Chagua maisha:Mtawa Mkatoliki aleta matumaini vijijini Zimbabwe
Na Sr. Christine Masivo, CPS
Kituo cha Sikhethimpilo, kinachoendeshwa na Masista Wamisionari wa Damu Azizi chini ya usimamizi wa Sr. Felistar Dube,CPS, hutumika kama kitovu cha matumaini mapya. ‘Sikhethimpilo’ linamaanisha "chagua maisha," ni kauli mbiu ambayo huishi kila siku katika kituo hicho. Kituo hicho kilianzishwa mwaka 1998 na Sr. Ludbirga Schumacher, CPS, mzaliwa wa Ujerumani, wakati wa siku zenye giza zaidi za historia ya Zimbabwe wakati Virusi vya Ukimwi (HIV/AIDS) vilipoangamiza watu na kuwaacha yatima, wagonjwa, waliotelekezwa, na kutengwa. Watu wengi walipoteza matumaini na kunyanyapaliwa ulikithiri zaidi kuliko huruma.
Kisiki kinachipuka tena
Sr. Ludbirga aliona hitaji la kuwasaidia watoto waliotengwa, maskini, na walio katika mazingira magumu, pamoja na watu wazima walioambukizwa na kuathiriwa. Alikusanya vikundi vya wanakijiiji na kuwafunza jinsi ya kutoa huduma kwa jamii hii, akapanga ziara za nyumbani, na akaanza kurejesha heshima pale ilipopotea. Aliifanya iwe dhamira yake kuwakumbusha wale wanaopambana na Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi (HIV/AIDS) kwamba maisha yao bado yana thamani, licha ya kunyanyapaliwa na ubaguzi wanaokabiliana nao katika jamii. Tumaini lilipyaishwa na shina la mti mkavu linalochipua upya likawa ishara ya mpango huo, ishara kwamba maisha hata katika hali ya kuvunjika yanawezekana. Leo hii, zaidi ya miongo miwili baadaye, Sr. Felistar anaendeleza dhamira hiyo kwa ujasiri ule ule.
Kituo cha ukuaji
Kituo cha Sikhethimpilo kinafikia nyumba za familia zilizo katika mazingira magumu, badala ya kuwatenganisha watoto na jamii zao. Kupitia usaidizi wa wafadhili, hasa kutoka Ujerumani na Hispania, kituo hicho hulipa ada za shule kwa karibu watoto 120, hutoa msaada wa kisaikolojia, na kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayehisi ameachwa katika maumivu yake. Matokeo chanya ni halisi. Wanafunzi wawili waliosaidiwa na kituo hicho sasa wako chuo kikuu, mmoja anasomea kazi za kijamii na mwingine masomo ya maendeleo, na wao hufika kutoa haya huduma mahali pale pale palipowahudumia.
Ujuzi unaobadilisha jamii
Mpango wa ajabu zaidi katika kituo hicho ni mpango wake wa mafunzo ya ujuzi wa vitendo. Kila mwaka, vijana 60 hufunzwa katika ushonaji, kilimo, mifumo ya umeme, ujenzi na kuoka. Vijana hawa wanaleta mabadiliko kijijini. Wale wanaosomea ujenzi husaidia kujenga nyumba kwa familia zilizo katika mazingira magumu, huku wanafunzi wa umeme wakiweka mfumo wa jua katika shule na nyumba za vijijini. Baadhi ya wale waliohitimu kutoka Sikhethimpilo wanafanya kazi kwa makampuni ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na mamlaka ya umeme ya Zimbabwe, wakijenga mustakabali wao wenyewe na jamii zao.
Imani na uvumilivu
Kufanya utume katika eneo lenye changamoto za kiuchumi hapakosi mahangaiko. Kuna uhaba wa maji na ufadhili si wa uhakika. Familia kubwa zinaweza kujikimu kwa muda mfupi tu kwa mgao wa chakula wa kila mwezi ambao kituo hicho hutoa. Lakini hata katikati ya changamoto hizi, Sr. Felistar anaona mkono wa Mungu ukifanya kazi. "Kuna nyakati ambapo tunafikiri hatuwezi kuendelea: hakuna mishahara, hakuna fedha, hakuna chakula cha kuwapa watu," alisema. "Lakini sala hutuweka tukisimama, kumwamini Mungu na kutusaidia kusonga mbele."Imani yake ni rahisi na ya kina. Mungu atawatengenezea njia wale wanaochagua maisha.
Mahali patulivu penye mguso mkubwa
Kutokana na hali ngumu ya kiuchumi nchini Zimbabwe, na ufadhili mdogo kutoka kwa wafadhili wa kimataifa, watawa hao hujitahidi kuwasaidia watu katika eneo hilo kwa kuwawezesha na kuunda ajira, ili waweze kujikimu. Kama njia ya kuunga mkono kazi yake ya kibinadamu, Sikhethimpilo inatoa vyumba kadhaa vya wageni, ukumbi wa mikutano, na huduma ndogo ya upishi. Mapato kutokakwenye kituo hiki hulipa mishahara ya wafanyakazi na na kuiwezesha utume kupata kipato.
Hata hivyo, changamoto bado ipo, jengo hilo ni nzuri na la kawaida lakini la zamani, tangu mwanzoni wakati kituo hicho kilipoanzishwa mwaka 1998, linahitaji ukarabati. Majumba ya kisasa vimeibuka katika eneo hilo vyenye ushindani, lakini watu wengi bado wanapendelea Sikhethimpilo kwa sababu ya utulivu na amani iliopo na na utume wake wa roho ya ukarimu. "Watu wafahamu kwamba watapokelewa vema mahali hapa,” Sr. Felistar alielezea, "na wanakuja kwa sababu wanahisi nyumbani mahali hapa."
Daima wakiwa na kusudi
Sr. Felistar kwa sasa anahudumu kama mtawa wakati wote katika kituo hicho. Jumuiya yake ya kitawa ni ndogo, lakini azma yake ni kubwa. Anaamini kwamba Sikhethimpilo siku moja ataweza kukua na kuwa kituo cha mafunzo ya ufundi, kitu ambacho vijana katika eneo hilo wanahitaji sana. "Tunafanya kazi pamoja kama watawa na watu tunaowahudumia, tunajitolea kama sadaka kwa Mungu," Sr. Felistar alisema kwa shukrani. "Kwa familia tunazowapa msaada, ninakushukuru, mnathamini hata kidogo tunachowapa, shukrani yenu inatupati nguvu. Na kwa wafadhili wetu hatuwezi kusimama kidete bila nyinyi, mbarikiwe sana.” Kazi ya Sikhethimpilo inategemea ukarimu wa washirika wake, kama vile Marafiki wa Kijerumani na Manus Unitas. Usaidizi wao unawasaidia Masista Wamisionari wa Damu Azizi kuendelea kuleta uhai, elimu, na heshima kwa walio katika mazingira magumu.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.