Katekesi ya Papa Leo XIV:Kutumaini ni kung’amua

Katika Katekesi ya Jubilei,Jumamosi Septemba 27,Papa alisisitiza juu ya "kuwa wadogo kwa mujibu wa Injili na kufahamu kutumikia ndoto za Mungu.Kuwa na mawazo ya silika ya watoto kwa ajili ya Ufalme wa Mungu kunaamanisha kuwa na nafasi na kudhihirishwa katika akili na Moyo wa Mungu.Walioelimika wanaelewa kidogo kwa sababu wanadhani wanajua kila kitu.Mungu ni rahisi na anajidhihirisha kwa wanyonge."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Hata Jumamosi tarehe 27 Septemba 2025, Uwanja wa Mtakatifu Petro umewaona waamini na mahujaji  wapatao 35elfu ili kushuhudia na kusikiliza Katekesi ya Baba Mtakatifu Leo XIV. Kabla ya saa 4 kamili,  masa ya Ulaya na saa 5 kamili,  masaa ya Afrika Mashariki na Kati,  kuanza Katekesi hiyo, kama kawaida ambapo Papa akiwa ndani ya gari lake jeupe, alizunguka katika Uwanja wa mbele wa Kanisa kuu la Vatican, akisimama ili kubadilishana salamu na kubariki watoto wengi sana, hata kuwabeba mikononi mwake, ishara ya upendo wa ubaba na kwa njia hiyo waliokuwepo walimkaribisha kwa uchangamfu, wakipeperusha bendera nyingi na vikundi vingi viliinua mabango ili kujitambulisha. Baba Mtakatifu alifanya ishara ya Msalaba na kusikiliza Somo lililochaguliwa, kutoka Injili: “Saa hiyo hiyo, Yesu alishangilia katika Roho Mtakatifu na kusema: “Nakushukuru, Baba, Bwana wa Mbingu na dunia, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na akili ukawafunulia wadogo. Ndiyo, Baba, kwa maana ndivyo ulivyokusudia. Vitu vyote vimekabidhiwa kwangu na Baba yangu”(Lk 10:21-22).“Kutumaini ni kung’amua.

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@VATICAN MEDIA)

Kwa njia hiyo "Kutumaini ni kung'amua: Ambrose wa Milano,” ndiyo ilikuwa mada ya Papa Leo XIV kufafanua tafakari ya Katekesi ambapo alisema: Jubilei inatufanya kuwa mahujaji wa matumaini, kwa sababu tunahisi haja kubwa ya kupyaishwa ambayo inatuhusu sisi na dunia nzima. Nilisema tu “tunahisi,”: kitenzi hiki, kuhisi, kinaeleza mwendo wa roho, akili ya moyo ambayo Yesu aliiona hasa kwa watoto wadogo, yaani, katika watu wenye roho ya unyenyekevu.  Mara nyingi, kiukweli, watu walioelimika hawana hisia ya Uelewa kama watoto, kwa sababu wanadhani kujua. Ni vyema, hata hivyo, kuwa na nafasi akilini na moyoni mwa Mungu kujidhihirisha. Kuna kiasi gani cha matumaini wakati utambuzi mpya unapotokea miongoni mwa watu wa Mungu! Yesu anafurahia hili; anajawa na furaha, kwa sababu anatambua kwamba watoto wanahisi. Sensus fidei, yaani wana “maana ya imani,” ambayo ni kama "fahamu ya sita" ya watu rahisi kwa mambo ya Mungu. Mungu ni rahisi na hujidhihirisha kwa wanyonge. Kwa sababu hiyo, kuna kutokukosea kwa watu wa Mungu katika kuamini, kuwa kutokosea kwa Papa ni usemi na huduma (Lumen gentium, 12; Tume ya Kimataifa ya Taalimungu,Maana ya imani Sensus fidei katika Maisha ya Kanisa, 30-40).

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Kuchaguliwa kwa Ambrose

Papa Leo alipenda kukumbusha kipindi katika historia ya Kanisa ambayo inaonesha jinsi tumaini linaweza kutoka katika uwezo wa watu wa kutambua. Katika karne ya nne, huko Milano, Kanisa lilikumbwa na migogoro mikubwa, na uchaguzi wa Askofu mpya ulikuwa ukigeuka na kuwa ghasia za kweli. Mamlaka ya kiraia, Gavana Ambrose, aliingilia kati, na kwa uwezo wake mkubwa wa kusikiliza na kupatanisha, alileta utulivu. Historia hii inakwenda kwamba basi sauti ya mtoto iliinuka na kupiga kelele: "Ambrose, Askofu!" Na hivyo watu wote pia walipiga kelele: "Ambrose, Askofu!" Ambrose wala  hakuwa amebatizwa; alikuwa mkatekumeni tu, yaani katika kujiandaa kwa Ubatizo. Watu, hata hivyo, waliona jambo la maana juu ya mtu huyo na wakamchagua. Hivyo Kanisa lilikuwa na mmoja wa Maaskofu wake wakuu, na Daktari wa Kanisa. Mwanzoni, Ambrose hakutaka, hata akafikia kukimbia. Kisha alielewa kwamba huu ulikuwa wito kutoka kwa Mungu, hivyo akajiruhusu kubatizwa na kuwekwa wakfu wa kiaskofu. Na akawa Mkristo, kwa kuwa Askofu! Papa aliongeza kusema "Je, mnaona ni zawadi gani kubwa ambayo watoto wadogo wametoa kwa Kanisa?"

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Swali la Baba Mtakatifu Leo XIV

Hata leo, hii  Papa leo aliongzea, ni neema ya kuomba: kuwa Wakristo huku wakiishi wito waliopokea! Je, wewe ni mama, baba? Kuwa Mkristo kama mama na baba yako. Je, wewe ni mjasiriamali, mfanyakazi, mwalimu, padre, mtawa? Kuwa Mkristo katika njia yako mwenyewe. Watu wana "silika" hii: wanaelewa kama tunakuwa Wakristo au la. Na wanaweza kutusahihisha, wanaweza kutuonesha mwelekeo wa Yesu. Kwa miaka mingi, Mtakatifu Ambrose alirudisha mengi kwa watu wake. Kwa mfano, alibuni njia mpya za kuimba zaburi, nyimbo, kuadhimisha misa, na kuhubiri. Yeye mwenyewe alijua jinsi ya kuelewa na hivyo matumaini kuongezeka. Mtakatifu Agostino aliongoka kwa mahubiri yake na kubatizwa naye. Hisia hii ya ndani ni njia ya kutumaini, tusisahau hilo!” Papa alishauri. Kwa njia hiyo,  hata Mungu hulisogeza Kanisa lake mbele, akionesha njia zake mpya. Kung’amua ni silika ya watoto kwa Ufalme ujao. Jubilei itusaidie tuwe wadogo kadiri ya Injili, ili kufahamu na kutumikia ndoto za Mungu!

Katekesi papa 27 Septemba
27 Septemba 2025, 10:47