Papa Leo XIV:Ni pale,ambapo mtu ameteswa sana,upendo mkuu unafunuliwa!

Kila kilio cha maumivu,ikiwa kimekabidhiwa kwa Mungu,si ishara ya udhaifu;haijapuuzwa kamwe;kinyume chake,ina thamani kubwa sana.Hata katika ukimya,wakati yote yanaonekana kupotea,Mungu yupo,anatukumbusha:kilio cha mwanadamuni njia ya kuepuka kujitoa kwa wasiwasi na kwamba Ulimwengu mwingine unawezekana.Katika mtihani uliokithiri tunajifunza kilio cha matumaini.Ni katika Tafakari ya Papa Leo XIV,Jumatano Septemba 10 kwa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika Mzunguko wa Katekesi ya Jubulei 2025, Yesu Kristo Matumaini yetu: Pasaka ya Yetu,” Baba Mtakatifu Leo XVI amejikita na tafakari kuhusu “Kifo” kwa kuongoza na kifungu cha Injili ya Marko kisemacho: “Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho”(Mk 15,37). Alianza kuwasalimia na “kuwashukuru kwa uwepo wao na kwamba ni ushuhuda mzuri,” akiwageukia  watu zaidi ya 35 elfu waliukasanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican,  licha ya mvua iliyokuwa ikinyesha kidogo kidogo,  lakini kwa kushikilia miavuli na kuvaa makoti ya mvua.

Kwa njia hiyo Papa alisema: “Leo tunatafakari kilele cha maisha ya Yesu katika ulimwengu huu: kifo chake msalabani. Injili zinabainisha jambo muhimu sana, ambalo linastahili kitafakariwa kwa akili ya imani. Juu ya Msalaba, Yesu hakufa kwa kimya. Yeye hazimiki pole pole, kama mwanga unavyofifia, bali anaonesha maisha kwa kilio: Yesu kwa pumzi kuu alikata roho “(Mk 15,37). ) Kilio hicho kina kila kitu: maumivu, kuachwa, imani, sadaka. Sio tu sauti ya mwili kukata tamaa, lakini ishara ya mwisho ya maisha kusalimu amri.

Katekesi ya Papa Leo XIV
Katekesi ya Papa Leo XIV   (@Vatican Media)

Kilio cha Yesu kimefuatwa na swali moja  ya kile  ambacho kinaweza kuumiza sana kutangazwa: Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Ni moja ya aya ya Zaburi ya 22, lakini juu ya mdomo wa Yesu inachukua uzito wa kipekee. Mwana ambaye daima aliishi kwa undani wa muungano na Baba, anafanya uzoefu sasa wa kimya, wa kutokuwapo,  wa kuzima. Huu siyo mgogoro wa imani, lakini ya hatua ya mwisho ya upendo unaojitoa kabisa. Kilio cha Yesu siyo cha kusumbuka, bali cha uwazi, ukweli uliochukuliwa hadi kikomo, imani ambayo inavumilia hata wakati yote yananyamaza. Katika wakati ule anga likawa jeusi na pazia la hekalu lilipasuka(Mc 15,33.38).

Ni kama vile muumbaji mwenyewe, anashiriki kwa uchungu ule, na pamoja anaonesha kitu kipya: Mungu haishi tena nyuma ya pazia, uso wake sasa unaonekana kamili katika Msulibiwa. Ni pale, katika mtu huyo aliyeteswa sana, kwamba upendo mkuu unafunuliwa! Hapo ndipo tunaweza kumtambua Mungu ambaye habaki mbali, lakini anayepenya maumivu yetu hadi kiini kabisa. Askari, mpagani, alimuelewa. Si kwa sababu alikuwa amesikia hotuba zake, bali kwa sababu aliona Yesu anakufa kwa namna hiyo na kusema “Hakika mtu huyo alikuwa ni Mwana wa Mungu (Mk 15,39).

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Ni ungamo la kwanza la imani baada ya kifo cha Yesu. Ni matunda ya kilio ambacho hakikupotezwa na upepo, lakini kiligusa moyo. Wakati mwingine, kile ambacho hatuwezi kueleza kwa maneno, tunaeleza kwa sauti zetu. Moyo ukijaa hulia. Na hii sio daima ishara ya udhaifu; inaweza kuwa tendo kubwa la ubinadamu. Tumezoea kufikiria kilio kama kitu kisichodhibitiwa, cha kukandamizwa. Injili inatoa thamani kubwa juu ya kilio chetu, ikitukumbusha kwamba inaweza kuwa maombi, kupinga, hamu na kujisalimisha. Na hata kuwa mtindo wa salamu kali sana, wakati hatuna maneno zaidi. Wakati wa kilio hicho,  Yesu alikuwa ameweka yote aliyokuwa nayo: upendo wake wote, na matumaini yake yote. Ndiyo, kwa sababu hii pia iko katika kulia: tumaini ambalo linakataa kukata tamaa. Unapiga kelele wakati unaamini kuwa mtu anaweza kukusikiliza. Unapiga kelele si kwa kukata tamaa, bali kwa shauku.

Licha ya Mvua waamini walikuwapo katika Katekesi
Licha ya Mvua waamini walikuwapo katika Katekesi   (@Vatican Media)

Yesu hakupaza sauti dhidi ya Baba, bali kuelekea Yeye. Hata katika kimya, alikuwa na uhakika kwamba Baba alikuwa pale. Na kwa hivyo alituonesha kwamba tumaini letu linaweza kulia, hata wakati yote yanaonekana kupotea. Kulia basi inakuwa ishara ya kiroho. Sio tu tendo la kwanza la kuzaliwa kwetu—tunapokuja ulimwenguni tukilia—pia ni njia ya kubaki hai. Tunalia tunapoteseka, lakini pia tunapopenda, tunaita, tunaomba. Kulia ni kusema kwamba tuko hapa, kwamba hatutaki kufifia katika ukimya, kwamba bado tuna kitu cha kutoa. Katika safari ya maisha, kuna wakati ambamo kuweka yote ndani inaweza kutumaliza tararibu. Yesu anatufundisha kutokuwa na hofu ya kupiga kelele, cha msingi iwe kweli, unyenyekevu, na mwelekeo kwa Baba. Kilio hakifai kamwe ikiwa kinatoka katika upendo. Na kamwe hakipuuzwi ikiwa kimekabidhiwa kwa Mungu. Ni njia ya kujiepusha na ubishi, kuendelea kuamini kwamba ulimwengu mwingine unawezekana.

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV, alisisitiza kuwa na tujifunze jambo hili kutoka kwa Bwana Yesu: tujifunze kilio cha matumaini saa ya majaribu makali sana ifikapo. Sio kuumiza, lakini kuamini. Sio kupiga kelele kwa mtu, lakini kufungua mioyo yetu. Ikiwa kilio chetu ni cha kweli, kinaweza kuwa kizingiti cha nuru mpya, ya kuzaliwa upya. Kuhusu Yesu: wakati kila kitu kilionekana kuisha, wokovu ulikuwa karibu kuanza. Ikioneshwa kwa imani na uhuru wa watoto wa Mungu, sauti ya uchungu ya ubinadamu wetu, ikiunganishwa na sauti ya Kristo, inaweza kuwa chanzo cha matumaini kwetu na kwa wale wanaotuzunguka.

Kabla ya katekesi ya Papa, ilizomwa Injili: “Na ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa. Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni, na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini. Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.(Mk 15,33-39).

Katekesi ya Papa
Katekesi ya Papa   (@VATICAN MEDIA)
Katekesi ya Papa 10 Septemba
10 Septemba 2025, 11:54