Baada ya kifo.Papa Leo XIV:karibu mtu anaweza kusikia sauti yake tena!
Isabella H. de Carvalho –Vatican.
Chapisho "ambalo karibu linaturuhusu kusikia sauti ya Papa Francisko tena," na "tunamshukuru Bwana kwa yote ambayo ametupatia kupitia kwake." Haya ni maneno ambayo Papa Leo XIV anamkumbuka mtangulizi wake, ambaye aliaga dunia mnamo Aprili 21, mwaka huu katika barua inayoonekana kwenye kitabu cha Papa Francisko baada ya kifo chake, chenye kichwa: "Mtakatifu wangu Francis," ambayo ni matunda ya mazungumzo yaliyofanyika katika miezi ya mwisho ya mwaka 2024 na Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu.
Kitabu hiki (Toleo la Messaggero Padova, kurasa 160), ambacho pia kina dibaji ya Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, kinarudisha uhusiano wa kina kati ya Papa Francisko na Mtakatifu Francis wa Assisi ambaye alichukua jina lake. Kitabu hiki kitapatikana katika maduka ya vitabu kuanzia Septemba 18 na kiliwasilishwa alasiri tarehe 11 Septemba 2025 huko Assisi katika Chumba cha Waandishi wa Habari cha Konventi Takatifu, kama sehemu ya tukio la kiutamaduni liitwalo:"The Courtyard of Francis yaani, "Ua wa Fransis." Kardinali Semeraro alikuwepo katika tukio hilo, katika mazungumzo na Ndugu Giulio Cesareo, mkurugenzi wa Ofisi ya Mawasiliano ya Konventi Takatifu na Ndugu Massimiliano Patassini, Mkurugenzi wa wahariri wa Gazeti la 'Messaggero di Sant'Antonio.'
![]()
Uwakilishi wa Kitabu huko Assisi
Papa Leo XIV:Utume wake kuanzia na Chaguo jina lake
Katika barua iliyoandikwa kunako tarehe 22 Mei, katika siku kuu ya Mtakatifu Rita wa Cascia, Papa Leo XIV anamshukuru kwa sababu za Watakatifu kwa chapisho hilo na anasisitiza jinsi ambavyo Papa Francisko sio tu "alichukua" jina hilo, "lakini pia alitaka kujitambulisha nalo, na kulifanya kuwa uso wa utume wake mpya." Zaidi ya hayo, katika maandishi hayo, yaliyoandikwa mwezi mmoja baada ya kifo cha Papa Bergoglio, Papa Leo XIV alisisitiza kwamba "matokeo yaliyosababishwa na kifo chake bado haijatoweka kutoka katika roho zetu, mada ambayo pia inashughulikiwa katika kitabu. Papa Leo XIV, kiukweli, ananukuu jibu la Papa wa Argentina kwa swali, kama alikuwa na hofu ya kufa: "Unapokuwa mzee, unatambua kwamba mwisho sio muda mrefu, na kisha inakuwa neema ya kuwa na uwezo wa kujiandaa kwa ajili ya kifo, kuwa na uwezo wa kusoma tena maisha yako ya nyuma, kumshukuru Bwana kwa yote ambayo ametupatia."
Kardinali Parolin:Matokeo ya Mtakatifu Francis katika Maisha ya Bergoglio
"Wakati mtu anashikamana na mtakatifu, ni kwa sababu mtu humgundua kama rafiki na chanzo cha msukumo" ili "kuishi Injili kwa furaha," na "hivi ndivyo ilivyotokea kwa Papa Francisko " na Maskini wa Assisi, anaandika Kardinali Parolin katika utangulizi wa kitabu hicho. Kwa upande wa Kardinali, ushawishi wa Mtakatifu huyu juu ya Jorge Mario Bergoglio unaweza kuonekana "katika mikunjo ya uwepo wake, katika tabia yake, katika chaguzi alizopendelea, katika mapenzi na matamanio yake, hata katika mikutano na matukio aliyopitia."
Katika kitabu hicho, Papa Francisko anakumbukwa nyakati na mang’amuzi mbalimbali kutoka katika maisha yake na “inaonekana karibu kufurahia matokeo ya baraka ambazo mfano wa Mtakatifu Francis ulikuwa umeziacha katika nafsi yake, ukimsaidia kuwa kama yeye kidogo, mwenye kumshukuru sana Bwana na mwenye shauku ya kugundua uwepo wake katika maskini, kumpenda katika wale wanaoteseka na walio peke yao. Hakika, kwa Katibu Mkuu wa Vatican, "ushuhuda" huu uliokusanywa katika miezi ya mwisho ya maisha ya Papa Fransisko ni karibu na "agano lake la kiroho" linalojumuisha kumbukumbu hai na shukrani. Mtazamo wa Papa katika siku za mwisho wa maisha yake pia unaonekana "kupatana" na furaha na shukrani kwa Mungu ambayo Mtakatifu wa Assisi aliionesha alipokuwa akikaribia mwisho wa maisha yake.
![]()
Uwakilishi wa Kitabu: "Mtakatifu wangu Francis"
Kardinali Semeraro:Mtakatifu Francis, Ufunguo wa Kutafsiri Upapa
Wakati wa mkutano na waandishi wa habari huko Assisi, Kardinali Semeraro alibainisha kwamba "Papa Francisko ameweka ndani sura ya Mtakatifu wa Assisi," na hii ilionekana katika mtindo ambao aliendesha upapa wake na katika mtazamo wake wa hali. "Utakatifu wa Mtakatifu Francis unaweza kuwa ufunguo wa kutafsiri huduma ya Petro," na Jorge Mario Bergoglio(Papa Francisko). Kardinali huyo alitoa mifano ya Nyaraka mbalimbali zilizoandikwa na Papa na kuongozwa na Maskini wawa Assisi, kama vile Laudato Si' na Fratelli Tutti, akieleza kwamba kitabu hicho pia kinagusa mada kama vile mazungumzo na Uislamu na dini nyingine na utunzaji wa kazi ya uumbaji. Kardinali Semeraro pia alitaja msisitizo wa Papa Francisko wa kutazama Ulimwengu kutoka pembezoni, "kuanzia kwa waliotupwa," na kuhamaisha "Kanisa linalotoka nje" kama mtazamo wa "mtindo wa Kifransiskani", kwa sababu husababisha kuelewa ukweli kutoka katika mtazamo tofauti. Papa "kwa namna fulani ameifanya sura ya Mtakatifu Francis wa Assisi kuonekana kama mwongozo kwa Kanisa leo hii," Kardinali Semeraro alisema.
![]()
Kardinali Marcello Semeraro
Kujitolea kwa Amani na Tafakari juu ya Kifo
Mwenyekiti wa Baraza la Kuwatangaza watakatifu aidha alisisitiza dhamira ya Papa Fransisko katika kuleta amani, ambayo Papa Leo XIV aliiendeleza kwa hisia sawa. "Wote wawili walisema hali hii ya kushindwa isitukatishe tamaa ya kuzungumzia amani. Wote wawili walitumia taswira ya mbegu; tunapozungumzia amani, tunapanda mbegu ambazo lazima ziingie kwenye moyo wa mwanadamu tukiwa na imani kwamba zitaota," alisisitiza Kardinali.
Hatimaye, akijibu swali kuhusu ikiwa kulikuwa na kipengele fulani cha maandishi ambacho kilikuwa karibu sana na moyo wake, Kardinali Semeraro alisema kwamba bado “anasukumwa” na mjadala wa kitabu hicho kuhusu kuzeeka na kujitayarisha kwa ajili ya kifo. Aliongeza kuwa mwaka 2024, mwaka ambao kitabu hicho kiliandikwa, hakuweza kufikiria kwamba mwaka uliofuata, Juma moja baada ya kusoma rasimu zilizokuwa tayari, Papa Francis angekufa. "Katika kitabu hicho, pia alizungumza kuhusu hili: kuwa tayari kuondoka na kuungana tena ili kuishi kwa amani."
![]()
Uwakilishi wa Kitabu huko Assisi
