ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na matumizi ya nguvu kupita kiasi na vyombo vya usalama, kukamatwa kiholela, unyanyasaji wa raia, na kupungua kwa nafasi ya kiraia na kidemokrasia."Amani ya kweli haiwezi kuwepo bila haki," wanasisitiza. Ongezeko la vurugu za kisiasa linahusishwa na maandalizi ya kampeni ya uchaguzi mkuu wa 2027.

Bunge liharakishe utekelezaji wa mageuzi muhimu ya uchaguzi

Katika ujumbe wao, Baraza la Maaskofu nchini Kenya wanabainisha kuwa: "unaitaka Bunge kuharakisha utekelezaji wa mageuzi muhimu ya uchaguzi. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) lazima iwe na rasilimali za kutosha na ipewe mamlaka ya kuanza maandalizi, ikijumuisha mafunzo yaliyopatikana kutokana chaguzi zilizopita." "Tunaisihi IEBC kuzindua mara moja kampeni ya kitaifa ya uhamasishaji wa wapiga kura na kampeni ya usajili wa wapiga kura. Hili ni muhimu ili kuhakikisha kwamba Wakenya wote wanaostahili kupiga kura, hasa vijana, wamesajiliwa na kwamba hakuna mtu anayenyimwa haki ya kupiga kura,” Maaskofu wanahimiza.

Kwaresima ni Kipindi kitakatifu:tuombe,tufunge, tutubu na kutoa sadaka

Ujumbe huo unahimishwa kwa kukumbusha kwamba “Kwaresima ni kipindi kitakatifu ambapo tutunajikita kutafakari, kuomba, kufunga, kutubu, na kutoa sadaka kwa ajili ya kuwasaidia maskini na walio katika mazingira magumu katika jamii yetu.” Kwa hivyo ni fursa ya “kuwaalika Wakenya wote kuchunguza wajibu wao binafsi na wa pamoja katika kujenga jamii yenye haki; kukataa ufisadi, vurugu, na kutojali.”

Maaskofu Kenya: Wito

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

17 Februari 2026, 18:48