2025.09.14 Inaonesha miaka 70 ya kuzaliwa kwa Papa Leo XIV kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro. 2025.09.14 Inaonesha miaka 70 ya kuzaliwa kwa Papa Leo XIV kwa waamini na mahujaji waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.  (@VATICAN MEDIA )

Miaka 70 ya kuzaliwa kwa Papa:Asante wazazi na walionikumbuka katika sala

Mara baada ya kusali sala ya Malaika wa Bwana,Papa aliyezaliwa huko Chicago,Illinois,tarehe 14 Septemba 1955,aliwasalimia wote waliomuonesha mapendo yao katika siku yake ya kuzaliwa.Mabango yalionesha matashi mema katika kila lugha na kutoka ulimwenguni kote.Papa amekumbusha kuwa "Septemba 15 ni miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu kwa mujibu wa Papa Mtakatifu Paulo VI."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mara baada ya Tafakari na sala ya Malaika wa Bwana, tarehe 14 Septemba 14, Baba Mtakatifu alisema kuwa:  Wapendwa kaka na dada, kesho (15 Septemba 2025) ni kumbu kumbu ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Sinodi ya Maaskofu, wazo la kinabii la Mtakatifu Paulo VI, ili Maaskofu waweze kufanya ushirika mkubwa na bora zaidi na Mrithi wa Petro.” Papa aliongeza: “Ninatumaini kwamba maadhimisho haya yatahamasisha kujitolea upya kwa umoja, sinodi, na utume wa Kanisa.”

Sinodi ya Maaskofu inafikisha miaka 60 tarehe 15 Septemba 2025
Sinodi ya Maaskofu inafikisha miaka 60 tarehe 15 Septemba 2025   (@Vatican Media)

Papa alitoa  salamu zake  za upendo kwa wote, waamini wa Roma na mahujaji kutoka Italia na nchi mbalimbali, hasa wale wa Villa Alemana na Valparaíso, Chile, kutoka Jimbo kuu la Mwanza, Tanzania, na Humpolec, Jamhuri ya Czech; Waperu wa Jumuiya ya Kidini ya Yesu wa  Nazareti  Cautivo. Kisha waamini wa Chiaiamari, Anitrella, Uboldo, Faeto, Lesmo, Trani, Faenza, Pistoia, Mtakatifu Martino huko Sergnano, Guardia ya  Acireale, Mtakatifu Martino wa Ngazi huko Palermo, na Alghero.

Un gruppo di fedeli in piazza San Pietro per l'Angelus

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana  (@VATICAN MEDIA)

Pia bendi za muziki za Borno na Sonico huko Val Camonica, Chama cha  "La Nuova Famiglia" cha Monza, Kamati ya Pro Loco ya Mkoa wa Lazio, Umoja wa Utume wa Kikatoliki, vijana wa Don Bosco, na Jumuiya ya Chama cha Ukombozi cha Roma; pamoja na Chama cha Sanaa na Ufundi cha Mtakatifu Agata wa Militello, waendesha pikipiki kutoka Ravenna, na waendesha baiskeli kutoka Rovigo.

"Happy Birthday!". Un augurio nella lingua madre di Papa Prevost.

"Happy Birthday!" Kumtakia heri Papa Prevost kwa lugha ya kiingereza. (@VATICAN MEDIA)

Papa ameshukuru kupewa heri za kuzaliwa kwake

Wapendwa, inaonekana mnajua kuwa leo ninatimiza miaka sabini. Ninamshukuru Bwana na wazazi wangu; na ninawashukuru wale ambao wamenikumbuka katika maombi yao. Asanteni nyote sana! Asante! Dominika Njema. Ikumbukwe Papa Leo XIV  alizaliwa huko Chicago, Illinois, tarehe 14 Septemba 1955. Katika Uwanja wa Mtakatifu Petro kila watu walionesha  Mabango mengi yenye matakwa mema  katika kila lugha na kutoka ulimwenguni kote.

Uno striscione di auguri per il Papa

Matashi mema kwa lugha ya kihispania   (@VATICAN MEDIA)

Baada ya Angelus Septemba 14
14 Septemba 2025, 15:23