2026.07.15 Shule ya Sekondayi ya Mslaba Mtakatifu ya  Lake View Senior kuadhimisha Tamasha la Kijani la Laudato Si’ huko  Jinja,Uganda. 2026.07.15 Shule ya Sekondayi ya Mslaba Mtakatifu ya Lake View Senior kuadhimisha Tamasha la Kijani la Laudato Si’ huko Jinja,Uganda. 

Uganda:Akili na maisha ya vijana kubadishwa Uganda

Mnamo tarehe 11 Julai 2026 tamasha la “Laudato Si’ Green” lilifanyika katika Shule ya Sekondri ya “Holy Cross Lake View,” Wanyange,Jinja,jiji lililoko ufukweni mwa Ziwa Victoria.Padre Peter Caxton Mayanja,Mmisionari wa Shirika la Wamisionari wa Msalaba Mtakatifu wa Kanda ya Afrika Mashariki,aliongoza Misa ya tamasha hilo.

Na Sr. Stella Watsema,OLGC, - Vatican.

Likiadhimishwa kwa kuongozwa na  mada ya mwaka huu 2026: “Uhifadhi wa Mazingira kwa ajili ya Amani na Maendeleo Endelevu,”(the green Festival) Tamasha la Kijani,  liliandaliwa na Klabu ya Laudato Si ya Shule ya Sekondari ya Msalaba Mtakatifu ya Lake View, Wanyange, na kikund cha Vijana cha Laudato. Mpango huo ni mpango wa hatua za tabianchi  na ikolojia unaoongozwa na vijana ambao unaotokana na Mafundisho Jamii ya Kanisa Katolili (KKK) ulioongozwa na Warka wa hati Laudato Si’ ya Ikolojia ya Papa Francisko ya 2015:  Shule ya Sekondari ya Msalaba Mtakatifu ya Lake View ni ya bweni kuanzia kidato cha Kwanza hadi cha Sita huko Wanyange, Jinja. Shule hiyo inamilikiwa na Shirika la Msalaba Mtakatifu la Afrika Mashariki na inalenga kutoa elimu kamili, inayozingatia thamani ya maisha ya mwanadamu.

Picha ya pamoja mara baada ya misa
Picha ya pamoja mara baada ya misa

Siku iliyojaa matukio

Katika Misa Takatifu yenye uchangamfu iliyoadhimishwa na Padre Peter Caxton Mayanja, Taasisi kadhaa za elimu zinazoongozwa na wamishonari wa Msalaba Mtakatifu, shule za serikali na taasisi za kibinafsi katika Wilaya hiyo, walihudhuria misa hiyo. Viongozi wa Serikali za mitaa na kitaifa pia walikuwepo. Mgeni rasmi katika Tamasha hilo alikuwa Justine Kasule Lumumba, Waziri wa Tehama na Mwongozo wa Kitaifa wa Uganda. Kwa ujumla, shughuli hizo zilijumuisha (Green Walk), yaani Matembezi ya Kijani,  matukio yanayohamasisha matumizi mazuri ya teknolojia, upandaji miti na usambazaji wa vichipukizi vya miti. Pia kulikuwa na nafasi ya maonesho ya ikolojia na wanafunzi na usimulizi wa historia kama zana muhimu kwa ikolojia Fungamani. Katika mahubiri yake, Padre Peter Caxton Mayanja alisema “kutomtambua Kristo kunafanya wanadamu kuwa vipofu hata katika majukumu ambayo wamepewa na Mungu.” Kwa uzoefu wake binafsi katika simulizi wa historia na kusoma, Padre Mayanja alizungumzia “umuhimu wa simulizi kwa ajili ya ufahamu wa ikolojia.”

Shule na mazingira yake yenye kuvutia na miti
Shule na mazingira yake yenye kuvutia na miti   (AFP or licensors)

Urithi wa Laudato Si’ nchini Uganda

Padre Mayanja alisema kwamba ujumbe uliokuwa kwenye mabango ya Matembezi ya Kijani ulivutia umakini wake na kumsukuma kutafakari. “Matembezi ya Kijani” ni matembezi ya Imani ambapo wanafunzi, wakuu wa shule, viongozi wa kidini, na wanajamii wa Wanyange wanaandamana pamoja ili kuongeza uelewa kuhusu kutunza uumbaji. Tamasha la Kijani la Laudato Si’ ni mojawapo ya matukio na mipango mingi ambayo Shirika la Wamisionari wa Msalaba Mtakatifu, kupitia Taasisi yake ya Shule ya Sekondari ya Msalaba Mtakatifu ya Lake View, Wanyange, inatumia kuwatia moyo wanafunzi na vijana kuchukua hatua na kulinda mazingira. Shule hiyo si ushuhuda wa urithi wa Papa Francisko wa Laudato  Si tu,  bali pia ni ule unaotafuta kutimiza malengo yake: Kufundisha akili, kugusa mioyo, na kubadilisha maisha.

Wanafunzi wakionesha mbinu ya kutunza mimea
Wanafunzi wakionesha mbinu ya kutunza mimea

Imesasishwa tarehe 17 Julai 2026 saa 4.05 na Sr Christina Masivo.

UGANDA AKILI NA MAISHA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

17 Julai 2026, 10:05