"Leo kutoka Chicago,"vyombo vya habari vya Vatica vyachimbua mizizi ya Papa Leo XIV huko Marekani

"Leo kutoka Chicago,"filamu ya hali halisi itakayokuja hivi karibuni kwenye vyombo vya Vatican,itawapa watazamaji taswira ya karibu ya maisha ya awali ya Papa Leo XIV huko Marekani,kuanzia ushuhuda wa kaka zake Louis na John,pamoja na sauti na historia nyingi zilizosimuliwa na wale walio karibu zaidi na mtu ambaye,tangu Mei 8, 2025,analiongoza Kanisa Katoliki duniani kote.

Vatican News

Utoto, mahusiano ya kifamilia, urafiki, masomo, elimu, wito, hatua za kwanza katika maisha ya kuwekwa wakfu, kujitolea kwa kijamii, shauku za michezo, na ladha ya chakula. Filamu ya hali halisi "Leo kutoka Chicago" inatoa picha ya kina na, kwa njia fulani, ya Papa Leo XIV isiyo na kifani. Uzalishaji kwa upande wa Kurugenzi ya Uhariri ya Baraza la Kipapa la Mawasiliano, kwa ushirikiano na Jimbo Kuu la Chicago na Apostolado El Sembrador Nueva Evangelización (ESNE), ilifuatilia historia, hadi mizizi, ya Papa wa sasa katika nchi yake ya asili: Marekani.

Safari hiyo, iliyofanywa na waandishi wa habari Deborah Castellano Lubov, Salvatore Cernuzio, na Felipe Herrera-Espaliat, inapitia vitongoji vya Chicago, ikianzia kwenye nyumba ya familia katika eneo la kitongoji cha Dolton, na kumbukumbu na historia za ndugu wake wawili, Louis Martin na John. Kisha kuna ofisi, shule, na parokia zinazoongozwa na Waagostinian; Umoja wa Kitaalimungu wa Kikatoliki; na maeneo yaliyotembelewa na Padre  wakati huo Robert Francis Prevost, kama vile Uwanja wa Aurelio na Rate Field, Uwanja wa White Sox. Lakini ratiba inaenea hadi Chuo Kikuu cha Villanova, Kilomita chache kutoka Philadelphia, na Port Charlotte (Florida), makazi ya kaka yake mkubwa.

Robert Francis Prevost bambino, studente, giovane sacerdote

Robert Francis Prevost mtoto,mwanafunzi na padre kijana

Takriban mashuhuda 30 wanaohusishwa na Papa wa sasa, kupitia historia, picha, na filamu, wanasaidia waraka huu kutafakari kwa undani sura ya mtu aliyeitwa kuliongoza Kanisa la Ulimwengu mnamo tarehe 8 Mei 2025. Mwanamume ambaye, hata alipokuwa mtoto, alionesha mwelekeo wa maisha ya kidini, akicheza kuadhimisha Misa na kusali sala katika Kilatini; ambaye, katika umri mdogo sana, alikumbatia mchakato wa utambuzi wa kuingia Shirika la Mtakatifu Agostino; ambaye alichukua masomo ya hisabati na Kitaalimungu, akianzisha uhusiano wa kweli na wanafunzi wenzake na pia kushiriki katika mipango ya kusaidia maisha.

Mwanamume aliyeiacha nchi yake kuelekea Peru na ambaye aliongoza mojawapo ya vikundi vya kitawa vilivyoenea sana ulimwenguni kwa uongozi mtulivu na wenye maamuzi. Mwanamume aliyesikiliza muziki wa miaka ya 60 na 70, aliyependa kuendesha gari, aliyetazama TV, na aliyefuatilia mchezo wa baseball.

"Leo kutoka Chicago" ni filam inayofuata ile filamu ya hali halisi ya "León de Perú," yaani Leo wa Pero" iliyowasilishwa mwezi Juni, iliyopita, kuhusu miaka ya umisionari wa Prevost katika nchi ya Amerika Kusini. Itachapishwa hivi karibuni kwenye idhaa za Vatican.

Tazama filamu kuhusu maisha ya Papa Leo wakati alikuwa Askofu wa Peru
Filamu mpya ya Papa Leo XIV
13 Septemba 2025, 18:27