Moto Mkali sana uleteketeza maeneo mengi huko Andalusia Moto Mkali sana uleteketeza maeneo mengi huko Andalusia  (AFP or licensors)

Andalusia,Askofu wa Almería:Tuwe mikono ya Mungu kwa wale wanaoteseka

Askofu Antonio Gómez Cantero alitafakari kuhusu mkasa wa moto wa porini huko Bédar na Los Gallardos,akisisitiza mshikamano uliooneshwa na wakazi wa eneo hilo na mwitikio wa Kanisa la eneo hilo.Alitoa wito wa matumaini katika maumivu na hasara,utunzaji wa uumbaji na imani hai iliyojikita katika jumuiya na huruma.

Na Sebastián Sansón Ferrari – Vatican.

Kanisa la huko Almería linawaomba watu wenye mapenzi mema  kuwa karibu na wakazi wa miji ya Bédar na Los Gallardos, waliothiriwa na mkasa wa moto wa porini ulionza tarehe 9 Julai 2026 na kuwasaidia kukidhi mahitaji yao ya dharura. Watu 13 walithibitishwa kufariki na 8 kujeruhiwa. Wengine 23 bado hawajulikani walipo kufuatia moto huo huko Andalusia - Los Gallardos, na tangu wakati huo umeenea kwa hekta 6,600. Karibu wakazi 1,500 wamehamishwa makazi yao. Andalusia ni Jumuiya ya kujitegemea  katika wilaya ya Almería. Akizungumza na Vatican News, Askofu Antonio Gómez Cantero wa Almería alisema kwamba moto ulienea kwa kasi ya ajabu, ukiendeshwa na halijoto ya juu na upepo mkali, ukipita kwenye makorongo na maeneo ambayo ni ngumu kufika na kwenye makazi ya watu wengi. "Kila dakika, upepo ulisukuma moto mita mia moja zaidi kwenye vichaka," alisema.

Mamlaka zilibadilisha hatua za uokoaji kulingana na hali mahalia, huku parokia na Caritas zikipanga hatua za haraka za msaada kwa waliohamishwa. Wakazi wengi walipata makazi katika vituo vya muda, huku wengine wakikaribishwa katika nyumba za kibinafsi. Askofu alisifu mshikamano ulioonyeshwa na wajitolea ambao waliotoa chakula na maji kwa wazima moto na kuwasaidia wale waliolazimika kukimbia makaazi yao. “Watu wote waliungana katika janga hilikubwa,”  alisema. Askofu pia alikumbuka jinsi mwanamke mmoja wa eneo hilo alivyopiga kengele za kanisa la parokia kuwaonya wakazi kuhama, hii ilikuwa njia ya kitamaduni ya kuwatahadharisha jamii wakati wa dharura.

Mwitiko wa Jimbo katika uchungaji

Akitafakari mwitiko wa Jimbo lake la kichungaji, Askofu Gómez Cantero alisema mapadre walibaki pamoja na wakaazi wa eneo hilo tangu mwanzo wa janga hili la moto, wakiwasaidia hasa wazee na familia zilizohamishwa. Naya alitangaza kwamba atawatembelea jamii zilizoathiriwa wakati wa sherehe za sikukuu ya Mama Yetu wa Mlima Karmeli. Akizungumzia kuhusu gharama ya maisha  katika janga hilo, alirejelea wale waliopoteza maisha yao, utambuzi wa waathiriwa, na wakwea mlima wawili waliopatikana wakiwa hai siku mbili baada ya kukwama kwenye korongo. Askofu alipoulizwa Mungu yuko wapi kati ya mateso hayo, alikumbuka maneno ya padre wake mmoja aliyesema kwamba "Mungu yuko pamoja nanyi, akiteseka hivi Msalabani." Aliwasihi Wakristo wasizingatie na kunyosha kidole cha lawama bali kuwajali wale walioathiriwa. "Sasa si wakati wa wakuwalaumu wengine, sote tunapaswa kuchukua jukumu na kuwasaidia  wake wanaoteseka,” alisema, akiwaita waumini kuwa "Kanisa la Wasamaria." Akikumbuka mfano wa Msamaria Mwema, alisema Wakristo wameitwa "kuwaona, kuwakaribisha, kuwaponya, kuwarejesha na kuwalinda wale wenye mahitaji.

Mshikamano ni ishara ya matumaini

Askofu alielezea mshikamano unaoonyeshwa na majirani, parokia na wajitolea kama ishara ya matumaini. "Kuanza tena ni kutazama wakati ujao, na kuanza tena ni kuwa na tumaini," alisema. Aliongeza kuwa Wakristo wameitwa kuwa vyombo vya huruma ya Mungu: "Mara nyingi, sisi ni mikono ya Mungu, miguu ya Mungu, macho ya Mungu, sauti ya Mungu na masikio ya Mungu, kwa sababu imani yetu inatuita kumleta Mungu kwa wengine kupitia maisha yetu wenyewe." Hatimaye, Askofu Gómez Cantero alisema msiba huo unapaswa pia kuhamasisha utunzaji mpya kwa uumbaji. Akirudia mafundisho ya Ensiklika ya Papa Francisco wa  Laudato si', alisisitiza umuhimu wa kutunza misitu na kuishi kwa amani na asili."Tukijali asili, asili itatujali," alisema.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

16 Julai 2026, 09:17