Askofu Mkuu Cupich wa Chicago Askofu Mkuu Cupich wa Chicago  (2025 Getty Images)

Jaji huko Chicago aamuru kuruhusu Huduma kwa Gereza la Brodaview,Illinois

Hii ni hatua muhimu sana katika mapambano yanayoendelea ya kuthibitisha u-Mungu na thamani na hadhi ya asili ya ndugu zetu wahamiaji katika jamii wakati ubinadamu wao unapungua na wakati udhalilishaji ni wa kawaida na wa mara kwa mara."Yalithibitishwa na Mkurugenzi wa Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma na mapadre baada Jaji huko Chicago kuamuru mamlaka ya uhamiaji kuruhusu kundi hilo kuingia katika kituo cha kizuizini kutoa huduma wakati wa Juma Kuu Takatifu.

Na Camillo Barone - National Catholic Repoter.

Jaji wa chama cha kifederali huko Chicago nchini Marekani, aliamuru mamlaka ya uhamiaji (ICE) kuruhusu kundi la Wakatoliki la Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma  na Mapadre kuingia katika kituo cha kizuizini cha uhamiaji huko Broadview, Illinois,  wakati wa Juma Takatifu, akiashiria kukemea vikali vikwazo vya serikali kwa huduma ya kidini ndani ya kituo hicho. Katika amri ya awali (preliminary injunction), iliyotolewa tarehe 31 Machi 2026, Robert Gettleman, Jaji wa Wilaya ya Marekani aligundua kuwa kukataliwa kwa serikali kuingia katika kituo hicho nje kidogo ya Chicago kuna uwezekano wa kukiuka sheria ya uhuru wa kidini ya shirikisho na Marekebisho ya Kwanza. Uamuzi huo unakubali, kwa sehemu, ombi kutoka kwa Umoja wa Uongozi wa Kiroho na Umma na wanachama kadhaa wa mapadre waliotaka kuwahudumia wafungwa katika siku zinazoelekea Pasaka.

Juma Takatifu, mojawapo ya vipindi vitakatifu zaidi katika kalenda ya Kikristo

Michael Okinczyc-Cruz, mkurugenzi mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma  na mapadre, alisema kwamba shirika la Uhamiaji na Utekelezaji wa Forodha na Idara ya Usalama wa Nchi hawakata rufaa kwa amri ya jaji na kwamba mapadre wanaweza kuingia katika kituo hicho kuanzia Alhamisi hii Takatifu hadi Dominika ya Pasaka alasiri. Amri hiyo inalenga katika dirisha finyu, lakini la dharura: Juma Takatifu, mojawapo ya vipindi vitakatifu zaidi katika kalenda ya Kikristo. Kuanzia Aprili 2 hadi Aprili 5, serikali lazima iwaruhusu Mapadre wa Chicago kuingia katika kituo cha Broadview kutoa huduma za kidini kwa wafungwa wanaochagua kushiriki.”

Kukutana na kujadiliana kuhusu huduma ya kidini inayoendelea katika kituo 

"Hii ni hatua muhimu sana katika mapambano yetu yanayoendelea ya kuthibitisha umungu na thamani na hadhi ya asili ya ndugu zetu wahamiaji katika jamii wakati ambapo ubinadamu wao unapungua, na wakati ambapo udhalilishaji ni wa kawaida na wa mara kwa mara," Okinczyc-Cruz alimwambia Mwandishi wa Habari Kitaifa Kikatoliki. "Ili kuanza ziara hizi za kichungaji siku ya Alhamisi Kuu, siku ambayo Yesu aliwaosha miguu wanafunzi wake, na Yesu alipokamatwa na mamlaka ya Kirumi, hii ni siku yenye maana sana ya kiishara ya kupata huduma ya kichungaji katika kituo cha Broadview ICE, ili washirika wa Kanisa letu, wahudumu wetu, waweze kutoa huduma ya kichungaji kwa ndugu zetu wahamiaji." Zaidi ya ufikiaji wa Juma Kuu kwa  haraka, mahakama iliwasukuma pande zote kuelekea azimio pana zaidi. Iliwaagiza "kukutana na kujadiliana" kuhusu huduma ya kidini inayoendelea katika kituo hicho, ikiwa ni pamoja na kama mapadre  wanaweza kuingia kibinafsi na wafungwa na kusali nje ya kituo hicho mbele ya wale walio ndani.

 Uamuzi huo unafuatia miezi kadhaa ya mzozo kuhusu ufikiaji wa kituo cha ICE Broadview

"Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma, unasimama katika mshikamano na jamii za wahamiaji, ukisisitiza heshima yao, ukipaza sauti zao, na kutetea matibabu ya huruma na utu," Padre David Inczauskis wa Kijesuit alisema katika taarifa. “Hatutaacha hadi tutakapofikia lengo letu la kutoa huduma ya kichungaji na Ushirika, hasa katika moja ya nyakati takatifu zaidi za mwaka." Uamuzi huo unafuatia miezi kadhaa ya mzozo kuhusu ufikiaji wa kituo cha ICE Broadview, ambapo Mapadre wa Chicago wanasema walikuwa wameruhusiwa kwa muda mrefu kutoa huduma ya kichungaji kabla ya mabadiliko ya ghafla ya sera mnamo 2025. Kulingana na mahakama, serikali iliweka vikwazo - vya kimwili na vya kiutawala - ambavyo vilizuia maombi kwa misingi hiyo na kuwazuia makasisi wanaotaka kuwahudumia wahamiaji waliofungwa ndani kuingia. Jaji alisema kizuizi hiki kilikuwa mzigo mkubwa kwa zoezi la kidini chini ya Sheria ya Urejesho wa Uhuru wa Kidini. Mahakama pia ilisisitiza hatari ya kibinadamu.

Uongozi wa Kiroho na Umma na Mapadre walipewa ruhusa ya kuingia katika kituo cha Broadview kwa ajili ya Jumatano ya Majivu

Jaji aliandika kwamba kuwanyima Mapadre  ruhusa ya kuingia inahatarisha madhara yasiyoweza kurekebishwa kwa kukiuka uhuru wa msingi wa kidini. Alitaja mfano wa muda mrefu wa Mahakama Kuu kwamba hata hasara fupi ya haki za Marekebisho ya Kwanza ni jeraha kubwa. Mnamo Februari 13, kufuatia amri tofauti ya mahakama, wanachama wa Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma na  Mapadre walipewa ruhusa ya kuingia katika kituo cha Broadview kutoa majivu na ibada za maombi zinazoashiria kuanza kwa Kwaresima. Ziara hiyo iliendelea bila usumbufu, Mapadre wa Chicago waliiambia Mwandishi wa Shirika la habari Katoliki (NCR,) baada ya ziara yao. Kwa walalamikaji, amri ya Juma Takatifu inajenga msingi wa mafanikio hayo. Muungano wa Uongozi wa Kiroho na Umma unajielezea kama mtandao wa zaidi ya Parokia 55, vyuo vikuu na vikundi vya jamii vinavyofanya kazi kushughulikia dhuluma za kijamii kupitia upangaji wa watu wa kawaida na hatua zinazotegemea imani. Kuwahudumia wahamiaji waliofungwa,  ambao wengi wao wana uhusiano na mashrika ya watu mahalia ambao  ni muhimu katika dhamira yake.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

04 Aprili 2026, 13:52