COMECE yatia moyo EU juhudi za kukomesha vurugu!
Vatican News
Askofu Mariano Crociata, rais wa Tume ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Umoja wa Ulaya (COMECE), aliandika ujumbe wake uliotolewa Jumatatu tarehe 30 Machi 2026 katika muktadha wa Juma Takatifu kwamba “Kukaribia kwa Pasaka ya Kikristo kunawahimiza waamini na watu wenye mapenzi mema kuhimiza juhudi zote za kukomesha vurugu, kutoa wito wa amani, na kutoa misaada ya kibinadamu." "Maaskofu" wamefuatilia kwa wasiwasi na tahadhari ufunguzi wa vita vipya Mashariki ya Kati, baada ya kile kinachoendelea Ukraine bila kusahau migogoro mingine mingi inayoendelea iliyoenea ulimwenguni Kote," Askofu aliandika. Kwa hivyo, mawazo yetu yanawaendea raia wasio na hatia wanaokabiliwa na "mateso ambayo hayajasikika."
Kuepuka kuchochea mvutano
Askofu Crociata pia alionesha "shukrani kwa juhudi za Umoja wa Ulaya za kuepuka kuchochea mvutano, badala yake kukuza, inapowezekana, mipango yakidiplomasia na mazungumzo."Katika ujumbe wake, Askofu alikumbuka kwamba kama Wakristo na raia wa Ulaya, tunaitwa kukaribisha zawadi ya amani na kuikuza "kwa kujitolea kulinda utu wa kila mtu, kukuza haki, na kufanya kazi kwa kufuata sheria za kimataifa."
EU kama Mpango wa Amani
Kwa hivyo Askofu Crociata alirudia wito wake wa kudumisha ahadi hii, "ambayo inahitaji hamu ya umoja miongoni mwa nchi wanachama," kwa ufahamu kwamba Umoja wa Ulaya(EU) ulizaliwa kama mpango wa amani. Ndani yake, Ulaya inatambua utambulisho wake na njia pekee inayofaa ya kufuatilia mema ya watu wake. "Matumaini yetu, ni kwamba matatizo ya kiuchumi na kisiasa, hata kama ni ya kipekee, yatakabiliwa kama changamoto inayoweza kupiga hatua zaidi katika njia ya ujumuishaji wa Ulaya,"Askofu alihitimisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.