2026.05.17 Kardinali Mario Grech wakati wa Mkutano wa Katholikentag 2026 huko Würzburg 2026.05.17 Kardinali Mario Grech wakati wa Mkutano wa Katholikentag 2026 huko Würzburg 

Kard.Grech,Katholikentag:Maswali hayapaswi kutukatisha tamaa

Kardinali Mario GrechKatibu Mkuu wa Sekretarieti ya Sinodi alizungumza na Vatican News katika Mkutano wa 104 wa Katholikentag,ambao ni mkutano mkubwa wa Wakatoliki wa Ujerumani na alisema kwamba Kanisa nchini humo “linanipa ujasiri mkubwa,tumaini kubwa.”

Na Christine Seuss – Würzburg

Kardinali Mario Grech, Katibu Mkuu Sekretarieti ya Sinodi, alikuwa mwakilishi wa Vatican katika Mkutano wa 104 (Katholikentag) ambao ni mkutano mkubwa wa Wakatoliki wa Ujerumani ambapo mwaka huu ilifanyika huko Würzburg, Ujerumani. Kardinali Grech alishirikishi  mjadala wa jopo tarehe 16 Aprili, 2026, kuhusu Sinodi katika Kituo cha Mkutano cha Würzburg, ambapo alitoa hotuba kuu. Dominika tarehe 17 Mei 20 aliongoza Misa ya kufunga na kusoma ujumbe na kuelezea ukaribu na baraka za Papa Leo XIV. Kardinali akielezea juu ya Papa alisema “Anabaki karibu nanyi na anasimama kwa moyo wote kando yenu akiunga mkono umoja na ushirika. Kama angekuwa hapa leo, nina uhakika angewaambia: Jipeni moyo, inukeni!”

Askofu Wilmer akizungumza na Mwandishi wa habari wa Vatican Christine Seuss
Askofu Wilmer akizungumza na Mwandishi wa habari wa Vatican Christine Seuss

Kwa Kardinali alisema kuwa “ Kanisa la kisinodi la kweli lina mustakabali ikiwa litaendelea kuwa wazi kwa Roho Mtakatifu.  Tumebarikiwa sana na huduma ya Askofu wa eneo kwa ajili ya Kanisa la eneo na huduma ya Petro kwa Kanisa la ulimwengu wote; kwa pamoja wanaweza kuhakikisha kwamba tunatimiza mapenzi ya Mungu.” Kabla ya kuonekana kwake hadharani, Kardinali Grech pia alitembelea vibanda na mipango mingi iliyoenea katikati mwa jiji la Würzburg, akitumia muda wa kukutana na washiriki na kushiriki katika mazungumzo. Katika hotuba yake, aliwaalika washiriki kufikiria Sinodi kama ala  ambayo kila chombo kina jukumu lake na uhalali wake, lakini ambapo maelewano hatimaye yana umuhimu zaidi. Ushiriki na ushirika, alisisitiza, lazima vibaki vimeunganishwa kwa karibu. Zaidi ya yote, Kanisa lazima litengeneze nafasi kwa ajili ya Roho Mtakatifu kutenda na kamwe lisipuuze mwelekeo wake wa kimisionari.

Kardinali Grech alisisitiza kwamba Sinodi haiwezekani bila ushiriki wa Makanisa mahalia, kama vile Makanisa mahalia hayawezi kueleweka mbali na Kanisa la ulimwengu wote. Uamuzi wa Sinodi, alionya, haupaswi kuwa suala la ujanja wa kisiasa au kupiga kura kwa wingi, lakini unapaswa kutokea kutokana na utambuzi wa kiroho unaotokana na kusikiliza na mahusiano. Wakati huo huo, alisisitiza kwamba hapapaswi kuwa na hofu ya maswali magumu. Maswali kama hayo, alisema, yanasaidia Kanisa kuchunguza kwa undani zaidi masuala na kuelewa vyema jinsi sinodi inavyoweza kutafsiriwa katika maisha ya kila siku. Mitazamo na misimamo tofauti ndani ya Kanisa inapaswa kuwa chanzo cha utambuzi na utajiri wa pande zote badala ya sababu za migogoro. Wakristo, wameitwa kujibu kwa ubunifu na kinabii mahitaji ya jamii zao huku wakibaki na mizizi imara katika Injili, aliongeza.

Mkutano Mkuu wa  Katholikentaga 2026
Mkutano Mkuu wa Katholikentaga 2026

Akizungumza kando ya tukio hilo, Kardinali Grech alisisitiza kwamba tafakari kuhusu jukumu la Watu wa Mungu lazima libaki likiwa limejikita katika mafundisho ya Mtaguso wa Pili wa Vatilcan. Tofauti na sinodi zilizotangulia zilizolenga masuala maalum, alisema, Sinodi kuhusu Kisinodi ni mchakato unaoendelea ambao kazi yake itaendelea hadi katika mkutano mkuu wa Kanisa uliopangwa kufanyika mwaka 2028.

Wakati wa mahojiano na Vatican News
Wakati wa mahojiano na Vatican News

Uko hapa Würzburg kama mwakilishi wa wadhifa wa juu zaidi wa Vatican. Ni ujumbe gani kutoka kwa Papa Leo XIV umewaletea Wakatoliki wa Ujerumani?

Papa Leo XIV anafuatilia maisha ya Kanisa nchini Ujerumani kwa karibu. Yeye ni baba mwema, kama baba mwema, anasindikizana na watoto wake wote. Sijui jinsi anavyosimamia, lakini Papa pia anayapatia kipaumbele Makanisa mahalia. Kwa hivyo nina uhakika kwamba anawasindikiza maaskofu kwa njia maalum, kwani hatimaye wao ni washirika wake.

Sasa uko katika mazingira ambayo yanawaunganisha Wakatoliki wengi ambao wanaweza kutofautiana lakini wameungana katika imani. Tukio hili limekuletea hisia gani?

Linanipatia ujasiri mkubwa, tumaini kubwa. Kwa sababu hili si Kanisa lililokufa. Ni kweli kwamba watu wanauliza maswali. Lakini hilo ni jambo zuri. Maswali hayapaswi kutukatisha tamaa; kinyume chake, ni fursa ya kufafanua na kuelewa mambo zaidi. Tukifanikiwa kutembea pamoja katika njia ya Kanisa Katoliki, basi hatuhitaji kuogopa. Lazima tujipe muda unaohitajika, kwa sababu wakati mwingine muda unahitajika ili kukomaa na kuelewa kikamilifu zaidi. Lakini tunaendelea kusonga mbele.

Wakati mwingine, kuna mtazamo kwamba Kanisa nchini Ujerumani linaonekana kwa kutoaminiana, labda hata na Vatican, kwa sababu ya masuala yanayojadiliwa sana hapa. Ungetoa ushauri gani kuhusu sinodi, ambayo inadaiwa sana nchini Ujerumani?

Naweza kukuambia kwamba nimekutana na maaskofu wengi kutoka Ujerumani, na sioni maaskofu waoga. Ninaona maaskofu wakiandamana na watu wao. Bila shaka, wao pia wanahitaji msaada na usaidizi. Ushauri wangu ni huu: tunashiriki katika mchakato wa kutafakari. Tunatembea katika ardhi takatifu, kwa sababu sinodi ni ufunguo wa kuelewa, katika angalau kwa sehemu, mapenzi ya Mungu. Na ili kufikia hili, tunahitaji hali ya kiroho imara. Nilipotembelea vibanda vya Katholikentag, mshiriki mmoja wa Kijerumani aliniambia: ‘Kardinali, tunahitaji hali ya kiroho sana, vinginevyo tunahatarisha kuendeleza mpango  wetu wenyewe badala ya mapenzi ya Bwana.’

Pia ulitangaza kwamba katika siku zijazo Sekretarieti ya Sinodi itachapisha miongozo ya kusindikiza Makanisa mahalia kuelekea mkutano wa 2028. Mada kuu ya hati hiyo ni ipi?

Ni tafakari inayoanzia ngazi ya chini - katika kila Kanisa mahalia. Sasa tuko katika awamu ya kutekeleza hati ya mwisho ya Sinodi. Kila Kanisa mahalia linaalikwa kutafsiri matunda ya hati hiyo kuwa uzoefu wa sinodi ulio hai. Kupitia mikutano ya Maaskofu, tutaomba kila mtu kushiriki matokeo nasi ili, mwaka 2028, tuweze kubadilishana uzoefu huu na  ni  kwa nini kutafuta majibu pamoja popote ambapo maswali bado yanabaki?

Mkutano wa  Katholikentag 2026 Ujerumani
Mkutano wa Katholikentag 2026 Ujerumani

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
 

20 Mei 2026, 09:48