Nembo ya Ziara ya Papa huko Guinea ya Ikweta Nembo ya Ziara ya Papa huko Guinea ya Ikweta 

Sauti za watoto za furaha za sikika kabla ya ziara ya Papa nchini Guinea ya Ikweta

Waamini wote na raia wa Guinea ya Ikweta wanatarajia kuwasiliki kwa Papa Leo XIV kuanzia Aprili 21 hadi 23,2026.Watoto nchini kote wanaelezea msisimko wao kupitia mikusanyiko iliyojaa imani na matukio ya kijamii.Kambi ya Watoto ya hivi karibuni huko Malabo imeakisiwa na uhusiano mkubwa wa kiroho na shauku miongoni mwa watoto Wakatoliki nchini humo.Watawa wa Kisalesiani waliandaa mpango huo unaonesha maandalizi mapana ya kitaifa yaliyoainishwa na sala,umoja na matumaini.

Na Sr. Christine Masivo, CPS – Vatican.

Kwa ziaya ya Kitume ya  Papa Leo XIV iliyopangwa kuanzia tarehe 21 hadi 23 Aprili 2026, maandalizi yanaendelea nchini  Guinea ya Ikweta. Asasi za kiraia na Kanisa mahalia  zinashiriki kikamilifu katika kuandaa matukio yanayoakisi umuhimu wa tukio hilo, na kusisitiza jukumu la Papa kama kiongozi wa kiroho anayeunganisha  Jumuiya ya Wakatoliki na watu wote ulimwenguni.  Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Kipapa la Habari la Kimisionari Fides. Katika maandalizi hayo, Watawa wa Maria Msaada wa Wakristo pia wanaojulikanao kama Masista wa Salesiani wamekuwa mstari wa mbele kwa umakini maalum katika kuwashirikisha watoto na kuhakikisha kwamba kizazi kijacho kina jukumu muhimu katika kumkaribisha Baba Mtakatifu.  

Kambi ya watoto Machi 28-30 

Masista waliandaa moja ya mipango yenye nguvu zaidi, "Campamento Infantil 2026,” yaani “Kambi ya Watoto” iliyofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Machi 2026 katika Kituo cha utume huko Malabo, ambapo watoto 200 na wahuishaji 35 walikusanywa pamoja kwa ajili ya maandalizi mema ya ziara ya Baba Mtakatifu nchini. Sr. Giusy Becchero alisema, "hii ni tukio nzuri ambalo kama matukio yote mazuri, inagusa moyo."

Kufuata mashuhuda wa upendo

Nchi imeweka na kuipa kipaumbele Kanisa na ziara ya Papa. Kwa kuongoza na kauli mbiu ya Ziara yake nchini huko isemayo: 'Kristo anaishi!' watoto na wahuishaji wao walikuwa na Misa Takatifu, warsha, vikundi vya tafakari, vipindi vya maombi, mashindano ya michezo na jioni ya kiutamaduni yenye kusisimua. Kwa kufuata tena siku ya Pasaka, shughuli hii pia iliwasaidia watoto kuelewa umuhimu wa Kanisa na utume wa Papa kama Mchungaji wa Ulimwengu. Kila kundi lilipewa jina la Mtakatifu kama Carlo Acutis, Pier Giorgio Frassati, Kizito na Josefina Bakhita wakiwahimiza watoto kuimarisha hisia zao za kuwa sehemu ya kanisa na kutamani utakatifu.

Ushuhuda wa kiutamaduni na ujenzi wa jamii

Washiriki katika kambi walikuwa na maombi na ushuhuda wa kibinafsi ambapo walishiriki pamoja. Kuwa kwao pamoja kulisisitiza maadili ya heshima, uwajibikaji na upendo wa kindugu. Tafakari hii ilisaidia kukuza mazingira ya usikivu na shauku miongoni mwao. Walisherehekea na kuenzi tofauti wa tamaduni zao katika nyimbo, densi, na maigizo ili  kuwawezesha watoto kuelezea fahari yao katika urithi wao huku wakiimarisha uhusiano wa kijamii kupitia mila za pamoja. Sr. Giusy aliwashukuru wahuishaji wa Salesiani kwa kujitolea kwao na kazi kubwa waliyofanya kuwaongoza watoto kwa 'shauku na moyo wa Salesian'. "Jitihada zao zinasaidia kuunda mustakabali wenye mizizi katika imani, amani na matumaini, maadili ambayo yanaonekana sana huku nchi ikijiandaa kumkaribisha Papa," alisema.

Watoto wanamsubiri Papa huko Guine ya Ikweta

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

 

10 Aprili 2026, 09:43