Haiti:Askofu atoa wito kwa viongozi wa dunia kuwasaidia watu wanaoteseka
Na Federico Piana – Vatican.
Nchi ya Haiti ikiwa imeachwa na kila mtu, tumaini liko katika sala, kulingana na Askofu Pierre-André Dumas wa Jimbo la Anse-à-Veau-Miragoâne nchini Haiti. Akizungumza na Vatican News, Askofu huyo, pia makamu rais wa Baraza la Maaskofu, mara nyingi alisisitiza hitaji la usaidizi wa maombi. Ingawa sauti yake ina wasiwasi mkubwa, pia alielezea matumaini ya mshikamano: "Watu wetu wameteseka kwa miaka mingi bila mtu yeyote anayeonekana kujali. Ndiyo maana dunia lazima isaidiwe kufahamu upya hisia ya mshikamano thabiti na Haiti kupitia sala. Itakuwa nzuri sana kuona watu binafsi, parokia, taasisi, familia, na jumuiya za kidini zikikusanyika pamoja kwa siku ya maombi duniani kote."
Wito wa kukata tamaa
“Kwa miaka mingi, Kanisa la hapa limekuwa likitoa wito wa kukata tamaa kwa Jumuiya ya Kimataifa ambazo hazijapatiwa majibu.” Kwa mujibu wa Askofu, vurugu za genge zinazosababisha vifo vya watu wengi kila siku, umaskini uliokithiri, na ukosefu wa utulivu wa kisiasa unaosababisha dhuluma na ukosefu wa usawa vimeshindwa kuvunja vipaumbele vya serikali za kimataifa vinavyolenga kwingineko. Lakini Askofu Dumas alikataa kukata tamaa na aliendelea kulia kwa sauti kubwa zaidi kuliko hapo awali kuwa: "Ninaamini kwamba ndani ya familia ya mataifa, ndugu mwenye nguvu zaidi hawezi kumsahau ndugu dhaifu na aliyejeruhiwa. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kujiruhusu kupingwa na kinachoendelea Haiti. Nchi yangu iko umbali wa saa moja tu kutoka Marekani, nguvu inayoongoza duniani. Hata hivyo inatumia pesa nyingi kwenye vita huku sisi tukiteseka kando yake. Haiti haiombi huruma ya juu juu, bali udugu halisi."
Kuteseka kwa miongo kadhaa
Viongozi wa dunia Askofu alisema kuwa, wanafahamu vyema mateso ya watu wa Haiti kwani yamekuwa yakiendelea kwa miaka mingi, daima ni yale yale. Na Askofu Dumas alisimulia tena jinsi "ghasia za magenge yenye silaha zinavyoendelea kueneza hofu, vifo, na uharibifu. Sehemu kubwa ya mji mkuu, Port-au-Prince, inadhibitiwa na magenge. Maelfu ya familia wamelazimika kukimbia nyumba zao, ambazo mara nyingi huchomwa au kuharibiwa. Watoto na vijana wanaishi wakiwa na kiwewe katika hali ya kudumu ya ukosefu wa usalama."
Mgogoro wa kibinadamu
Kisha kuna mgogoro wa kibinadamu. Zaidi ya watu milioni tano wako hatarini kufa kwa njaa. Idadi kubwa ya watu hawana huduma za msingi za afya kwa sababu baadhi ya hospitali zimekaliwa na magenge, huku shule nyingi zikiwa zimefungwa na maelfu ya wanafunzi wananyimwa haki ya kupata elimu. Kiwango cha kisiasa na kitaasisi pia kimeanguka katika mgogoro ambao haujawahi kutokea. "Kuna," Askofu Dumas alilaani, "udhaifu mkubwa katika taasisi za serikali, ambapo kuna kutoaminiana sana, ufisadi mkubwa wa umma, na ukosefu wa utulivu usio wa kiafya wa serikali. Haiti ni jeraha upande wa dunia ambalo linapaswa kutikisa dhamiri ya kila mtu."
Usaidizi kutoka Vatican
Askofu Dumas alifahamu vyema kwamba wasiwasi kama huo hauwezi kuchukuliwa kirahisi. Ndiyo maana aliishukuru Vatican kwa kuendelea kuwaunga mkono watu wake wapendwa. "Mkutano kati ya Papa Leo XIV na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, na ujumbe wa serikali ya Haiti siku chache zilizopita ulituwakilishia juhudi thabiti kuelekea amani. Baada ya yote, ilikuwa Vatican ambayo ilitambua uhuru wa jimbo letu kwa mara ya kwanza."
Ndoto kubwa
Katika moyo wa Askofu wa Anse-à-Veau-Miragoâne ambaye kwa sasa anandelea na matibabu na kupata nafuu huko Florida nchini Marekani, baada ya kunusurika shambulio la magenge yaliyopinga juhudi zake za kupatanisha amani kati ya serikali na vikundi vyenye silaha kuna hamu nyingine. Aliiita ndoto: "Kuona Papa akitembelea Haiti siku moja. Nina uhakika kwamba uwepo wake, kama kivuli chenye mwanga lakini chenye nguvu, unaweza kuleta amani kubwa."
Imesasishwa tarehe 15 Mei 2026 saa 9.45 Alasiri na Sr Christine Masivo.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.