Papa Leo XIV:familia ni wimbo wa matumaini&umaskini na vita uhatarisha hadhi yake
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV alieleza safari kwa wakati ujao wa familia, kwa washiriki wa Mkutano wa Jubilei, ulioandaliwa siku hizi jijini Roma na Baraza la Maaskofu Amerika Kusini(CELAM), kwa kushirikiana na Taasisi ya Kipapa ya Maisha na ya Yohane Paulo II. Na kwa njia hiyo Tukio hilo lilifanyika Makaio Makuu ya Taasisi ya Kipapa ya Taalimungu ya Yohane Paulo II ambayo inajikita hasa na mafunzo ya familia , lakini kwa kwa namna ya pekee, Mkutano huo ulioongozwa na mada ya “changamoto zinazokabiliwa na familia katika pembezoni mwa dunia hasa kwa Amerika Kusini, na Visiwa vya Carribiean, katika mazungumzo na dini nyingine duniani.” Kwa njia hiyo katika hotuba ya Papa alionesha furaha ya kuwakaribisha katika nyumba ya Petro, Nyumba ya Kanisa, ambapo lazima sote tujisikie kama familia moja kubwa, iliyokusanyika karibu na moto wa upendo wake. Umejihusisha na mazungumzo siku hizi kufuatia mbinu ya sinodi, ukitafakari baadhi ya masuala ya sasa kuhusu maisha ya familia.
Jubilei ya Matumaini ni safari kuelekea kukutana na kweli ambayo ni Mungu mwenyewe. Yesu, mwanzoni mwa utume wake, anaelezea Jubilei hii kuwa ni mwaka wa neema (rej.Lk 4:19) na, baada ya ufufuko, anawaalika wanafunzi wake "kurudi Galilaya" (taz. Mt 28:10). Hatupaswi kuanguka katika hatari ya kuweka maisha yetu juu ya dhamana za kibinadamu na matarajio ya kidunia. Katika nyanja ya kijamii, tunaweza kutafsiri jaribu hili kuwa jaribio la "kupitia tu," kama Mtakatifu Pier Giorgio Frassati alivyosema (rej.Barua kwa Isidoro Bonini, Februari 27, 1925). Wakati huo huo, Papa alisema, tunafahamu kwamba leo kuna vitisho vya kweli kwa heshima ya familia, kama vile matatizo yanayohusiana na umaskini, ukosefu wa ajira na upatikanaji wa huduma za afya, unyanyasaji wa watu walio hatarini zaidi, na uhamiaji, na vita (taz. Francisko,Wosia wa Post- Amoris Laetitia,44-46). Taasisi za umma na Kanisa zina wajibu wa kutafuta njia za kukuza mazungumzo na kuimarisha vipengele hivyo katika jamii vinavyopendelea maisha ya familia na elimu ya washiriki wake (taz. Mtakatifu Yohane Paulo II, Barua ya Sollectudo Rei Socialis,8).
Papa Leo aliendelea kusisitiza kuwa, kwa mtazamo huu, tunaweza kuelewa familia kama zawadi na kazi. Ni muhimu kukuza uwajibikaji pamoja na umaarufu wa familia katika maisha ya kijamii, kisiasa na kitamaduni, kukuza mchango wao muhimu kwa jamii. Katika kila mtoto, katika kila mwanandoa, Mungu anatukabidhi kwa Mwanawe, kwa Mama yake, kama alivyofanya kwa Mtakatifu Yosefu, kuwa pamoja nao, msingi, chachu na ushuhuda wa upendo wa Mungu kati ya wanadamu. Kuwa Kanisa la nyumbani na makaa ambapo moto wa Roho Mtakatifu unawaka, kueneza joto lake kwa wote na kuwaalika kwa tumaini hili.
Mtakatifu Paulo wa sita katika mahubiri yake mashuhuri huko Nazareti, alituasa kuiga mfano wa Familia Takatifu, kwa kuwasindikiza na kuwaunga mkono wengine katika ukimya, kazi na sala, ili Mwenyezi Mungu aweze kutimiza ndani yao mpango wa upendo aliouweka kwa ajili yao. Huu ni upendo unaomwilishwa katika kila maisha yanayozaliwa kwa imani kwa njia ya ubatizo na kupakwa mafuta "kutangaza mwaka wa neema" kwa wanaume na wanawake wote, ambao watakutana na Yesu katika Ekaristi na katika sakramenti ya msamaha, ambao watamfuata katika utume wake kama kuhani, kama baba wa Kikristo, au kama mtu aliyewekwa wakfu, hadi mkutano wa uhakika, hadi lengo la tumaini letu.
Jubilei ni furaha isiyo na maneno ,furaha zaidi ya yote isiyoelezeka
Papa Leo kwa hitimisho la tafakari hiyo aliongeza kuwa lazima liwe wito wa kujitoa na kwa furaha ile iliyofurika iliyojaa wanafunzi walipokutana na Yesu Mfufuka na kuwaongoza kutangaza jina lake duniani kote. Mtakatifu Agostino aliifafanua hii “Jubilei” kuwa ni furaha isiyo na maneno, furaha ambayo, zaidi ya yote, inafaa kwa isiyoelezeka (taz. Tafakari ya Zaburi 94:3). “Familia zetu ziwe wimbo huo wa kimya wa matumaini, wenye uwezo wa kueneza nuru ya Kristo kwa maisha yao, “ili furaha ya Injili ifikie miisho ya dunia na pasiwepo pembezoni inayonyimwa mwanga wake” (Papa Francisko Evangelii Gaudium, n. 288). Baba Mtakatifu anawakabidhi wote kwa maombezi ya Familia Takatifu ya Nazareti, kielelezo kamili ambacho Mungu anatoa katika kujibu kilio cha familia cha kutaka msaada. Kwa kuwaiga, nyumba zetu zitakuwa taa zinazowashwa na nuru ya Mungu. Bwana awabariki. Asante.
