Kardinali Pierbattista Pizzaballa,Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu hivi karibuni alitembelea Taybeh,kijiji cha mwisho cha Kikristo kilichobaki huko Palestina na kuomba hifadhi ya Kikristo katika Kijiji hiki. Kardinali Pierbattista Pizzaballa,Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu hivi karibuni alitembelea Taybeh,kijiji cha mwisho cha Kikristo kilichobaki huko Palestina na kuomba hifadhi ya Kikristo katika Kijiji hiki.  (AFP or licensors)

Kardinali Pizzaballa Atembelea Taybeh, Aomba Hifadhi ya Kikristo Katika Eneo Hili

Kardinali Pierbattista Pizzaballa,Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, hivi karibuni alitembelea Taybeh, kijiji cha mwisho cha Kikristo kilichobaki huko Palestina. Huku kijiji kikikabiliwa na vikwazo vikali vya mawasiliano alisisitiza,"Mfano wenu ni muhimu ili tuweze kuendelea kuwa sauti ya Kikristo katikati ya hali hii ngumu sana." Amewahimiza wakaazi wa mji huu kulinda, kuhifadhi na kutunza amana na utajiri wa historia ya Kikristo katika eneo hili, kama kumbukumbu endelevu!

Na Valerio Palombaro, - Vatican.

Kardinali Pierbattista Pizzaballa, Patriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, alionesha mshikamano wake na watu wa Taybeh wakati wa ziara yake katika kijiji kidogo cha Kikristo katika Ukingo wa Magharibi kwenye Sherehe ya Kupalizwa kwa Bikira Maria. Tutaendelea kufanya kila tuwezalo kuhifadhi uwepo wa Kanisa hapa, katika kila ngazi, katika Nchi Takatifu. Huenda nisiwe na majibu katika ngazi ya kibinadamu au ya kidunia, lakini ninaamini katika Mungu. Na nina uhakika kwamba, kwake, tunaweza kuendelea kuleta uzima, hata hapa Taybeh," Kardinali Pizzaballa alisema hayo wakati wa Misa katika Kanisa la Kilatini la Kristo Mwokozi huko Taybeh. Kukaribishwa “miongoni mwa watu wake”: Akimkaribisha Patriaki mwanzoni mwa Ibada ya Misa Takatifu, Padre Bashar Fawadleh wa Parokia ya Taybeh, alisema kwamba kijiji hicho kilimkaribisha “miongoni mwa watu wake na nyumbani kwake.” Kulingana na taarifa kutoka Upatriaki wa Kilatini wa Yerusalemu, Padre huyo alielezea uwepo wa Kardinali kama ule wa Baba aliyesimama kando ya watoto wake katika nyakati ngumu.

Kanisa linasimama na waamini wake likiwa limebeba Msalaba wa Matumaini
Kanisa linasimama na waamini wake likiwa limebeba Msalaba wa Matumaini   (AFP or licensors)

Padre Bashar pia alisema kwamba uwepo wa Kardinali Pizzaballa uliikumbusha jamii kwamba wako pamoja na kwamba Kanisa linasimama na watoto wake, likiwa limebeba “Msalaba na matumaini ya nchi hii.” Kardinali Pizzaballa alielezea Sherehe ya Kupalizwa Mbinguni kama “tunda la Ufufuko” na kusema kwamba Maria anawafundisha Wakristo kutazama uhalisia “kwa macho ya kimungu,” badala ya mtazamo wa kibinadamu. Kisha aliunganisha ujumbe huu moja kwa moja na Taybeh, akiwahimiza watu wake kisimama imara katika imani na matumaini hata wakati hali zinapofanya wakati ujao kuwa mgumu au uonekane kuwa hauwezekani.

Haya ni maeneo ya historia ya Ukristo yanapaswa kuhifadhiwa
Haya ni maeneo ya historia ya Ukristo yanapaswa kuhifadhiwa

Kulinda moyo dhidi ya hofu: Kardinali pia alisisitiza kwamba kuhifadhi uwepo wa Kikristo kunahitaji kulinda moyo dhidi ya hofu, kukata tamaa na athari za hali ngumu. "Lakini tunataka kubaki kama jumuiya iliyo na uhai, bila kuacha haki zetu, haki yetu ya kuishi," alisema. "Kwa hivyo muwe na ujasiri. Msiogope." Kardinali Pizzaballa pia alisema kwamba anafuatilia maendeleo huko Taybeh kwa karibu kupitia masasisho ya mara kwa mara kutoka kwa Padre Bashar. Ziara ya Patriaki ilifanyika katika muktadha wa amri ya Israeli iliyotolewa mwezi Julai iliyopita ikitangaza "eneo la Taybeh na Rimon" kuwa eneo la kijeshi lililofungwa, na kuwazuia Waisraeli na raia wa kigeni kuingia au kubaki huko.

Kardinali Pizzaballa wakati wa Ibada ya Misa Takatifu
Kardinali Pizzaballa wakati wa Ibada ya Misa Takatifu

Haja ya uwepo endelevu wa Kikristo: Eneo lililotengwa linajumuisha sehemu ya eneo lililojengwa la Taybeh, ardhi ya kilimo, na maeneo ya kidini na kihistoria. Agizo hilo pia limeibua maswali kuhusu ufikiaji wa Taybeh kwa mahujaji, wageni, waandishi wa habari, watu wa kujitolea na raia wengine wa kigeni. Kardinali Pizzaballa alisema kwamba kinachoendelea Taybeh kinazidi kujulikana zaidi ya mji wenyewe. Kwa kuzingatia hili, Kardinali Pizzaballa alisisitiza, "Mfano wao ni muhimu, ili tuweze kuendelea kuwa sauti ya Kikristo katikati ya hali hii ngumu sana."

Kard Pizzaballa Yaybeh

 

26 Agosti 2026, 11:16