Ufaransa:Wasiwasi wa Maaskofu kuhusu Sheria ya Mwisho wa Maisha
Na Jean-Charles Putzolu –Vatican.
Kanisa nchini Ufaransa lilielezea kusikitika kwake, Jumatano jioni tarehe 15 Julai 2026 kufuatia na idhini ya mwisho ya Bunge la Kitaifa ya mswada wa sheria, kuhusu haki ya kujiua kwa usaidizi. “Ninajuta kwa uamuzi unaovunja utamaduni mrefu wa utunzaji na wito wa kupunguza mateso na kusindikizana na kila mtu hadi mwisho wa asili ya maisha yake,” alisema Msemaji wa Kanisa. Maaskofu walikumbuka ushiriki wao katika mazungumzo kuhusu mada hiyo katika kipindi cha miaka minne iliyopita, wakisisitiza uzoefu wa Kanisa la karne nyingi katika kuwasindikiza wagonjwa na familia zao. Kulingana na Maaskofu, athari za sheria hiyo zitabadilisha uhusiano na udhaifu, uzee, ulemavu, na magonjwa. Hata hivyo, Maaskofu wa Ufaransa hawakati tamaa: "Historia haijaisha," wanasema. "Njia nyingi za kisheria zinabaki wazi," Askofu Mathieu Rougé, wa Jimbo la Nanterre na msemaji wa Baraza la Maaskofu wa Ufaransa (CEF) kuhusu masuala ya mwisho wa maisha, alielezea kwa vyombo vya habari vya Vatican.
Mwashamu, kuhusu kifungu cha dhamiri kilichotolewa katika sheria mpya, kinafanyaje kazi kwa taasisi za Kikatoliki?
Sheria, kama ilivyoidhinishwa, inajumuisha kifungu cha pingamizi la dhamiri kwa madaktari. Hata hivyo, inasikitisha kwamba haijumuishi kifungu cha pingamizi la dhamiri kwa wafamasia, ambao, katika visa vya kujiua kwa usaidizi nyumbani, watalazimika kutenda kama tendo hilo la kudunga sindano hatari ya kifo. Kwa upande mwingine, jambo linalotia wasiwasi zaidi, ya ukweli rahisi wa kuidhinisha kujiua kwa usaidizi, ni kwamba, taasisi ambazo sheria zao za kimaadili au historia ya kidini inalaani kitendo cha euthanasia—zitalazimika kutoa. Hiki si kifungu cha kupinga dhamiri kwa sababu dhamiri ni jambo la kibinafsi. Ni sharti la kitaasisi. Katika hatua hii, serikali ilikuwa imetoa uhakikisho fulani kwa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Ufaransa ambao bado haujatimizwa. Kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa Taasisi za kitawa na zile zenye asili ya kidini. Ninawafikiria hasa Dada Wadogo wa Maskini, lakini pia Masista wa Mtakatifu Thomas wa Villanuova, Mtakatifu Mlinzi wa hospitali za Kikatoliki za uzazi. Pia kuna taasisi kama Jeanne Garnier huko Paris. Inatarajiwa kwamba katika Majuma yajayo, changamoto mbalimbali za kisheria zitasababisha kifungu cha kitaasisi, ili taasisi ambazo historia yake, hali ya sasa, au hati ya maadili inalaani kujiua kwa usaidizi ziweze kuendelea na dhamira na maadili yao.
Kanisa la Ufaransa linaweza kuwa na sauti gani leo?
Mnamo tarehe 15 Julai 2026, Baraza la Maaskofu lilichapisha taarifa iliyosainiwa na rais na makamu wawili wa rais, likielezea huzuni na wasiwasi wa maaskofu. Aina hii ya sheria inashindwa kushughulikia kikamilifu matokeo katika suala la udugu, maisha ya kijamii, na upanuzi unaoendelea wa vigezo. Kwa hivyo, uangalifu mkubwa unahitajika. Sasa ni wakati wa kusonga mbele, hasa kwa kufuatilia uhuru mzuri wa taasisi, kuhakikisha kufuata kanuni zao za maadili, na kwa kuhimiza na kufuatilia kwa karibu miito yote niliyotaja.
Kuna watu katika hali ya upweke, udhaifu, na unyonge ambao wametengwa, wapweke, na hawawezi kuungwa mkono. Wakikabiliwa na swala la msingi la maisha ya mwanadamu, watu hawa watajikuta peke yao wanapokabiliwa na chaguo la mwisho wa maisha: kuishi au kufa...
Jibu la Wakristo kwa idhini ya sheria kama hii si kutokubali kimaadili tu, bali pia ni hitaji la kujitolea. Hii ndiyo sababu, katika taarifa tuliyochapisha Jumatano jioni na katika misimamo mbalimbali iliyochukuliwa na baadhi yetu, hata kabla ya kupigia kura sheria hiyo, tuliwahimiza Wakristo kufanya kila wawezalo ili kushirikiana zaidi na watu wanaopitia udhaifu, upweke, na hatari. Kwanza kabisa ni kwa njia ya udugu wa kazi kwamba tutaitikia kukata tamaa ya kukatisha maisha ya mtu, ambayo wakati mwingine hupitia mioyo ya watu katika shida kubwa na kutengwa kwa kina. Jibu letu si la kimaadili tu kwa asili, lakini kimsingi ni dhamira ya kidugu. Hivi ndivyo tunamaanisha ... Naomba Wakristo wa Ufaransa, zaidi ya sheria - ambayo kamwe si kitu kingine isipokuwa sheria - wajitolee zaidi na zaidi kwenye njia ya udugu. Hili ndilo litakalotuwezesha kuzuia kifo kilichosababishwa na kuchukua nafasi isiyo na uwiano katika nchi yetu.
Baada ya miezi miwili Ufaransa itapokea ugeni kutoka kwa Papa Leo XIV. Unatarajia aseme nini juu ya mada hii?
Nina uhakika kwamba Papa atatuambia mambo muhimu sana katika maeneo mengi, hasa katika hili. Alizungumza kwa nguvu hivi karibuni huko Roma, lakini pia nchini Hispania. Mara nyingi nimenukuu kifungu chenye mkazo sana kutoka katika Waraka wa Magnifica Humanitas, ambapo Baba Mtakatifu anatangaza kwamba, haki ya kwanza, ile inayowapatia wengine wote masharti, ni haki ya kuishi, na kwamba wakati euthanasia inapohalalishwa, haki hii inadhoofishwa kwa kiasi kikubwa. Pia nafikiria tamko la Kiti Kitakatifu,Samaritanus Bonus, ya 2020, maandishi muhimu sana kuhusu mada hii. Nina imani kwamba Papa Leo XIV atakuwa na mambo muhimu ya kuwaambia Wakristo, kuwasaidia kushirikiana na watu walio katika mazingira magumu, na kwa jamii yetu kwa ujumla. Kwa kawaida, tungefurahi kumkaribisha katika muktadha mzuri zaidi wa kisheria, lakini maneno yake, kuhusu jambo hili kama ilivyo kwa mengine mengi, yatakuwa na thamani kubwa kwetu, na tunayasubiri kwa subira kubwa."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.