Papa Leo XIV:Fumbo la Jumamosi kuu,kushuka kwa Kristo kuzimu kwa ajili ya wokovu wa binadamu

Kwa mujibu wa mapokeo ya utamaduni,Mwana wa Mungu aliingia katika giza kuu zaidi ili kuwafikia hata wa mwisho kaka na dada zake ili kuweza kuwapeleka juu katika mwanga wake.Katika ishara hiyo,kuna nguvu zote na upendo wa tangazo la Pasaka:“Kifo siyo mwisho wa Neno.”Ni katika Katekesi ya Baba Mtakatifu,Jumatano Septemba 24 kwa waamini na mahujaji waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Mzunguko wa Katekesi kuhusu Jubilei, "Yesu Kristo Tumaini Letu,”  mada ya Katekesi ya nane ya Baba Mtakatifu Leo XIV iliyofanyika Jumatano tarehe 24 Septemba 2025, katika Uwanja wa  Mtakatifu Petro  imejikita na  ‘Pasaka ya Yesu,’  kwa takriban mahujaji 35,000 waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ambapo kabla ya kuanza, kama kawaida Baba Mtakatifu akiwa juu ya kigari chake  alizunguka huku akisimama  kubariki watoto, na hasa baada kusalimiana na baadhi ya waamini na wagonjwa waliokusanyika katika Ukumbi wa Paulo VI na vikundi vingine katika ua la Ukumbu huo.

Waamini wengi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini wengi katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu akianza tafakari yake, alisema kuwa “leo tutafakari juu ya fumbo la Jumamosi Takatifu. Ni siku ya Fumbo la Pasaka ambamo utafikiri imesisimama na kimya, wakati kwa hali hali inatimizwa  matendo ya wokovu yasiyoonekana: Kristo anashuka katika ufalme wa mauti ili kupeleka tangazo la Ufufuko kwa wote ambao walikuwa katika giza na kivuli cha kifo. Tukio hili, tulilokabidhiwa kwa liturujia na mapokeo, linawakilisha ishara ya kina na kali zaidi ya upendo wa Mungu kwa wanadamu. Kwa hakika, haitoshi kusema au kuamini kwamba Yesu alikufa kwa ajili yetu: ni lazima tutambue kwamba uaminifu wa upendo wake ulitutafuta pale ambapo sisi wenyewe tulipotea, ambapo ni nguvu tu ya nuru yenye uwezo wa kutoboa eneo la giza linaweza kupenya. Kuzimu, katika dhana ya kibiblia, si mahali kama hali ya kuwepo: hali ambayo maisha yanadhoofika na maumivu, upweke, hatia, na kutengwa na Mungu na wengine hutawala.

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Kristo anatufikia hata katika shimo hili, akivuka malango ya ufalme huu wa giza. Anaingia, kwa njia ya kusema, nyumba yenyewe ya kifo, ili kuiondoa, kuwaweka huru wakazi wake, akiwashika mkono mmoja baada ya mwingine. Ni unyenyekevu wa Mungu asiyesita mbele ya dhambi zetu, ambaye haogopi kukataliwa kabisa kwa ubinadamu. Mtume Petro, katika kifungu kifupi kutoka katika barua yake ya kwanza ambayo tumetoka kuisikia, anatuambia kwamba Yesu, aliyehuishwa na Roho Mtakatifu, alikwenda kupeleka ujumbe wa wokovu “hata kwa roho zilizokuwa kifungoni”(1Petro 3:19).

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@VATICAN MEDIA)

 

Hii ni mojawapo ya picha zinazogusa moyo zaidi, ambazo hazikupatikana katika Injili za kisheria, bali katika maandishi ya apokrifa yanayoitwa Injili ya Nikodemu. Kwa mujibu wa mapokeo ya utamaduni, Mwana wa Mungu aliingia katika giza kuu zaidi ili kuwafikia hata wa mwisho kaka na dada zake ili kuweza kuwapeleka juu katika nuru yake. Katika ishara hiyo, kuna nguvu zote na upendo wa tangazo la Pasaka: “Kifo siyo mwisho wa Neno.” Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa kushuka huku kwa Kristo hakutazami wakati uliopita, lakini unagusa maisha ya kila mmoja wetu. Kuzima hakutazami tu hali ya aliyekufa, lakini hata ambaye anaisha na kifo, kwa sababu ya ubaya na dhambi. Hata ni kuzimu kila siku, kwa upweke, wa aibu, wa kutengwa, na wa ugumu wa kuishi.

Katekesi
Katekesi   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alikazia kusema kuwa Kristo anaingia katika mambo haya yote ya giza ili kushuhudia kwetu upendo wa Baba. Sio kuhukumu, lakini kukomboa. Sio lawama, lakini kuokoa. Yeye anafanya hivyo kwa utulivu, kwa kunyata, kama mtu anayeingia kwenye chumba cha hospitali ili kutoa faraja na usaidizi. Mababa wa Kanisa, katika kurasa za uzuri wa ajabu, walielezea wakati huu kama mpambano: ule kati ya Kristo na Adamu. Mkutano ambao unaashiria mikutano yote inayowezekana kati ya Mungu na mwanadamu. Bwana hushuka pale ambapo mwanadamu amejificha kwa hofu, na kumwita kwa jina lake, humshika mkono, humwinua, na kumrudisha kwenye nuru. Anafanya hivyo kwa mamlaka kamili, lakini pia kwa utamu usio na kikomo, kama baba aliye na mwana ambaye anaogopa kuwa hapendwi tena. Baba Mtakatifu alisema katika sanamu za Mashariki zinazoonesha Ufufuko, Kristo anaoneshwa akivunja milango ya kuzimu na, akinyoosha mikono yake, akishika mikono ya Adamu na Eva. Hajiokoa tu, harudi kwenye uzima peke yake, lakini anavuta ubinadamu wote pamoja naye.

Katekesi
Katekesi   (@Vatican Media)

Huu ndio utukufu wa kweli wa Mfufuka: ni nguvu ya upendo, mshikamano wa Mungu ambaye hataki kuokolewa bila sisi, lakini pamoja nasi. Mungu asiyefufuka tena bila kukumbatia taabu zetu na kutuinua kwa ajili ya maisha mapya. Jumamosi Takatifu, basi, ni siku ambayo Mbingu hutembelea dunia kwa undani zaidi. Ni wakati ambapo kila kona ya historia ya mwanadamu inaguswa na mwanga wa Pasaka. Na ikiwa Kristo angeweza kushuka hadi sasa, hakuna kitu kinachoweza kutengwa na ukombozi wake. Hata usiku wetu, hata dhambi zetu za kale, hata vifungo vyetu vilivyovunjika. Hakuna wakati uliopita ulioharibiwa sana, hakuna historia iliyohatarishwa kiasi kwamba haiwezi kuguswa na huruma. Papa Leo XIV aliwaelekea Kaka na dada waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na kusema kuwa, kwa Mungu, kushuka sio kushindwa, lakini utimilifu wa upendo wake.

Katekesi
Katekesi   (@VATICAN MEDIA)

 

Sio kushindwa, lakini njia ambayo anaonyesha kwamba hakuna mahali pa mbali sana, hakuna moyo uliofungwa sana, hakuna kaburi lililofungwa sana kwa upendo wake.Hii inatufariji, hii inatutegemeza. Na ikiwa nyakati fulani tunahisi kana kwamba tunagonga mwamba, acheni tukumbuke: hapo ndipo mahali ambapo Mungu anaweza kuanzisha uumbaji mpya. Uumbaji ulioundwa na watu walioinuliwa, wa mioyo iliyosamehewa, ya machozi yaliyokauka. Jumamosi takatifu ni kumbatio la kimya ambalo Kristo anawasilisha viumbe vyote kwa Baba ili kuviweka tena katika mpango wake wa wokovu.

Umati wa waamini katika Katekesi
Umati wa waamini katika Katekesi   (@VATICAN MEDIA)
KATEKESI YA PAPA SEPT 24
24 Septemba 2025, 14:47